26 March 2013
WAMA yapongezwa kwa kusaidia wanawake
Na Anna Nkinda, Maelezo
MKE wa Rais wa China Mama Peng Liyuan, amezipongeza kazi zinazofanywa na Mke wa Rais Tanzania, Mama Salma Kikwete kupitia taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA).
Mbunge kuweka umeme shule za Chalinze
Na Omary Mngindo, Chalinze
MBUNGE wa Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Said Bwanamdogo, anataraji kugawa vifaa vinavyozalisha umeme unaotumia mionzi ya jua (sola), katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo jimboni kwake.
Viongozi wa dini waombea mradi wa maji
Na Steven William, Muheza
VIONGOZI wa dini ya Kikristo na Kiislamu, katika Kijiji cha Lusanga, Wilaya Muheza, mkoani Tanga, wameshiriki katika
ibada ya kuombea mradi wa kisima kirefu cha maji ili ujenzi
wake uweze kukamilika haraka na kuwasaidia wananchi.
Uwamsho wasomewa mashtaka upya
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uwamsho, jana imeanza kusomwa upya katika Mahakama Kuu ya Zanzibar,
mbele ya Jaji Fatma Hamid Mohmoud.
Tuilinde amani yetu kuvutia wawekezaji kutoka China
RAIS wa China Xi Jinping, jan alimaliza ziara yake ya siku mbili nchini na kusisitiza umuhimu wa nchi hizo, kuendeleza uhusiano uliodumu muda mrefu.
20 March 2013
Bunduki yatumika kuombea rushwa *Wananchi walalamika kubambikiwa kesi na polisi *Viongozi CCM wataka iundwe tume kuchunguza
Na Mwandishi Wetu, Tabora
BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, wamelalamikia kitendo cha baadhi ya askari wa vituo vya polisi Usinge na Kaliua, kuomba rushwa kwa mtutu wa bunduki.
BAADHI ya wananchi katika Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, wamelalamikia kitendo cha baadhi ya askari wa vituo vya polisi Usinge na Kaliua, kuomba rushwa kwa mtutu wa bunduki.
Papa asimikwa,atoa ujumbe mzito
ROME, Italia
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I, jana amesimikwa rasmi kutumikia wadhifa huo na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi mbalimbali, kuwalinda wanyonge na masikini.
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I, jana amesimikwa rasmi kutumikia wadhifa huo na kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi mbalimbali, kuwalinda wanyonge na masikini.
Kikwete aomboleza kifo cha trafiki
Na Jesca Kileo
RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuomboleza kifo cha askari WP 2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari juzi mchana katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam.
RAIS Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema, kuomboleza kifo cha askari WP 2494 Koplo Elikiza ambaye amepoteza maisha kwa kugongwa na gari juzi mchana katika eneo la Bamaga, Dar es Salaam.
Hukumu wafuasi a ponda
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kesho inatarajia kutoa hukumu ya washtakiwa wa kesi ya kufanya maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), inayowakabili wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kesho inatarajia kutoa hukumu ya washtakiwa wa kesi ya kufanya maandamano haramu kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), inayowakabili wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda.
Kituo kikubwa cha kuzalisha gesi kujengwa nchini
OSLO, Norway
KAMPUNI za Statoil na BG Group, zinatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 10 kujenga kituo cha kuzalisha na kusafisha
gesi ya asili nchini Tanzania ili kuiuza Asia.
19 March 2013
Lwakatare apanda kortini kwa ugaidi *Akabiliwa na mashtaka manne, anyimwa dhamana *Mawakili wake wakwama, Machi 20 kurudi tena
Na Grace Ndossa
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana limewafikisha kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Wilfred Lwakatare pamoja
na Bw. Ludovick Joseph.
JK: Nataka hospitali ya wazazi Dar
Rachel Balama na Rehema Mohamed
RAIS Jakaya Kikwete, ameziagiza Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kujenga hospitali ya wazazi ya Mkoa ili kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika baadhi ya hospitali.
NCCR-Mageuzi wamsamehe Kafulila
Na Mwajabu Kigaza, Kigoma
MBUGE wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. David Kafulila, amekiri kufanya kosa la utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho na kusababisha uongozi kutaka kumvua uanachama.
IGP Mwema: Leteni taarifa za uhalifu tuzifanyie kazi
Na Anneth Kagenda
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amewataka wananchi na waandishi wa habari, kutozungumzia na kuandika matukio ya uhalifu ambayo upelelezi wake haujakamilika badala yake kama wana taarifa zozote, waziripoti Kituo cha Polisi ili
ziweze kufanyiwe kazi.
Papa mpya kusimikwa rasmi leo
ROME, Italia
VIONGOZI mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki misa ya kusimikwa kwa Papa mpya wa kanisa hilo duniani Francis I ambayo itafanyika leo Vatican.
Trafiki agongwa, afa akiwa kazini Dar
Na Waandishi Wetu
ASKARI wa Kitengo cha Usalama Barabarani, WP 2492 Elikiza Nko, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari yenye namba
T 328 BML, aina ya Land Rover Discover, mali ya Kanisa la
TAG wakati akiongoza msafara wa Rais Jakaya Kikwete.
Marekani kupambana na rushwa nchini
Na Godfrey Ismaely
BALOZI wa Marekani nchini, Bw. Alfonso Lenhardt, amesema kuanzia sasa Serikali yake itashiriki kikamilifu kupambana na rushwa nchini hasa kwa viongozi.
Moat yaitaka Serikali kutumia analojia, digitali
Na Goodluck Hongo
WAMILIKI wa Vyombo vya Habari Nchini (Moat) wameitaka Serikali kutumia mifumo yote miwili ya analojia na digitali kwa wakati mmoja hadi kufikia mwaka 2015 ambapo itakuwa mwisho wa kutumia analojia.
DAWASA ina mpango wa kuongeza mitambo
Na Darlin Said
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ina mpango wa kuongeza mitambo mikubwa ya maji taka mipya mitatu ya kusafisha mfumo wa maji kwa ajili ya kutatua tatizo la maji jijini Dar es Salaam.
Utumishi yaonya matangazo feki ya ajira
Na Peter Mwenda
SEKRETARIETI ya Ajira imeonya kuwa wao pekee ndiyo wenye jukumu la kutoa matangazo mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais,Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam ilisema kuwa matangazo yanayochapishwa au kuandikwa katika mitandao ya kijamii hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Madawa ya kulevya bado yanaingizwa nchini- Nzoa
Na Veronica Ikonga
JESHI la Polisi nchini limewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapoona ama kuwahisi watu wanaojihusisha na uingizaji dawa ya kulevya nchini watoe taarifa sehemu husika.
Chadema :Hatutoki tena Bungeni
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
WABUNGE wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametangaza kubadili utaratibu wao wa kutoka nje ya vikao vya Bunge kutokana na kutoridhishwa na baadhi ya mambo na badala yake sasa watakuwa wakikomaa ndani mpaka kieleweke.
Kamati yawarejesha walioacha tiba ya VVU
Na Pendo Mtibuche,Dodoma
KAMATI ya afya katika Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na programu ya Tunajali imeanzisha mkakati wa kuwarejesha kwenye tiba watu 5,358 wanaoishi na VVU (WAVIU) ambao walipotea na kuacha huduma hizo mkoani hapa.
Polisi yawashikilia tisa kwa ujambazi
Na Masau Bwire, Bagamoyo
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia watu tisa wanaodaiwa kuwa majambazi baada ya kupora sh.milioni 7.5 na kuwajeruhi familia kwa kuwakataka kata mapanga.
CCM wagawanyika makundi Shinyanga
Na Suleiman Abeid,Shinyanga
SAKATA la kuachishwa uongozi kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga mjini, Charles Shigino limepokelewa kwa mawazo tofauti na wanachama wa CCM mjini hapa huku wengi wakipinga maamuzi hayo na wengine wakiunga
mkono.
Sote tuwajibike kukomesha tatizo la mimba shuleni
TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.
Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinathibitisha kuwa tatizo hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku hasa baada ya kuanzishwa shule za kata.
18 March 2013
Majambazi yapora gari, milioni 200/-*Wachina wanne wajeruhiwa,msako mkali waanza *TANROADS YADAI FEDHA ZILIZOPORWA NI MIL.7.9
Na Eliasa Ally, Iringa
MAJAMBAZI 10 wakiwa na bunduki tatu pamoja na mapanga, wamevamia kambi ya Mkandarasi wa Kampuni ya SIETCO kutoka nchini China, iliyopo eneo la Igingilanyi, mkoani Iringa na kupora fedha taslimu sh. milioni 100, dola za Marekani 11,560, euro 54,910 na kuwajeruhi wachina wanne kwa mapanga.
MAJAMBAZI 10 wakiwa na bunduki tatu pamoja na mapanga, wamevamia kambi ya Mkandarasi wa Kampuni ya SIETCO kutoka nchini China, iliyopo eneo la Igingilanyi, mkoani Iringa na kupora fedha taslimu sh. milioni 100, dola za Marekani 11,560, euro 54,910 na kuwajeruhi wachina wanne kwa mapanga.
Ridhiwani amshukia Mbunge wa Korogwe
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Ridhiwan Kikwete, amesema Mbunge Korogwe Mjini, Bw. Yusuph
Nassir, anahatarisha jimbo hilo kwenda upinzani.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Ridhiwan Kikwete, amesema Mbunge Korogwe Mjini, Bw. Yusuph
Nassir, anahatarisha jimbo hilo kwenda upinzani.
Waislamu Morogoro wampinga Mufti Simba
Na Aziz Msuya, Morogoro
SAKALA la Shekhe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba, kumvua uongozi Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Yahaya Samwali, sasa limeanza kuchukua sura mpya.
SAKALA la Shekhe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba, kumvua uongozi Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Yahaya Samwali, sasa limeanza kuchukua sura mpya.
Lowassa akusanya mil.85/-za ajira kwa vijana
Richard Konga, Arusha
WAZIRI Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, amekusanya sh. milioni
85 katika harambee ya uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Waendesha Pikipiki mkoani Arusha (UWAPA), maarufu
kama 'bodaboda'.
IGP Mwema kufungua mkutano wa makachero
Na Frank Geofray, Jeshi la Polisi
WAKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI’s) kutoka Umoja wa Wakuu wa Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO), leo wanatarajia kuanza mkutano wa siku mbili jijini Dar es Salaam, chini ya Uenyekiti wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai nchini.
Katibu Uenezi CCM Shy avuliwa uongozi
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Shinyanga Mjini, kimemuondoa katika nafasi ya uongozi Katibu wake wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Bw. Charles Shigino ikiwa ni miezi michache tangu achaguliwe katika wadhifa huo.
Mbunge afichua siri kutojiunga na JKT
Na Benedict Kaguo
MBUNGE wa Kisesa, mkoani Simiyu, Bw. Luhaga Mpina, ametoboa siri ya kukataa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kutokana na wananchi wa jimbo hilo kukubwa na baa la njaa hali iliyowalazimu wengine kuzikimbia familia zao.
Waibuka 'kidedea' Shinda Biashara na Majira
Na Anneth Kagenda
WAJASIRIAMALI watatu akiwamo mwanafunzi wa Chuo cha St. Yohana kilichopo mjini Dodoma, Bw. Andrew Manjira, wameibuka washindi wa shindano la “Shinda Biashara na Majira”.
Mkuchika ataka gesi ichochee maendeleo
Na Casmir Ndambalilo, Newala
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika, ameiomba Serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuongeza muda na kasi ya kusambaza umeme unaotokana na gesi iliyogundulika mkoani Mtwara ili kuchochea
maendeleo ya wananchi.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika, ameiomba Serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kuongeza muda na kasi ya kusambaza umeme unaotokana na gesi iliyogundulika mkoani Mtwara ili kuchochea
maendeleo ya wananchi.
Raila Odinga afungua kesi kumpinga Kenyatta
Na Isaac Mwangi, EANA
ALIYEKUWA mgombea urais nchini Kenya kutoka Muungano
wa CORD, Bw. Raila Odinga, amefungua kesi katika Mahakama
ya Juu nchini humo kupinga ushindi wa Bw. Uhuru Kenyatta, ambaye alishinda kiti hicho kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika
Machi 4 mwaka huu.
Wajawazito Amana wapatiwa vifaa vya kujifungulia
Na Heri Shaaban
MADIWANI Wanawake wa Maniaspaa ya Ilala wametoa vifaa vya kujifungulia wanawake wajawazito katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo Amana.
UZINDUZI
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera, Kanali mstaafu Issa Njiku, akikata utepe ili kuzindua vyumba viwili vya madarasa kwenye Shule ya Msingi Kyaka, vilivyojengwa kwa msaada wa Taasisi ya Vodacom Foundation wilayani humo. Taasisi hiyo pia imetoa madawati tisini ikiwa ni jitihada za Kampuni ya
Vodacom Tanzania kuchangia maendeleo ya elimu nchini.
(Na Mpigapicha Wetu).
Rais Kikwete awashukia wanaokejeli Serikali
Na David John
RAIS Jakaya Kikwete, amewataka baadhi ya wananchi kuacha tabia ya kukejeli jitihada zinazofanywa na Serikali na hasa za kuwasogezea huduma za kijamii wananchi wake ,badala yake waunge mkono jitihada hizo.
'Serikali angalieni upya maslahi ya walimu'
Na Mercy James,
Mufindi
SERIKALI imetakiwa kuangalia upya maslahi ya walimu ili kuboresha taaluma katika shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Ajeruhiwa vibaya na mamba wakati akichota maji mtoni
Na Joseph Mwambije,Namtumbo
MKAZI mmoja wa kijiji cha Likuyu wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Bw.Rashid Almasi(59)amejeruhiwa vibaya na mamba baada ya kupambana na mamba huyo na hatimaye kumshinda nguvu.
Vijana watakiwa kuacha propaganda,wachape kazi
Na Florah Temba,
Moshi.
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Kilimanjaro,umewataka vijana wa chama hicho kufanya kazi na kuacha propaganda, hatua ambayo itakiwezesha chama cha CCM kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, unaotarajiwa kufanyika mwakani 2014, na kuyakomboa majimbo yaliyochukuliwa na upinzani katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Mkuchika azungumzia vurugu za wanasiasa Masasi
Na Casmir Ndambalilo, Masasi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika, amekemea vurugu zinazoanzishwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati nchini ili kujipatia umaarufu kwa kuwapotosha wananchi juu ya uendeshwaji wa Serikali iliyoko madarakani inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Watoto wachomwa midomo wakidaiwa kula karanga
Na Lilian Justice, Morogoro
JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamsaka mkazi wa Ujenzi, katika Kata ya Ndege, Bw. Jaribu Bakari, kwa kosa la kuwachoma moto mdomoni wanawe wawili kwa banio lenye mkaa.
Mhariri Majira kuwania tuzo uandishi mahiri
Na David John
MHARIRI Mtendaji wa Gazeti la Majira Imma Mbuguni ameteuliwa kuwania Tuzo za Uandishi mahiri wa habari,ambapo sherehe zake zitafanyika Aprili 5, mwaka huu Dar es salaam
Askofu awakemea wanaochoma makanisa
Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, amewataka baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Kiislamu nchini, kuacha kuchoma makanisa kwani kufanya hivyo watavuruga amani na utulivu uliopo.
Wajumbe Mara waipongeza TRA
Na Veronica Modest
Musoma.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa na wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara kwa
kufanikisha kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 kwa kipindi cha julai
2011 hadi June 2012.
Musoma.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa na wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara kwa
kufanikisha kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 kwa kipindi cha julai
2011 hadi June 2012.
Wanawake washauriwa kudai haki kwa utaratibu
Na Raphael Okello,Bunda.
WANAWAKE wametakiwa kutosababisha vurugu ndani ya ndoa zao kwa
kigezo cha kudai haki sawa badala yake wameshauriwa kufuata taratibu katika
kudai haki hizo.
WANAWAKE wametakiwa kutosababisha vurugu ndani ya ndoa zao kwa
kigezo cha kudai haki sawa badala yake wameshauriwa kufuata taratibu katika
kudai haki hizo.
Wakazi wa Majengo walalamika nyumba zao kujaa maji
Na Patrick Mabula,
Kahama,
Wananchi wanaoishi eneo la mitaa ya majengo mjini Kahama wamelalamikia kero ya
mafuriko yanayotokana na mvua zinaponyesha na kufanya mitaro kumwaga maji ambayo
huingia na kujaa ndani ya nyumba zao na kuwafanya wazikimbie na kulala nje huku
wengine wakilala kwa majirani.
Kahama,
Wananchi wanaoishi eneo la mitaa ya majengo mjini Kahama wamelalamikia kero ya
mafuriko yanayotokana na mvua zinaponyesha na kufanya mitaro kumwaga maji ambayo
huingia na kujaa ndani ya nyumba zao na kuwafanya wazikimbie na kulala nje huku
wengine wakilala kwa majirani.
TAKUKURU kushirikiana na asasi za dini
Na Rehema Maigala
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wameungana na asasi za dini katika kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)wameungana na asasi za dini katika kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania.
15 March 2013
Lwakatare ibua mapya Chadema *Dkt. Slaa adai mpango wa kumkamata waliujua *Asema propaganda zinatumika ili kuwachafua
Na Anneth Kagenda
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kukamatwa kwa Mkurugenzi wake wa Ulinzi na Usalama, Bw. Wilfred Lwakatare ni mkakati wa Jeshi la Polisi nchini.
Papa Mpya: Nimeanza kazi rasmi
ROAMA, Italia
PAPA mpya wa Kanisa Katoliki duniani, Francis I, ambaye ni wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini, ameanza kazi
rasmi akitangaza kulileta kanisa hilo pamoja.
Membe: Sihusiki kumtesa Kibanda *Afananisha jambo hilo na kuchafuliwa kisiasa
Na Rachel Balama
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema hausiki na hana sababu ya kuhusika
na vitendo vya ukatili na unyama aliofanyiwa Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri (TEF), ambaye pia ni Mhariri Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya New habari, Bw. Absalom Kibanda.
Moravian laguswa na shambulizi la Kibanda
Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa Kanisa la Moravian Tanzania (KMT), Jimbo la Kusini, umelaani vikali tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Bw. Absalom Kibanda na kudai vyombo vya Ulinzi na Usalama, vinapaswa kuwafuatilia na kuwakamata watuhumiwa hao.
Polisi aliyeua Mwalimu afukuzwa
Na Mercy James, Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe, limemfukuza kazi askari wake PC Gelvas Joseph, mwenye namba 9790, kwa kosa la kufanya mauaji
ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo, wilayani Makete.
Pinda ashauri njia za kuepuka tatizo la figo
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, amewahimiza Watanzania kuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku ili kujikinga na matatizo ya figo yanayozini kuongezeka kila siku.
Mtoto auawa, kunyofolewa macho
Na Elizabeth Joseph, Dodoma
MTOTO Happyness Paulo (3), mkazi wa Kijiji cha Handali,
Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, ameuwawa na watu wasiofahamika na kumchuna ngozi.
Mbwa mwenye kichaa awauma watu watano
Na Israel Mwaisaka, Chunya
WATU watano wakiwemo wanafunzi wawili, wakazi wa Wilaya
ya Chunya, mkoani Mbeya, wameng’atwa na mbwa mwenye kichaa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya kwa matibabu.
Muhubiri mbaroni kwa uchochezi
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
MUHUBIRI wa dini ya Kikristo, mkazi wa Kigogo, Dar es Salaam, Damian Ndhimbo (35), juzi alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, akituhumiwa kusambaza nyaraka mbalimbali zinazodaiwa kuwa za uchochezi.
13 March 2013
Mauaji ya waandishi yawagusa wadau
Na Rehema Maigala
WADAU wa habari nchini, wamekubaliana kuunda kamati ya watu 16 ambayo itakutana na wakuu wa vyombo vya usalama nchini ili kuzungumzia undani wa suala la usalama wa waandishi wa habari nchini.
WADAU wa habari nchini, wamekubaliana kuunda kamati ya watu 16 ambayo itakutana na wakuu wa vyombo vya usalama nchini ili kuzungumzia undani wa suala la usalama wa waandishi wa habari nchini.
TAMKO MOAT
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Ufuatiliaji wa kuzorota kwa mazingira ya usalama wa wahariri na waandishi wa habari, ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Business Times Limited, Bw. Aga Mbuguni (kushoto), akisoma moja ya matamko ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dar es Salaam jana, kuhusu matukio ya utekaji na utesaji kwa waandishi na wahariri yanayoendelea kutokea nchini na hatua zitakazochukuliwa kudhibiti vitendo hivyo. Wengine ni baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo. (Picha na Charles Lucas)
Wabunge Chadema kuhojiwa kwa pingu *Polisi wapewa kazi hiyo kuhakikisha wanahojiwa *Ndugai asema kamati wasiyoitambua ipo kisheria *Dkt. Slaa, Lissu wajibu mapigo, wamtega Makinda
Grace Ndossa na Gladness Theonest
OFISI ya Bunge imesema, wabunge ambao watagoma kwenda kuhojiwa katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Jeshi la Polisi litawapeleka kwa pingu katika kamati hiyo.
BAJETI MANISPAA
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mstahiki Yusuph Mwenda (katikati), akisoma tamko la kuidhinisha bajeti ya manispaa hiyo ya mwaka 2013-2014, mara baada ya kuungwa mkono kwa kauri moja na Baraza la Madiwani Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Naibu Meya, Bw. Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty. Zaidi ya sh. Bilioni 156 zitatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya manispaa hiyo. (Picha na Charles Lucas)
MATOKEO IV Walimu waliopengezana kuchunguzwa *TCRA kusaka ujumbe waliotumiana katika simu zao
Na Rose Itono
SERIKALI itashirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ili kuwabaini walimu waliopongezana kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012.
Abiria reli ya kati Dom wakwama
Na Elizabeth Joseph, Dodoma
MVUA zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo ya Godegode, Miganga na Gulwe, mkoani Dodoma, zimesababisha abiria zaidi ya 1,000 ambao wanatumia reli ya kati, kushindwa kuendelea na safari kutokana na njia za reli kuharibika.
Mwenyekiti CHADEMA asimamishwa uongozi
Na Wilhelm Mulinda, Mwanza
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Ilemela, mkoani Mwanza, kimemsimamisha uongozi aliyekuwa Mwenyekiti wa kata kwa tiketi ya chama hicho, Bw. Isack
Nyatega, kutokana na tuhuma mbalimbali.
Wawakilishi Z'bar wamuomba IGP Mwema kuboresha makazi ya askari
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, jana amefanya mazungumzo na wajumbe tisa wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar chini ya Mwenyeketi wake Bw. Hamza Hassan Juma.
Viroba 53 vya mirungi vyakamatwa Arusha
Na Pamela Mollel, Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha, limekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi viroba 53, katika matukio mawili tofauti.
TCRA: Mionzi ya simu haina madhara
Na Darlin Said
MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA), imekanusha taarifa zinazodai mionzi inayotumika katika vyombo vya mawasiliano ikiwemo simu za mkononi, ina madhara kwa afya ya binadamu.
TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya warsha ya wahariri na waandishi Dar es Salaam jana, iliyohusu mionzi inayotumika katika vyombo vya mawasiliano zikiwamo simu za mikononi ambapo alikanusha kuwa mionzi hiyo haina athari kwa watumiaji. (Picha na Prona Mumwi)
12 March 2013
Washtakiwa kesi ya uchochezi, wizi wakana waelezo ya awali
Rehema Mohamed na Rehema Maigala
WASHTAKIWA wa kesi ya wizi na uchochezi inamkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Issa Ponda na wenzake, jana waliendelea kujitetea baadhi yao wakikana maelezo ya awali waliyotoa katika Kituoa cha Polisi Mabatini, Kijitonyama.
DC Korogwe apinga taarifa ya Ofisa Elimu matokeo kidato IV
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, ameungana na vyama vya upinzani kuikataa taarifa ya Kaimu Ofisa Elimu Sekondari wilayani humo Bw. Shabaan Shemzigwa, kuhusu chanzo cha kufeli kwa wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2012 na kudai haina mashiko.
Mtikila ampongeza Dkt .Nchimbi
Na Kassim Mahege
SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi kuwasimamisha kazi maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali, Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party(DP) Mchungaji Christopha Mtikila amempongeza kwa hatua hiyo na kumtaka asiishie hapo.
SIKU moja baada ya Waziri wa Mambo ya ndani Dkt.Emmanuel Nchimbi kuwasimamisha kazi maofisa wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali, Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party(DP) Mchungaji Christopha Mtikila amempongeza kwa hatua hiyo na kumtaka asiishie hapo.
Mbatia amtaka Raila Odinga kuheshimu matokeo
Na David John
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James
Mbatia, amemshauri aliyekuwa mgombea urais nchini Kenya
kwa tiketi ya Chama cha Muungano CORD, Bw. Raila Odinga kuheshimu matokeo ambayo ndio maamuzi ya wananchi.
Serikali iwasaidie wajasiliamali kwa kuwapa mafunzo
KUJIAJIRI ni suala linalopewa kipaumbele na mamlaka
mbalimbali nchini pamoja na mataifa yaliyoendelea.
Mabadiliko makubwa katika mifumo ya uchumi, yamechangia
wananchi wengi kukosa kazi za kuajiriwa ambapo ajira binafsi
11 March 2013
Vigogo 6 polisi wasimamishwa *Dkt. Nchimbi afichua tuhuma nzito dhidi yao *Wadaiwa kupokea rushwa, kubambikia kesi *Wengine wabadili vidhibiti dawa za kulevya
Na Rehema Maigala
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewasimamisha kazi maofisa sita wa Jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma mbalimbali
za ukiukwaji wa maadili na taratibu za jeshi hilo.
Hali ya Kibanda sasa yaimarika *Taya, meno vyafungwa waya maalumu
Na Mwandishi Wetu
HALI ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Bw. Absalom Kibanda, inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa oparesheni ya kuondoa jicho la kushoto na kurekebisha taya.
UZINDUZI
Balozi Khamisi Kagasheki akikata utepe kwenye kasha la kuhifadhia fedha ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kikundi cha Habari Group uliofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni mlezi wa Kikundi hicho Bi. Angela Kairuki ambaye ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, wa pili kushoto ni Mbunge wa Busega Bw. Titus Kamani (Picha na Gladness Theonest).
'Waumini Anglikana tumuombee Dkt. Mokiwa'
Na Anneth Kagenda
WAUMINI wa Kanisa la Anglikana nchini, wameshauriwa kuzama katika maombi na kuiombea familia ya Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Valentino Mokiwa, ambaye mwishoni mwa wiki alivamiwa nyumbani kwake Mbezi Luis, Dar es Salaam,
eneo la Mashirikiano na watu wasiofahamika.
Maalim Seif ambana JK ripoti za mauaji
Peter Mwenda na Anneth Kagenda
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameitaka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete iweke hadharani matokeo ya uchunguzi wa matukio mbalimbali ya
mauaji na utekwaji nyara uliotokea hivi karibuni nchini.
CCM watoa tamko gesi ya Mtwara
Na Casmir Ndambalilo, Newala
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, imeunga mkono tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya kukubali ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaaam baada ya kubaini wakazi wa Mkoa huo watanufaika na mradi wa gesi uliopo mkoani humo.
Wanafunzi kidato cha II wakimbia masomo
Na Masau Bwire, Rufiji
ZAIDI ya nusu ya wanafunzi waliofeli mtihani wa kidato cha pili mwaka 2012 na kutakiwa kurudia masomo mwaka huu katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, hawajaripoti shuleni na hawajulikani waliko.
DC ambana Mbunge wa Korogwe kuelezea kazi za Mfuko wa Jimbo
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho
Gambo amemtaka mbunge wa Korogwe Mjini, Bw. Yusuph
Nassir, kuzunguka jimboni kwake ili kuwaeleza wananchi
kazi zinazofanywa na Mfuko wa Jimbo.
ABIRIA
Abiria wanaosafiri wa treni na kutoka Stesheni Kuu ya Dar es Salaam kwenda Ubungo wakisukumana kugombea kuingia saa za ajioni ambako abiria huongezeka baada ya kutoka kazini kama inavyonekana mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Kamata Dar es Salaam mwishoni mwa wiki (Picha na Peter Mwenda)
RC Moro awabana Ma DC, DED
Na Severin Blasio, Morogoro
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Joel Bendera, ameahidi kuwachukulia hatua za kinidhamu Wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi mkoani humu ambao watashindwa kusimamia
usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Rasimu ya Katiba Mpya kukamilika Mei-Warioba
Na Grace Ndossa
MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amesema rasimu ya Katiba Mpya inatarajiwa kukamilika ifikapo Mei mwaka huu.
Viongozi wa dini walaani wanaohatarisha amani
Na Christina Mokimirya
VIONGOZI wa Jumuiya na Taasisi mbalimbali za kislamu nchini zimeshauri Serikali kuweka utaratibu wa kutambua Jumuiya au Taasisi za kidini kwa nafasi sawa katika uwakilishi wa masuala ya kidini ndani ya serikali.
INAUZUNISHA*Mwalimu Mkuu ampa mimba mwanafunzi wake *Amefaulu kidato cha kwanza, akwama kuendelea *Mtuhumiwa yupo uraiani,Polisi watupiwa lawama
Na Gift Mongi
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Kigwe, iliyopo Wilaya
ya Bahi, mkoani Dodoma, Bw. Martin Mbowe, anadaiwa kumpa mimba wanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 (jina tunalo),
hivyo kushindwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza
katika shule ya Serikali mwaka huu.
Mbuge CHADEMA kortini kwa uchochezi
Na Jovither Kaijage, Ukerewe
MBUNGE wa Jimbo la Ukerewe, mkoani Mwanza, Bw. Salvatory Machemli (CHADEMA), jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya hiyo akikabiliwa na shitaka la uchochezi.
MBUNGE wa Jimbo la Ukerewe, mkoani Mwanza, Bw. Salvatory Machemli (CHADEMA), jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya hiyo akikabiliwa na shitaka la uchochezi.
DC Korogwe amseka ndani Ofisa Misitu
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, jana alimuamuru Mkuu wa Polisi wilayani humo,
Madaraka Majiga, kumkamata na kumuweka ndani Ofisa
Misitu Wilaya, Bw. Damas Mumwi baada ya kubishana
naye katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC).
MKUU wa Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, Bw. Mrisho Gambo, jana alimuamuru Mkuu wa Polisi wilayani humo,
Madaraka Majiga, kumkamata na kumuweka ndani Ofisa
Misitu Wilaya, Bw. Damas Mumwi baada ya kubishana
naye katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC).
SIKU YA FIGO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hussein Mwinyi, akizungumza na waandishi wa habari,(hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Figo Duniani Machi 14, mwaka huu. Kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema. (Picha na Prona Mumwi)
Kigogo scania kortini akidaiwa kuiba milioni 177/-
Na Judith Michael
OFISA Utawala wa Kampuni ya Scania (T) Limited tawi la Dar es Salaam, Didier Abdallah Mlawa(38) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kughushi saini ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na kujipatia kiasi cha sh. Milioni 177
Balozi Sefue aifagilia NHC
Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni, amelipongeza Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kufanyakazi nzuri katika miradi yake ya nyumba nchi nzima na kwamba ikikamilika yote baada ya miaka mitano itasaidia kuboresha maisha ya Watanzania.
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni, amelipongeza Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kufanyakazi nzuri katika miradi yake ya nyumba nchi nzima na kwamba ikikamilika yote baada ya miaka mitano itasaidia kuboresha maisha ya Watanzania.
Mbowe amaliza mgogoro Ktavi
Na Goodluck Hongo
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw.Freeman Mbowe amemaliza mgogoro mkubwa uliokuwa ukifukuta na kutishia mpasuko ndani ya Chama hicho mkoani Katavi, hadi kusababisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Said Arfi kuripotiwa kutupa kadi yake ya uanachama kwenye kikao cha ndani na kutishia kujitoa,
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw.Freeman Mbowe amemaliza mgogoro mkubwa uliokuwa ukifukuta na kutishia mpasuko ndani ya Chama hicho mkoani Katavi, hadi kusababisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Said Arfi kuripotiwa kutupa kadi yake ya uanachama kwenye kikao cha ndani na kutishia kujitoa,
MAKTABA YA BUSINESS TIME
Meneja Usambazaji wa Kampuni ya Business Times Ltd, Bi. Sophia Mshangama akimuonesha Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), baadhi ya vitabu na magazeti katika maktaba ya kampuni hiyo. (Picha na Zourha Malisa)
Mchungaji mbaroni kwa kutorosha wanafunzi
Na Heckton Chuwa,
Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro,linamshikilia mtu mmoja anaedaiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,(DRC), kwa tuhuma ya kuwatorosha wanafunzi wawili, (majina yanahifadhiwa), kwa lengo la kuwasafirisha nje ya
nchi.
Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro,linamshikilia mtu mmoja anaedaiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,(DRC), kwa tuhuma ya kuwatorosha wanafunzi wawili, (majina yanahifadhiwa), kwa lengo la kuwasafirisha nje ya
nchi.
Wasilisheni maombi wajumbe wa baraza-Warioba
Na Grace Ndossa
MWENYIKITI wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Mpya Jaji Joseph Warioba amewataka wananchi wenye sifa za kuwa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya Wilaya na ambao wangependa kuwa wajumbe wa mabaraza hayo kuwasilisha maombi yao kwa maofisa watendaji wa vijiji au mitaa kuanzia kesho hadi machi 20 mwaka huu.
WAFANYAKAZI WA BUSINESS TIME SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanykazi wa Kampuni ya Business Times Ltd, mara baada ya kutembelea kampuni hiyo. (Picha na Zourha Malisa)
Serikali yataka uangalizi maalum kwa watuhumiwa.
Na Rehema Mohamed
SERIKALI imewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kutaka watu wanne wanaotuhumiwa kukutwa na nyaraka za uchochezi, wawe chini ya uangalizi maalumu.
Manyanyaso ya wanawake duniani yakomeshwe
PAMOJA na umri mkubwa tangu kuanza kwa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, bado tunachoshuhudia katika jamii zetu ni manyanyaso mbalimbali wanayofanyiwa akina mama duniani.
UANDAAJI
Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhariri wa Habari za Michezo wa gazeti hili, Bi. Elizabeth Mayemba, kuhusu uandaaji wa kurasa za michezo, wakati waziri huyo alipotembelea Kampuni ya Business Times Ltd, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Usambazaji wa kampuni hiyo. Bi. Sophia Mshangama. (Picha na Anna Titus)
Sekondari yaanzisha jela ya mateso *Inaitwa “Guantanamo”, siri nzito yafichuka
Na Rashid Mkwinda, Mbeya
WALIMU wa Shule ya Sekondari Forest, iliyopo jijini Mbeya, wanadaiwa kutumia moja ya ofisi za walimu kama chumba cha
mateso kilichopewa jina la “Guantanamo”, ambacho hutumiaka
kutoa adhabu kwa wanafunzi wanaoshindwa kutoa hongo ya
sh. 500 hadi 1,000 wanapofanya makosa shuleni hapo.
4 mbaroni wakidaiwa kuchochea udini Dar
Rehema Maigala na Leah Daudi
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za uchochozi wa kidini baada ya kunaswa katika msako mkali uliofanyika jiji hilo.
Mbatia akataa ujumbe tume ya Pinda
Na Darlin Said
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James
Mbatia ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa, amesema hakubaliani na uteuzi uliofanywa na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, kuwa mmoja wa wajumbe katika tume ya kuchunguza sababu za kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012.
CCM yabaini 'madudu' katika miradi yake
Na David John
KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Zakia Meghji, amesema mikataba ya muda mrefu iliyosainiwa
na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika vitega uchumi vyake, imechangi wakose mapato ya uhakika.
Lipumba ataka wakazi wa Mtwara wasikilizwe
Na Said Hauni, Lindi
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeishauri Serikali kutopuuzia madai ya wakazi wa Mtwara kupinga usafirishaji wa gesi asilia
kwa njia ya bomba kutoka Kijiji cha Mnazi Bay, mkoani humo
na kuipeleka mikoa mingine ili kuzalisha umeme.
Polisi wakiri kuua raia kwa risasi
Na Damiano Mkumbo, Singida
MKAZI wa Bariadi, mkoani Simiyu, Methusala Shing'oma (36), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na polisi ambao walikuwa wakipambana na majambazi walioyateka magari mawili moja likiwa na maiti mbili pamoja na lori la mbao kwenye Kijiji Milade, Wilaya
ya Mkalama, Barabara ya Singida-Nzega.
Wafariki papo hapo katika ajali
Na Steven William, Muheza
WATU wawili wamefaliki dunia papo hapo baada ya malori
mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika Kijiji
cha Kilapula, kilichopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.
05 March 2013
MSAADA
Wasamaria wakisaidia kulinasua gari la polisi lenye namba PT 1448, Dar es Salaam jana, lililotumbukia katika mtaro uliofunikwa kwa maji ya mvua zilizoendelea kunyesha jijini, kamaabara ya Msimbazi eneo la KAMATA. Elimu ya Ulinzi Shirikishi Polisi Jamii imesaidia kuleta mahusiano mazuri kati ya jeshi hilo na wananchi. (Picha na Prona Mumwi)
Issa Ponda ana kesi ya kujibu *Mahakama yathibitisha mashtaka dhidi yao *Sasa kuanza kujitetea kuanzia Jumatano
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaona Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Issa Ponda na wenzake 49, wana kesi ya kujibu.
SHEKHE PONDA
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kisilamu Shekhe Issa Ponda akiwa chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana,wakati akirudishwa mahabusu baada mahakama hiyo kushindwa kutoa maamuzi hadi Jumatano wiki hii wakati washitakiwa watano wa kesi hiyo watakapojitetea upya.(Picha na Heri Shaaban)
Polisi wauawa Uchaguzi Mkuu Kenya
NAIROBI, Kenya
KATIKA hali isiyo ya kawaida, watu wasiopungua 17 wameuawa wakiwemo Maofisa sita wa polisi katika Mkoa wa Pwani, nchini Kenya siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu ulioanza jana.
Mapya zaidi yabuka kifo cha kigogo UVCCM
Na Pamela Mollel, Arusha
TUKIO la kufariki kwa aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, mkoani Arusha, Benson Mollel (26), limevuta hisia za wakazi
wa Mkoa huo baada ya vitu mbalimbali kupatikana katika
chumba alichokuwa amelala.
Mwalimu Mkuu Ifunda anusurika kuuawa
Na Eliasa Ally, Iringa
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Ifunda, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, jana walifanya vurugu kubwa shuleni hapo na kutaka kumuua Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shaaban Nsute.
GEMA HATARI
Wapitanjia wakipita kando ya gema eneo la Magomeni Mapipa, Dar es Salaam jana. Gema hilo linalotishia usalama wa nyumba zilizopo karibu limesababishwa na mmomonyoko wa udongo kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha jijini. (Picha na Charles Lucas)
Rais Kikwete ahimiza ufugaji wa kisasa
Na Freddy Maro, Bagamoyo
RAIS Jakaya Kikwete, amewataka wafugaji nchini kupima na kupanga ardhi kwa ajili ya ufugaji bora wenye tija ili kuepusha
migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Bodo Mpya TBS ilete mabadiliko-Dkt. Kigoda
Na Reuben Kagaruki
SERIKALI imeiagiza Bodi ya Mpya ya Shirika la Viwango nchini (TBS), kufanya haraka mabadiliko ya Menejimenti ya shirika hilo na idara zake ili kukirejesha chombo hicho kwenye hadhi yake.
MSHANGAO
Baadhi ya wapitanjia wakilishangaa tingatinga lililokuwa likiondoa tope chini ya daraja la Jangwani, Dar es Salaam jana. Tabia ya baadhi ya wananchi kushangaa hata mambo ya kawaida linasababisha kupoteza muda wa kujishughulisha katika masuala muhimu ya maendeleo yao. (Picha na Charles Lucas)
Jela miaka 30 kwa ujangili
Na Mary Margwe, Babati
MAHAKAMA ya Wilaya ya Babati, mkoani Manyara, imemuhukumu Bw. Hamis Said (32), kutumikia kifungo
cha miaka 30 jela na kulipa faini ya sh. milioni 10.
Dkt. Bilal: Muungano usidharauliwe
Na Veronica Modest, Butiama
MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amewataka Watanzania kutoudharau Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar badala yake uheshimiwe na kulindwa.
04 March 2013
AJIRA
Wasichana hawa walikutwa na mpigapicha wetu wakisafisha vioo vya magari yaliyokuwa katika foleni katika makutano ya Barabara za Nyerere na Msimbazi, Dar es Salaam jana, tatizo la ajira kwa vijana linachangia baadhi yao kubuni ajira zisizo rasmi ili kujipatia kipato. Hata hivyo malipo ya kazi hiyo ambayo hufanyika bila makubaliano hutegemea huruma ya mwenye gari. (Picha na Charles Lucas)
Kagasheki, Meya 'waipasua' CCM *Mgogoro wao wadaiwa kuvuka mipaka *Nape: Tume iundwe kuchunguzi tuhuma
Na Theonestina Juma, Bukoba
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, kimesema mgogoro wa kisiasa katika Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera, kati ya Meya wa Manipaa hiyo Dkt. Anatory Amani na mbunge wa jimbo hilo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kashakeki, umevuka mpaka.
Mbowe apewa ushauri wa bure *Viongozi wa dini wamtaka asitishe maandamano
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
KAMATI ya Maadili na Haki za Binadamu kwa Jamii inayoongozwa na Maaskofu, Mapadre, Wainjilisti na walimu, imekiomba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kusitisha maandamano waliyopanga kuyafanya jijini Mbeya wiki hii.
Maandamano kumpinga Muingereza yaandaliwa
Na Rose Itono
SIKU chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari nchi kutoa matangazo yanayohusu udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na raia
wa Uingireza dhidi ya Watanzania, taasisi isiyo ya kiserikali ya Human Settlement of Tanzania (HUSETA), imeamua
kuchukua hatua ya kupinga udhalilishwaji huo.
Moravian: Msemaji wa Kanisa ni M/kiti tu
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
KANISA la Moravian nchini, Jimbo la Kusini, limemkana Mchungaji Emaus Mwamakula na kusema yeye si msemaji wa kanisa hilo Jimbo la Misheni, kama anavyodai.
Mwanafunzi kidato cha nne awaua
Na Mercy James, Njombe
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Sekondari ya Ikuwo, Tarick Mbwilo (18), ameuawa na watu wasiofahamika pamoja
na mama yake mzazi Ester Mwalukolo (49).
Makamba: Nachonganishwa na CCM
Na Yusuph Mussa, Korogwe
KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuf Makamba, amesema baadhi ya vyombo vya habari nchini vinamchonganisha na chama chake.
Wauza samaki Feli wafungiwa geti na uongozi
Na Anneth Kagenda
MAGARI yaliyobeba samaki, jana yalifunga babaraba katika Soko
la Kimataifa la Feli baada ya uongozi wa soko hilo, kufunga geti ambalo hutumiwa na magari hayo kuingiza samaki sokoni hapo.
'Mfumo wa elimu sasa uangaliwe upya'
Na Raphael Okello, Bunda
MFUMO wa Elimu nchini, bado haujawawezesha wahitimu
kuwa wabunifu na kuwapa maarifa ya kupambana na maadui
watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini.
Hatima ya Ponda kujulikana leo
HATMA ya Katibu wa Junuiya za Taasisi za Kiislam nchini Sheikh Issa Ponda na wenzake 49 itajulikana leo ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa uamuzi kama wana kesi ya kujibu au la, anaripoti Rehema Mohamed.
JK ashangazwa na matokeo IV *Asema tume ya Pinda itatoa majibu stahiki *Adai vurugu za kidini kamwe hazivumiliki
SAKATA la matokeo mabaya ya wanafunzi waliomaliza kidato
cha nne mwaka 2014, limeigusa Serikali ambayo imekiri kuwa, jamii inahitaji kupatiwa majibu ya uhakika kuhusu anguko hilo.
Siri ya ushindi CCM-2015 yafichuka *Lowassa: Ipo siku Mungu atanipa utajiri
Na Daud Magesa, Mwanza
WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Edward Lowassa, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM), kitashinda vizuri uchaguzi Mkuu wa 2015, kama Serikali itarejesha utaratibu wa kuwapa mikopo wajasiliamali kupitia ‘Mabilioni ya JK’, ili waweze kujikomboa kiuchumi.
Mganga wa kienyeji azua 'kizaazaa'
Na Steven William, Muheza
KUNDI la wakazi waishio Kijiji cha Kibanda, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, juzi waliandamana hadi katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kushinikiza mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Aweso Kipaku, apewe kibali cha kuwasaka na kuwafichua wachawi waliopo kijijini hapo.
Shibuda 'awalipua' viongozi wa CCM
Na Suleiman Abeid, Maswa
MBUNGE wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda (CHADEMA), amekebea tabia ya baadhi ya viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayi humi wanaolitumia vibaya jina la Rais Jakaya Kikwete kuwatisha watendaji wa
Serikali.
Shahidi 'amkaanga' Mbunge Badwel
Na Rehema Mohamed
MENEJA wa Idara ya Mapokezi katika Hoteli ya Peacock, Bw. Casto Crales, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa, yeye ni miongoni mwa watu waliozithibitisha fedha za mtego wa rushwa alizokamatwa nazo Mbunge wa Bahi, mkoani Dodoma, Bw. Omary Badwel, kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).
Bila Serikali kuchukua hatua, vita ya rushwa kamwe haitakoma
TATIZO la rushwa nchini lipo katika sekta mbalimbali lakini
hali hiyo haina maana kuwa inakubalika katika jamii.
Subscribe to:
Posts (Atom)



