19 March 2013
Papa mpya kusimikwa rasmi leo
ROME, Italia
VIONGOZI mbalimbali duniani wanatarajiwa kushiriki misa ya kusimikwa kwa Papa mpya wa kanisa hilo duniani Francis I ambayo itafanyika leo Vatican.
Kwa mujibu wa Kituo cha Redio cha Sauti ya Ujerumani (DW), kimesema hafla hiyo inatarajiwa kuwa tofauti na hali ilivyokuwa siku za nyuma (kuzoeleka), kutokana na kiongozi huyo jinsi alivyojionesha katika siku chache za kwanza.
Papa huyo alijionesha kuwa yeye ni mtu wa kawaida kama kiongozi wa kwanza wa Kanisa hilo duniani kutoka Amerika ya Kusini.
Rais wa Agentina, Bi. Cristina Fernandez de Kirchner, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Waziri Mkuu Mariano Rajoy wa Hispania na Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria misa hiyo.
Wengine ni Rais wa Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy, Rais wa Halmashauri ya umoja huo, Jose Manuel Barosso, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden ambaye ni Mkatoliki, aliwasili Roma jana kuiwakilisha nchi yake katika sherehe hizo.
Juzi mchana, Papa Francis aliwahutubia watu 150,000 ambao walikusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment