15 March 2013

Lwakatare ibua mapya Chadema *Dkt. Slaa adai mpango wa kumkamata waliujua *Asema propaganda zinatumika ili kuwachafua


Na Anneth Kagenda

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kukamatwa kwa Mkurugenzi wake wa Ulinzi na Usalama, Bw. Wilfred Lwakatare ni mkakati wa Jeshi la Polisi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, alisema jeshi hilo linatumia propaganda chafu dhidi ya CHADEMA ili kukichafua.

Alisema chama hicho hakipo tayari kuona kinachafuliwa kwa propaganda hizo ambapo hivi sasa, wako kwenye mkakati wa kufuatilia kwa karibu tukio la kukamatwa Bw. Lwakatare.

“Tunafuatilia ili kuangalia kama ukamatwaji wake umezingatia sheria za nchi au la, sisi tunaona kuna ambayo chama chetu kinafanyiwa ambayo hayaturishi na kuona wazi hini ni
propaganda za kutaka kutuchafua,” alisema Dkt. Slaa.

Akizungumzia tukio hilo kwa undani, Dkt. Slaa alisema kinachoonekana ni jeshi hilo na vyombo vingine vya dola vinashiriki kutengeza  propaganda chafu dhidi yao.

“Hii imetokana na vyombo husika kuwahusisha viongozi wetu na unyama unaondelea nchini wa kuteswa watu, kupigwa, kung'oa kucha na baadaye kuwateketeza wakiwa nusu mfu,” alisema.

Dkt. Slaa aliongeza kuwa, vitendo vya uvamisi, utekwaji na mateso vilianza baada ya tukio la kutekwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dkt. Steven Ulimboka, kuuawa kwa mwandishi
wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, marehemu Daud Mwangosi na sasa Bw. Kibanda.

“Jeshi la Polisi linapaswa kutenda haki katika uchunguzi wao juu
ya tukio la kuvamiwa na kupigwa Bw. Kibanda na kufanya kazi bila ushabiki wa kisiasa au shinikizo la wanasiasa kwani kufanya hivyo, inaweza kutokea hatari zaidi,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu video ya Bw. Lwakatare inayodaiwa kuwa ya uchochezi Dkt. Slaa alisema, video hiyo inaonesha mtu mmoja akizungumza na kama ni ofisa huyo (Lwakatare) ambapo
kinachoonekana ni sauti si picha.

Alisema chama hicho kinaamini video hiyo imetengenezwa na hakuna ushahidi wowote ambapo kitendo cha kukamatwa kwake, CHADEMA walipata taarifa mapema za kuwepo mkakati unaoratibiwa na kufanikishwa na vyombo hivyo.

Dkt. Slaa alisema, kutokana na matukio mbalimbali dhidi yao, wamefungua majalada polisi wakilalamikia mchezo mchafu wanaofanyiwa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Kauli ya Dkt. Slaa imekuja siku mbili baada ya kukamatwa Bw. Lwakatare kwa tuhuma za kuhusisha na mashambulio ya watu mbalimbali kutokana na ushahidi uliopo kwenye video
ambayo pia imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

15 comments:

 1. Ni rahisi kuiamini cdm kuliko ccm. ccm iko madarakani na wako kwenye nafasi nzuri kutumia utaalam wa kutesa toka majeshi ya serikali. Nadhani cdm wanaweza tu kufanya wanayodaiwa na ccm kufanya kama wana wazimu kitu ambacho siamini. ccm wako madarakani (sawa na mbwa na mfupa halafu unataka kumnyang'anya). cdm wanatamani wapewe wao mfupa. Sasa hapo pima tabia ya kila mmoja.

  ReplyDelete
 2. Inakuwaje watuhumiwa wengine wakubwa kabisa katika matukio ya Mwangosi,Ulimboka na wengineo inakuwa kigugumizi kuwakamata ila kwa wengine ni very very simple

  ReplyDelete
 3. HAKUNA MTUHUMIWA MKUBWA NA MDOGO MUUAJI NI MUUAJI TU AWE CHADEMA AWE CCM ROHO ZA BINADAMU HAKUNA SPEA HAKUNA ALIYETUMWA KUZIMU AKARUDI TUSITUMIWE WENZETU WALIOTOLEWA KAFARA KUJITANGAZA KISIASA MTU WA AINA HIYO KAMA MUNGU ANGECHUKIZWA NA UMWAGAJI DAMU HUU ANGEMFANYA TAAHIRA AU HATA BUBU ILI AACHE KUENEZA SUMU MBAYA TANZANIA TUMECHOKA KUMWOMBA MUNGU AMANI WAKATI KUNA WANAMWOMBA MUNGU AWAPE NGUVU YA KUENEZA UCHOCHEZI WATU WAUANE ILI AFANIKIWE KISIASA ANAYEINGIA MADARAKANI KWA KUMWAGA DAMU NA DAMU YAKE HUMWAGWA

  ReplyDelete
 4. huu uliofanywa ni unyama,haukubaliki hata kidogo,
  ila waandishi kalamu itumike kwa maslahi ya taifa,si kuwalnda mafisadi wakuu na kutumika kuchafua maisha wa watu ambao angalau ni waadilifu.musiwe na bei kama wanasiasa wetu.au wanasheria wa serikali

  ReplyDelete
 5. Nadhani Rais anastahili kuingilia kati mambo kama haya. Kutesa na kuua watu kwa nia tu ya kuichafua CHADEMA ili CCM iendelee kutawala kutamchafua Rais Kikwete maisha yake yote. Atadharaulika ndani ya Tanzania na kila nchi Duniani, na pengine kuja kushtakiwa.

  Mwigulu alizungumzia zamani kuhusu video inayoonesha CHADEMA kupanga mikakati ya mauaji. Huyu huenda ndiye aliyeiandaa video hiyo au alikuwa akifahamu uandaaji wake. Vitendo hivi vinazidi kuichafua CCM, Serikali na Rais.

  ReplyDelete
  Replies
  1. JAMANI RAIS AINGILIE ILI IWE NINI? YAKITOKEA MAMBO KAMA HAYA TUNALALAMIKA POLISI HAWAFANYI VYEMA KAZI ZAO, SASA KWA HILI WAMEPATA PA KUANZIA, WANASIASA TUWAPE POLISI NAFASI WAFANYE KAZI YAO BILA KUINGILIWA< WANANCHI TUJIEPUSHE NA HOJA ZA KISHABIKI

   Delete
  2. Hivi kweli Watanzania wote tumekuwa wanasiasa na kushindwa kusimama kwenye ukweli na kuanza kulalamikia Rais na Polisi kila kukicha hata kwenye mambo ya wazi?

   KUSOMA TUMESHINDWA,JAMANI HATA PICHA ITUSHINDE KUTAMBUA?

   Delete

 6. CCM INAZIDI KUPOTEZA MUDA WAKE KWA MIPANGO YA KIFEDHURI ISIYO NA TIJA KWAO. WAMESHINDWA KUJIVUA MAGAMBA SASA WAMEAMUA KUPANDIKIZA MBEGU YA VITISHO, KUCHAFUANA KWA MAUAJI NA KUTESA. CCM DAWA NI MOJA TU ACHENI UFISADI, TATUENI SHIDA ZA WANANCHI( MAJI, ELIMU BORA, MFUMUKO WA BEI NA MASLAHI BORA KWA WATUMISHI) MKIYAWEZA HAYO WANANCHI WATAWAKUBALI TU

  ReplyDelete
 7. Nadhani tusubiri uchunguzi wa jambo leneyewe hapa.Kuna mengi zaidi ambayo yanahitajika kufanyika.(uhalisia wa mkanda ) una mengi ya kuhoji,upekuzi una mengi ya kuhoji.

  mambo mengine hapa yanahitaji utalaam zaidi kuyapatia ufumbuzi.Tuiache hii kazi kwa ulelezi tuonen unafika wapi.Kivumbi kipo mahakamani na sio nje ya mahakama.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hapa tunapumbazwa tu tusahau majukumu muhimu yaayotukabidhi, tuhitaji hospitali ziboreshwe, maji safi kwa wananchi, umeme nao shida, watu wakidai haki zao wanayamazishwa na kuteswa hata kuuawa. Kamati zinazoundwa ni za kula hela tu maana wanachofanya wanakijua watajihukumu wenyewe???? Mambo yanatendeka kiongozi amekaa kimya hata vyombo vilivyo chini yake haviwajibishwi. Elimu ambayo ndio uti wa mgongo wa Taifa lolote imesahaulika, wakipata mtu wa kuwaambia walipojikwaawajirekebishe wanampiga mikwara - Tutafikaa. Rasilimaliza nchi zinatokomea Je, Mungu alifanya makosa kutupa hii nchi yenye kila aina ya utajiri. Ni bora kuwa na umaskini wa mali kuliko akili. Cheo ni dhamana when U are there think of your Nation, leo unacho kesho huna, unapopanda ngazi angalia wa chini yako usiwatupie mawe maana iko siku na wewe utashuka.

   Delete
 8. Kama SERIKALI NA DOLA VINAJIHUSISHA NA UHARANIA WA KUTEKA, KUJUMU CHADEMA HATA KUUA wananchi especially IKULU INAYOHUSISHWA BASI JUMBA LETU KUU NA RAISI WAJITAFITI NANI ANAFANYA HAYA MAMBO NDANI YA IKULU NA KWA FAIDA YA NANI? KAMA NI UTAWALA KILA MTANZANIA WA CHAMA CHO CHOTE ANA HITAJI KUISHI KWA HESHIMA. TUSIWAFUMBIE DESTRUCTIVE ELEMENTS WATAKAOHATARISHA AMANI NA KUMCHAFULIA JINA JEMA RAISI KIKWETE

  ReplyDelete
  Replies
  1. Haya! uhuru wa mawazo, hata matusi ya nguoni ni uhuru wa mawazo. ila tungejua conspiracy ya haya yanayotendeka tusingeamini kuwa mafia wa chadema wako nyuma ya hili. Hivi kusema kuwa nchi haitatawalika nini maana yake? Nani alishawahikuhoji maana ya kauli hii nzito na kuhusisha na haya yanayotekea? Tatizo la watanzania ni wasahaulifu na wanasukumwa zaidi na hisia na chuki.

   Delete
 9. Hizi ni propaganda za CCM zinazolenga kuichafua CHADEMA mbele ya wananchi baada ya kuona kwamba wameshindwa kutimiza ahadi walizoahidi kwa wananchi huku wakiona uchaguzi ukikaribia kwa kasi ya kutisha!

  Wananchi tunazo akili, tunajua njama hizi zote zinatengenezwa na CCM ili kutusaulisha matukio ya kipuuzi kama UFISADI, mauaji ya Dr Ulimboka, Mwangosi, mashehe, mapadri na masuala mengine tete kama vile matokeo mabaya ya darasa la saba, kidato cha pili na kidato cha nne. Tafakari, chukua hatua!

  ReplyDelete
 10. Kuishi kwingi ni kuona mengi. Wanasiasa si watu wa kuwaamini wanaweza kufanya jambo lolote. acheni kulaumu kila kitu serikali,hawa jamaa hata kama Slaa ni msafi kazungukwa na watu wachafu wenye tamaa ya madaraka kwa njia yoyote ile,sishangai Lwakatare kuhusika na upangaji huo kwa faida yake binafsi na chama chake. nina umri wa wa miaka sitini nimefanya kazi na wahaya na wachaga kwa miaka mingi,hawa jamaa ni hatari sana. mchaga hulka na tabia zake ni za Kikikuyu na Mhaya na Mnyaruanda. ni wakatili,wauaji,wenye tamaa ya utajiri hata kwa kuua au kufanya chochote,ni wakabila wa kupindukia. kwa sifa zote hizi na ndani ya hicho chama wamejipachika wengi tu,hata huyo Slaa wanaweza wakamuua halafu wakaishika nchi wao. kwa waandishi wa habari,nyoka hafugiki iko siku atakudonoa,sasa hawa mnaowapamba sana,wanawageuka na kuwadonoa wapate kuonekana wao sio kwa kumchafua mwingine,kuweni wakweli bila kumpamba mtu,unaowapamba wanakudonoa kumchafua mwingine na mwenye hasara ni wewe

  ReplyDelete
 11. kuna mambo mengi sana katika siasa, nadhani kinachotutatanisha watanzania wengi ni kuona Lwakatare kakamatwa kwa sababu ya video zilizosambazwa kwenye mtandao wakati kuna video kama hizo zilishawahi kuonekana na watu hawakuchukuliwa hatua. Ulimboka aliwataja kwa majina waliomtesa lakini hawajakamatwa, taarifa ya kamati ya uchunguzi wa mauwaji ya Daud Mwangosi sjui ni nani kati yetu alishawahi kuisikia! kuna mambo mengi sana, kijamii,kiuchumi, kisiasa na kidini ambayo yanavurugwa na kamati kuundwa lakini hatujasikia wahusika wakikamatwa na kufikishwa mahakamni. Mimi simtetei Lwakatare maana naye ni binadamu na kwa wana-siasa kuchukua dora huwa ni 'priority number one' bila kujali ni kwa njia zipi wakati mwingine zinatumika. Lakini kukamatwa kwake kunatengeneza mazingira yanayoonekana ni kandamizi zaidi ya haki na sheria kuchukua mkondo wake.Haki ya mtenda kosa ni kuchukuliwa hatua za kisheria lakini sheria inapokuwa 'segregative' ktk misingi ya kisiasa ndipo inapoleta shida.Nadhani kuna mambo mengi yanayotakiwa kutazamwa upya kuanzia kwa wananchi wenyewe maana serikali ikitimiza wajibu wake kwao wanaona kama ni zawadi au ukarimu wamefanyiwa! wananchi kutowajibika, uvivu wa kufikiri na kuwakabidhi watu wachache kufikiri kwa niaba yao, kutokujua haki zao, kuwa na bei (tena the cheapest cost ahasa wakati wa uchaguzi), kuwa wepesi wa kubali yaishe,na uvivu wa kufanya kazi ni chanzo cha yote yanayofanyika Tanzania. Tuendelee kuwa washabiki na kuiuza haki yetu ya kuwa watanzania maana ndilo tulilolichagua lakini cjui tutawajibu nini wajukuu na watoto wetu ck wakihitaji kujua tulifanya nini kuhakikisha mambo katika nchi yetu yanabadilika!

  ReplyDelete