18 March 2013
Lowassa akusanya mil.85/-za ajira kwa vijana
Richard Konga, Arusha
WAZIRI Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, amekusanya sh. milioni
85 katika harambee ya uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Waendesha Pikipiki mkoani Arusha (UWAPA), maarufu
kama 'bodaboda'.
Katika harambee hiyo ambayo ilifanyika juzi mkoani humo Bw. Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi, alichangia sh. milioni
10 pamoja na pikipiki 10.
Kabla ya harambee hiyo, Bw. Lowassa aliipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Rais Jakaya Kikwete kwa
kuwapa fursa vijana kujiajiri wenyewe kupitia vyombo hivyo
ili kuongeza ajira na kupunguza vitendo vya uhalifu nchini.
“Ajira za bodaboda zimewasidia vijana wengi kujipatia ajira
ambazo zimekuwa na msaada mkubwa katika maisha yao, nawaomba wafanyabiashara kote nchini, kuungana pamoja
na kuonesha nia ya kuwasaidia vijana waweze kujiajiri.
“Fedha ambazo zitachangwa hapa, zitawasaidia kujikwamua
kimaisha na kujiletea maendeleo...vijana wasio na ajira ni sawa
na bomu ambalo likiripuka madhara yake ni makubwa, wakiwa
na ajira wataachana na maandamano yasiyo na tija,” alisema.
Aliwataka vijana hao kujiepusha na ushawishi wa wanasiasa kwa kushiriki maandamano yasiyo na tija badala yake wajikite katika maendeleo yao na fedha wanazopata wakopeshane ili waweze
kuinuana kiuchumi.
Awali katika risala ya umoja huo iliyosomwa na Katibu wao, Bw. Fabian Shayo, alisema waliiomba Halmashauri ya Arusha iwapatie tenda mbalimbali ikiwemo ya usimamizi wa usafi wa mazingira.
“Pia tunahitaji kuwa na sare wakati tunapoendesha vyombo hivi
ili tuweze kutambulika kwani wapo baadhi ya waendesha pikipiki
ambao si waanifu kwa abiria hivyo kuharibu sifa yetu,” alisema.
Alisema wakati Rais Kikwete alipokwenda mkoani humo katika uzinduzi wa jiji hilo, alitoa ahadi ya kuwapa pikipiki 10 lakini
hadi sasa msaada huo haujawafikia.
Wachangiaji wengine katika harambee hiyo ni pamoja na mfanyabiashara wa madini, Bw. Mathias Manga na Bw
Fhilemon Mollel, ambao wote walichangia sh. milioni
15 kila mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment