03 December 2013

LOWASSA ‘AFUNGUKA’ KWA WAUMINI



Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa (mwenye suti),akiwaaga waumini wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mtandi,Wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,baada ya kuendesha harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo ya Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKU),mwishoni mwa wiki ambapo sh.milioni 103 zilichangwa katika harambee hiyo. Kulia kwake ni Askofu wa Kanisa hilo,Dayosisi ya Newala,Oscar Mnung'a.

  •   ACHANGISHA MILIONI 103/-,AMMWAGIA  SIFA MKAPA

Na Mwandishi Wetu, Masasi
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, amesema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote katika mapambano ya kuondoa umaskini kwenye jamii.

Bw. Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Mjini Masasi mkoani Mtwara, katika harambee iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, mkoani humo.
Harambee hiyo ilikuwa na lengo la kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKI) na kusisitiza kuwa, yeye ni mdau wa mapambano hayo.
“Mtu yeyote anayepambana kuondoa umaskini katika jamii, niko tayari kushirikiana naye katika harambee za harakati hizi,” alisema Bw. Lowassa na kuongeza kuwa, wanawake ni jamii inayochukia sana suala zima la umaskini.
“Wanawake ni wadau wakubwa wa kupambana na umaskini ndiyo maana chama changu CCM, katika rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya uwakilishi bungeni kati ya wanawake na wanaume kwa sababu kinawapenda,” alisema.
Alisema kwa sababu hiyo, ndiyo maana ameridhia kushiriki harambee hiyo ambapo kufika kwake kanisani hapo kumetokana na Wilaya hiyo kutoa kiongozi makini, mwadilifu na shupavu mkubwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa.
“Hapa pana historia ya kutoa kiongozi aliyeiongoza nchi yetu kwa uadilifu na umakini mkubwa, walikuwepo watu waliyojaribu kumsema sema katika vyombo vya habari.
“Mwisho wa siku watu hao wamekiri kuwa Bw. Mkapa alikuwa kiongozio makini,” alisema Bw. Lowassa ambaye wakati kiongozi huyo akiwa madarakani, alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano kabla ya kupelekwa Wizara ya Maji na Mifugo.
Katika harambee hiyo, zaidi ya sh. milioni 103 zilipatikana ambapo Bw. Lowassa na marafiki zake alichangia sh. milioni 10 na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. milioni 100.

9 comments:

  1. WANAJARIBU KUMWIGA LOWASA WENGI WANAUMBUKA WAKISHINDWA HAWAKOSI LA KUSEMA NI SAWA NA SUNGURA ANAPORUKIA NDIZI ZIKIMSHINDA ANADAI NI MBICHI ILA HII KATIBA SIJUI TANZANIA ITANUSURIKA AU YALIYOTOKEA USSR,YUGOSLAVIA NA ROMANIA YATATOKEA KWETU MUNGU ATUNUSURU

    ReplyDelete
  2. Hii ni rushwa kubwa. Kuwanunua wakristu kutumia makanisa ni rushwa.

    ReplyDelete
  3. BAADHI YA VITENDO VYA UADILIFU KIMITAZAMO NI;KILE AMBACHO KINALETA HALI BORA AU KINACHOLETA MADHARA KIDOGO AU KINACHOLETA MANUFAA MENGI[MTAZAMO WA MANUFAA/MATUMIZI] AU NI KILE AMBACHO KINALINDA NA KUHESHIMU HAKI ZA WALIOATHIRIKA[MTAZAMO WA HAKI] AU KILE AMBACHO KINAWALETEA HAKISAWA BINADAMU WOTE[ MTAZAMO WA HAKI ZA KISHERIA] AU NI KILE AMBACHO KINAFANYIKA KWA FAIDA YA JAMII[MTAZAMO WA FAIDA KWA JAMII] SIFA ZA WATU WAADILIFU NI NYIGI BAADHI YA HIZO NI ;-NI WALE WENYE DIRA YA KUKUZA UADILIFU NA KUUSIMAMIA KIKAMILIFU,HAWAYUMBISHWI KATIKA MISIMAMO YAO NA MARA ZOTE HUFANYA KAZI ZAO KITAALAMU- HUWA VIONGOZI WA WATU WOTE BILA KUWA NA UBAGUZI WA AINA YOYOTE,,-WANAKUWA MFANO WA KUIGWA,-WANAJENGA MAZINGIRA YA KULETA MAENDELEO YA KUDUMU ,-WANATOA FURSA KWA WATU WENGINE KUJIENDELEZA KIMASLAHI NA KITAALAMU,-HUWAFANYA WATU WENGINE WAJIONE BORA NA WANATHAMINIWA NA KUTAMBULIWA UTU WAO,-UADILIFU WAO HUWAFANYA WADUMISHE VIWANGO VYA UAMINIFU,KUSEMA KWELI DAIMA NA KUJENGA IMANI KWA WALE WANAOWAONGOZA

    ReplyDelete
  4. These natural disasters ALLAH punishment to the government and people of Tanzania to convert to Islam on 10.4.2018 to avoid an earthquake plus 7 volcano flood hurricane meteorite tornadoes and other disasters and if the end of the world to avoid hell.
    Ces catastrophes naturelles punition d' ALLAH aux gouvernement et peuple de Tanzanie de se convertir a l'islam le 10.4.2018 pour éviter un séisme plus 7 volcan les inondations ouragan les tornades météorite et d'autres catastrophes et si la fin du monde pour éviter l'enfer.

    ReplyDelete
  5. Cyclone Kenneth ALLAH punishment to Christians to convert to Islam and witches and witches to end their crime witchcraft in Mozambique and Tanzania on 26.4.2019 to avoid these punishments of ALLAH cyclone strong earthquake tsunami floods lightning storms meteorites Ebola viruses in Mozambique and Tanzania.
    Cyclone Kenneth punition d' ALLAH aux chrétiens de se convertir a l'islam et aux sorciers et sorcières de mettre fin a leurs crime la sorcellerie en Mozambique et en Tanzanie le 26.4.2019 pour éviter ces punitions d' ALLAH cyclone fort séisme tsunami les inondations les foudres les météorites Ebola les virus en Mozambique et en Tanzanie.

    ReplyDelete
  6. Just question I am another can I use majira news paper to publish my story? My name Saudi mbungu
    Penni LA Tamaa and Janga comic?
    Thanks

    ReplyDelete
  7. La dulzura del sueño.
    ( third version )

    Cuando el canto
    de las luces
    se dispersa en
    la campaña siento
    un mágico sonido
    que se expande
    dulcemente
    regalando la
    tristeza a una
    tímida ilusión:
    y así, en un
    instante, vuelvo
    al soplo del pasado
    y a la hermosa
    juventud...

    Francesco Sinibaldi

    ReplyDelete

  8. Great web site you've got here.. It's difficult to find high-quality writing like
    nowadays. I seriously appreciate people like you! Take care!!

    my website - 휴게텔
    (jk)

    ReplyDelete