18 March 2013

Ridhiwani amshukia Mbunge wa Korogwe

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Ridhiwan Kikwete, amesema Mbunge Korogwe Mjini, Bw. Yusuph
Nassir, anahatarisha jimbo hilo kwenda upinzani.


Alisema Bw. Nassir hafanyi mikutano na wananchi wala
kuhudhuria vikao vya chama ili kupanga mikakati ya ushindi
wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Bw. Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika hafla
fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Benki ya
NMB, ili kuanzia kwa mashindano ya kombe la Mkuu wa
Wilaya hiyo, Bw. Mrisho Gambo.

Aliongeza kuwa, madhara ya kutofanya mikutano ya wananchi
au kuhudhuria vikao vya chama ni makubwa kwani CCM ndio
itakayoathirika na kusisitiza kuwa, uchaguzi ujao unatarajiwa
kuwa mgumu kutokana na upinzani uliopo.

Alisema yeye amefika wilayani humo mara tatu, kuonana na viongozi wa chama ambapo Bw. Nassir hakuonekana katika
vikao hivyo lakini bado ameshindwa kuwatembelea wapiga
kura jimboni kwake jambo ambalo linaiweka CCM pabaya.

“Hapa Korogwe Mjini kuna matatizo ya uongozi, nimekuja mara tatu lakini sijamuona mbunge wa jimbo hili (Nassir), zaidi ya kuwa
na Mbunge wa Mbunge Korogwe Vijijini (Stephen Ngonyani).

“Kutokana na hali hii, yeye (Nassir), hawezi kuumia bali chama
ndio kinachoathirika...juzi nimesikia watu wakisema Mary Chatanda (Mbunge wa Viti Maalumu), anataka kugombea ubunge, kama hali yenyewe ni hivi kwa nini asigombee.

“Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, si rahisi kama mnavyofikiria, bila kuwatumikia wananchi hatutavuka,” alisema Bw. Kikwete.

Katika hafla hiyo ambayo Bw. Kikwete alikuwa mgeni rasmi, pia walikuwepo madiwani ambapo Bw. Gambo, alimueleza Katibu wa Bw. Nassir, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Manundu, Bw.
Robert Bago, ampangie mbunge huyo mikutano ambayo
itamwezesha kukutana na wananchi.

“Bago msaidie mbunge wako aweze kufanya mikutano ya wananchi, ubunge si wa kwake bali wa chama, akianguka yeye kinachoathirika ni CCM si vinginevyo,” alisema Bw. Gambo.

8 comments:

  1. WEWE RIDHIWANI SASA UMEKUWA HAKIMU WA CCM?

    BWANA MDOGO UNATAKA KULETA UFALME, KUFIKA KWAKO MARA TATU KOROGWE UNATAKA MBUGE WA WANANCHI AKUKIMBILIE KISA WEWE UKO KOROGWE?
    ACHA MAMBO YA KIHUNI NAKUSHAURI USITUMIE MADARAKA YA MZEE KUWAAMRISHA WAWAKILISHI WA WANANCHI MBUNGE HUYO NI MTU MZIMA NA ANAELEWA WAJIBU WAKE.

    ReplyDelete
  2. huyu ngojeni atakuwa kama watoto wa Saddam au Gadafi! Kwani 2015 mbali? Atauza sura huyu ngojeni kidogo

    ReplyDelete
    Replies
    1. KUMBE NI RAHISI KUWAKAMATA WALIOMDHURU MWANDISHI WA HABARI KIBANDA WAKO WALIOLISHWA LIMBWATA NA FREEMASON WANACHOTAKA NI DAMU ZA WENZAO TU ILA UTAWALA WA SHETANI HAKUNA AMANI SI IRAQ,LIBYA,MISRI,TUNNISIA,WALA SIRYA

      Delete
  3. hujuwi kama huko ni kumnyima mwenzako kura? maneno gani hayo ya uchochezi. jirekebishe bwana mdogo wenzako hawafanyi hivyo

    ReplyDelete
  4. Kweli hii nchi inahitaji raia kuingia msituni, kwa jina la baba mwana nae analeta kibesi?! Ni ajabu sana, hivi hawakuwepo viongozi wengine yaani watoto wa wakulima hicho kiti cha ujumbe wa halmashauri kuu (NEC) mpaka wakapeana hawa vibaka? Inauma sana watanzania wenzangu. Tuzindukeni 2015 tusifanye kosa.




    ReplyDelete
  5. Harambeee eee harambe mama harambeee!
    Usione naimba ukadhani nina furaha, ...........

    ReplyDelete
  6. Hatred statements rather than political. Ila kwa USA kina Bush, Clinton si tatizo. Tusubiri huo mwitu mnaotaka kwenda halafu tuone nini kitatokea kwa kina mama na watoto.

    ReplyDelete
  7. Ama kweli Mbwa wa Bwana na yeye Bwana.

    Kwani Ridhwani asipeleke malalamiko yake kwenye vikao halali vya chama na kukurupuka kwenye vyombo vya habari.

    Ridhwani hebu tulia maana wenzio watoto wa Husni Mubarak wa Egypt walikuja na meno ya juu kama wewe kujipeleka mbele mbele kwenye Chama Tawala na sasa wako korokoroni.

    Sasa wewe bora tulia kula mamilioni yako usije kusumbuka baadae maana Upinzani hata mkitumia mabavu 2015 watachukuwa nchi

    ReplyDelete