19 March 2013
Madawa ya kulevya bado yanaingizwa nchini- Nzoa
Na Veronica Ikonga
JESHI la Polisi nchini limewataka wananchi kutoa ushirikiano pale wanapoona ama kuwahisi watu wanaojihusisha na uingizaji dawa ya kulevya nchini watoe taarifa sehemu husika.
Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Madawa kulevya nchini Bw.Geofrey Nzoa alisema ni ngumu sana kumkamata mtuhumiwa kwa kosa la madawa ya kulevya bila kuwa na kithibitisho.
"Kwani hata hao tunaowashikilia na tuhuma hizo hakuna hata mmoja ambaye anashirikiana na kigogo yoyote hivyo ni ngumu kumkamata mtu kwa kusikiliza maneno ya uvumi kuwe na ushahidi na kumpeleka mtuhumiwa mahakamani pasipo kuacha shaka"alisema
Alisema kuwa ili kuweza kufikia malengo wananchi wanapaswa kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa pindi wanapomuhisi mtu kuhusika na biashara hiyo ili kuweza kufanyiwa uchunguzi zaidi bila ya kujali cheo alichonacho.
Kamanda Nzoa alikiri kuendelea kuingia kwa madawa ya kulevya nchini lakini kwa njia ambazo si rasmi hivyo bado juhudi zaidi zinafanyika ili kuwabaini wahusika.
"Kuna njia tatu za wanazotumia hawa wanaofanya biashara za madawa ya kulevya kuingiza nchini kama bahari,ndege na barabarani tumefanikiwa kudhibiti hizo njia zote kuhakikisha hazingii nchini na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, "alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment