Michezo na Burudani

Arsenal kuwapiga bei watano

LONDON, Uingereza

WACHEZAJI Andrei Arshavin, Maroune Chamakh, Squillaci ni wachezaji wanaotajwa kuuzwa huku Manuel Almunia na kipa mwenzie, Vito Mannone wakiwa tayari wameshapewa baraka za kuondokan Emirates.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Arsenal ina mpango wa kuwapunguza wachezaji hao mwezi ujao katika kipindi cha dirisha dogo kutokana na kushindwa kucheza vizuri katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa mjini, Athens Ugiriki.

Arsenal pia itasikiliza ofa ya kumtaka mchezaji Tomas Rosicky, ingawa klabu inahofia kutopata viungo mbadala, huku Jack Wilshere akiwa majeruhi. Arsenal  iliwaacha wachezaji watano katika majira ya joyo yaliyopita.

Wilshere atasubiri hadi wiki hii kuona kama atapewa adhabu kutokana na kuvunja sheria inayokataza wachezaji kucheza kamari ya kutabiri.

Kabla ya mechi ya Jumanne iliyopita dhidi ya Olympiakos, kiungo huyo alisema kwenye mtandao wake kuwa anatabiri Emmanuel Frimpong kufunga bao la kwanza.

Wilshere  baadaye aliandika tena kwenye mtandao wake na kukanusha kutabiri. Shirikisho la soka la Ulaya linakataza wachezaji kuhusika utabiri wa mechi.