19 March 2013

DAWASA ina mpango wa kuongeza mitambo


Na Darlin Said

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) ina mpango wa kuongeza mitambo mikubwa ya maji taka mipya mitatu ya kusafisha mfumo wa maji kwa ajili ya kutatua tatizo la maji jijini Dar es Salaam.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Bw.Archard Mutalemwa wakati akisoma taarifa kwa Kamati ya Maji, Kilimo, Mifugo na Uvuvi iliyohusu hali ya maji na namna walivyojipanga katika kutatua tatizo la upatikanaji wa maji jijini hapa.

Alisema mitambo hiyo mikubwa itaongezwa kutoka asilimia 10 ya utekelezaji wa hivi sasa hadi kufikia asilimia 30 ambapo mtambo mkubwa utajengwa katika Mto Msimbazi na mingine itakuwepo Mbezi Beach pamoja na Kurasini.

Pia alisema zaidi ya lita za ujazo mita 756 za maji zinatarajiwa kuongezeka baada ya kukamilika kwa miradi ambayo itakidhi upatikanaji wa maji hadi kufikia 2027.

Alisema kukamilika kwa miradi hiyo kwa upande wa Mto Ruvu Chini maji yataongezeka hadi kufikia lita milioni 270 kwa siku , Ruvu Juu lita milioni 196 kwa siku, Kimbiji lita milioni 156.

"Lakini kwa pande wa Visima vidogo vitazalisha lita milioni 130 na kuwezesha kuwepo kwa maji ya uhakika hadi ifikapo 2030,"alisema.

"Naye Meneja mradi DAWASCO Bw. Romanus Mwangi, alisema ili kukamilika kwa miradi ya kimbiji na Mpera inahitaji bilioni 56, mpaka kukamilika kwake hivyo aliomba kamati hiyo kuwaunga mkono ili bunge lipitishe bajeti hiyo.

"Kamati tunaomba mtuunge mkono kwani mpaka sasa tumeisha tumia bilioni 18 katika awamu ya kwanza,"alisema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Peter Msolwa aliwataka kuhakikisha miradi iliyo lazima iende sambamba na ongezeko la watu ili kumaliza kabisa tatizo la maji wakati.

No comments:

Post a Comment