11 March 2013

Mbuge CHADEMA kortini kwa uchochezi

Na Jovither Kaijage, Ukerewe

MBUNGE wa Jimbo la Ukerewe, mkoani Mwanza, Bw. Salvatory Machemli (CHADEMA), jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Wilaya hiyo akikabiliwa na shitaka la uchochezi.


Bw. Machemli alisomewa shtaka hilo na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Rouben Luhasha na kulikana ambapo Mwendesha Mashtaka Enis Rwiza alidai kuwa, shitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 23,2011, katika Kijiji cha Nyamanga, kisiwani Ukara.

Alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CHADEMA kwa kuwataka wananchi wachukue uamuzi mgumu wa kuwazuia Maofisa wa
polisi ili wasifanye kazi zao kisiwani humo.

Aliongeza kuwa, kupitia mkutano huo mshtakiwa aliwataka wananchi wamzuie hata kumshambulia kwa siraha za jadi
yakiwemo marungu, mapanga na fimbo Ofisa wa polisi
ambaye atakwenda kuwatafuta washtakiwa usiku.

“Kipindi hicho kulikuwa na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji ya watu wanne waliouwa na wananchi Desemba 10,2010 mbele ya Maofisa wa polisi kwa tuuma za ujambazi.

Alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu 390 na 35 sura 16 ya kanuni ya adhabu  iliyolekebishwa mwaka 2002 na kuongeza
kuwa, upepezi wa kesi hiyo tayari  umekamilika na kuahirishwa
hadi Machi 21 mwaka huu, itakapotajwa tena kwa kusikiliza maelezo ya awali ya upande wa mashtaka. 

Mshtakiwa alipewa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa ya kuwa na wadhamini watatu wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya sh. milioni mbili.

No comments:

Post a Comment