18 March 2013
Waibuka 'kidedea' Shinda Biashara na Majira
Na Anneth Kagenda
WAJASIRIAMALI watatu akiwamo mwanafunzi wa Chuo cha St. Yohana kilichopo mjini Dodoma, Bw. Andrew Manjira, wameibuka washindi wa shindano la “Shinda Biashara na Majira”.
Washindi hao wamejipatia mitaji ya biashara ambayo ni mashine
za kusaga nafaka zenye thamani ya sh. milioni 3.5. Wengine waliopata mashine hizo ni Bi. Mariam Hussen, mkazi wa Morogoro, Bw. Revocatus Anthony, mkazi wa Sumbawanga, ambao wote ni wafanyabiashara.
Akikabidhi mashine hizo Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki,
katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Kampuni ya Business Times Limited (BTL), inayochapisha magazeti ya Majira, Business Times na Sport Starehe, Meneja Biashara wa Gazeti la Majira, Bw. Cecil Mushi, alisema washindi hao wamepatikana kutokana na shindano lililokuwa likiendeshwa katika gazeti hilo.
Bw. Mushi alisema BTL ilishirikiana na Kampuni ya Kishen kuendesha shindano hilo na kutoa mitaji ya biashara ili washindi waweze kutoa ajira, kukuza mitaji yao na kujikomboa kiuchumi.
Alisema lengo la shindano hilo na mengine yanayokuja ni kuwakomboa wajasiriamali na wale wenye mawazo ya kufanya biashara lakini hawana mitaji.
“Wale ambao hawajapata bahati ya kushinda ni vyema wakaendelea kuchangamkia fursa hii kwa kusoma Gazeti la Majira,” alisema.
Naye Ofisa Maendeleo, Biashara na Masoko wa Kampuni ya Kishen, Bw. Prashant Dinesh, alisema lengo la kushirikiana na
BTL katika shindano hilo ni kuwainua wajasiriamali.
“Pia tuna lengo la kuwainua kiuchumi ili wawe wafanyabiashara wakubwa ndio maana tunawapa mitaji...naomba wasomaji wa Majira waendelee kununua gazeti ili waweze kujua shindano linaloendelea na kushiriki,” alisema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kukabidhiwa zawadi hao, washindi hao walisema wamefarijika kuibuka washindi na kwamba malengo yao ya kujikwamua kiuchumi yatafanikiwa
kupitia mitaji waliyoipata katika shindano hilo.
Mmoja wa washindi hao, Bw. Anthony, alisema alisema anajipanga kuwavuta wakulima wengi zaidi ili wapeleke kusaga nafaka zao kwenye mashine yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment