04 March 2013

Hatima ya Ponda kujulikana leo
HATMA ya Katibu wa Junuiya za Taasisi za Kiislam nchini Sheikh Issa Ponda na wenzake 49 itajulikana leo ambapo  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatoa uamuzi kama wana kesi ya kujibu au la, anaripoti Rehema Mohamed.


Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Victoria Nongwa, anayesikiliza kesi hiyo ambapo washtakiwa wa kesi hiyo wanashtakiwa kwa kesi ya uchochezi na wizi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 56.

Februari 27 mwaka huu mawakili wa pande zote mbili katika kesi hiyo waliwasilisha hoja zao za kuona kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu au la.

Wakili wa utetezi katika kesi hiyo, Juma Nassoro, wakiwasilisha hoja hizo aliiomba mahakama hiyo kuona washtakiwa wa kesi hiyo hawana kesi ya kujibu huku akitoa sababu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment