15 March 2013

Polisi aliyeua Mwalimu afukuzwa


Na Mercy James, Njombe

JESHI la Polisi mkoani Njombe, limemfukuza kazi askari wake PC Gelvas Joseph, mwenye namba 9790, kwa kosa la kufanya mauaji
ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo, wilayani Makete.


Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi, Focus Malengo, alisema askari huyo alifanya kosa hilo Februari 27 mwaka huu kwa kumpiga risasi kifuani mwalimu
Castory Sote (31), na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema askari huyo amefukuzwa kazi baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na kubaini alikiuka kanuni za utumishi ambapo hivi sasa anakabiliwa na mashtaka.

Aliongeza kuwa, kosa hilo alilifanya akiwa lindoni kwenye Benki
ya NMB, tawi la Makete, ambapo marehemu alikuwa akichukua fedha katika mashine za benki hiyo.

Ilidaiwa kuwa, siku ya tukio hilo kulitokea malumbano kati ya mwalimu huyo na askari ambaye alimtuhumu marehemu kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu kichwani.

Hali hiyo ilizua mzozo kati yao baada ya marehemu kudai kuwa, polisi huyo si askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

3 comments:

  1. haki imefuatwa nanyi polisi lindo benki na ubu wapi na wapi njoo mpanda nikupe jembee tukalime kilimo kwanza kinalipa

    ReplyDelete
  2. Haki inafuta mkondo wake ila sasa Na Sisi Walimu tuwe na majibu mazuri wakati mwingine maana ukimkuta mwalimu mahali fulani anapoelekezwa utaratibu anakuwa mbishi asietaka kushindwa. Hata kama tumezoea kukimbizana na wanafunzi na kuwataka kutekeleza yale tunayowaambia tusifikiri kwamba tunatakiwa kutoa maagizo kila mahali tunapoenda, sehemu nyingine tuwaelewe wale wanaotuambia na sio kubisha kila kitu mpaka inatughalimu maisha. TUDAI HAKI NA TUFUATE UTARATIBU UNAOSTAHILI. Kufukuzwa kazi na kupoteza maisha kipi bora. Mungu atusaidie.

    ReplyDelete
  3. Haki imefuatwa,polisi siyo mahakama,ni vema kila mmoja kufuata taratibu za kazi,ili usipoteze keki ya taifa uliyo kuwa umeizoea.

    ReplyDelete