19 March 2013

IGP Mwema: Leteni taarifa za uhalifu tuzifanyie kazi


Na Anneth Kagenda

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amewataka wananchi na waandishi wa habari, kutozungumzia na kuandika matukio ya uhalifu ambayo upelelezi wake haujakamilika badala yake kama wana taarifa zozote, waziripoti Kituo cha Polisi ili
ziweze kufanyiwe kazi.

IGP Mwema aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa siku mbili Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ((DCIs) wa Shirikisho la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

“Watanzania wote wakitoa taarifa na kuzipeleka katika mamlaka inayohusika, kwa mujibu wa sheria za mwenendo wa jinai kifungu namba 7, zinasema Watanzania wenye taarifa zozote kuhusu uhalifu utanaotaka kutendeka, kabla haujatendeka au uliokwisha tendeka wapeleke taarifa zao kwenye mamlaka inayostahili.

“Mamlaka zinazopaswa kupelekewa taarifa ni polisi, kituo cha
jirani na Mamlaka za Serikali za Mitaa au kijiji ziweze kufanyiwa uchunguzi hatimaye watuhumiwa waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema IGP Mwema.

Aliongeza kuwa, jeshi hilo halina mamlaka la kujadili ushahidi badala yake kazi waliyonayo ni kupeleleza na kukusanya ushahidi wa matukio ya uhalifu yanayoripotiwa na kuyafikisha mahakamani.

Alisema jukumu la kulinda na kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ni la kila mtu si jeshi hilo pekee na haliwezi kumaliza tatizo la uhalifu bila kushirikiana na wananchi kwani wahalifu
wamo ndani ya jamii hivyo ni vyema wakafichuliwa ili
iweze kuwa salama.

“Pamoja na kuwepo malalamiko mengi na wananchi kuwa jeshi letu halishughulikii haraka upelelezi wa matukio ya utekaji likiwemo la  Dkt. Steven Ulimboka, kesi za upelelezi huwa haziharakishwi kwani suala la upelelezi halina ukomo linaweza kuchukua hata miaka 30,” alisema.

IGP Mwema ambaye ni Mwenyekiti wa SARPCCO, alisema matukio ya utekaji nyara, mauaji, watu kumwagiwa tindikali upelelezi wake lazima uchukue muda mrefu ambapo jeshi hilo
linategemea taarifa kutoka kwa wananchi.

Alisema baadhi ya vyombo vya habari vimeandika habari juu ya kuwepo mikakati ya kuwateka Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia
ni Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP, Bw. Reginard Mengi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe.

Aliongeza kuwa, taarifa hizi ni mzuri kwo na zitawasaidia kujua ni wapi pa kuanzia uchunguzi wao.

Akizungumzia mkutano huo, IGP Mwema alisema una umuhimu mkubwa katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini kwani Tanzania inasifiwa kwa utendaji mzuri wa kukamat shehena ya
dawa za kulevya pia ni nchi ya pili Afrikakwa kudhibiti
uingizwaji silaha.

6 comments:

  1. TAMKO LA IGP SIYO LA KWELI LA KUTAKA ALETEWE TAARIFA ZA UHALIFU AZIFANYIE KAZI.AMESAHAU KWAMBA ALILETEWA TAARIFA ZA MTU ALIYEMTEKA DR.ULIMBOKA NA MATOKEO YAKE WALIFANYIA KAZI KWA KULIFUNGA GAZETI LA MWANAHALISI AMBALO LILITOA TAARIFA ZA MTU ALIYEHUSIKA NA UOVU HUO.SASA ANATAKA TUMPELEKEE TAARIFA GANI KAMA AMESHINDWA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA KWELI?

    ReplyDelete
  2. IGP MWEMA TANZANIA UMBEA NA UDAKU NDIO NYUMBANI KWAKE SINA UHAKIKA UTAWEZA KUJIBU HOJA ZA MAJARIDA 763 ,REDIO 86 NA TELEVISHENI 26 TULIKOSEA KUTOA UHOLELA WA KUBWABWAJA BILA REFA WA KUCHUJA UMBEA NA UDAKU KAWAIDA TAARIFA ZA UONGO ZINANUNULIKA KWA HARAKA ZAIDI KULIKO ZA KWELI

    ReplyDelete
  3. Watanzania tunaishi kwa kupenda taarifa mbaya, halafu furaha ya waliowengi ni pale wanapoona wenzao wanateseka. Hata tukileta taarifa sidhani kama zitakuwa za kweli zaidi ya zile za uchochezi. Wewe kama unataka taarifa c unaowataaalamu(wapelelezi), watumie vema hao watakuletea taarifa za kweli kama nao uliwaajili kwa sifa zinazostahili vinginevyo watakudanganya. Tumeona watu wakijitangaza hadharani kuwa ni Maafisa Usalama wa Taifa, Sasa sijui wanaruhusiwa au vipi.na kama hawaruhusiwi sidhani watu kama hao wanaweza kukuletea taarifa za kweli!

    ReplyDelete
  4. IGP MWEMA KWANZA NIKUPONGEZE KWA UJASIRI WAO WA KUFANYA JITIADA ZA MAKUSUDI KAIKA KUHAKIKISHA UHARIFU UNAPUNGUA KWA KASI ILA NI UNGANE NA WAHAGIAJI WENGINE KWAMBA BADO UNAYO KAZI KUBWA KWA WATENDAJI WAKO KUHAKIKISHA MNAFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADII MLIYOJIWEKEA TAARIFA ZIPO ILA UPOKEAJI WA TAARIFA NA JINSI ZINAVYOFANYIWA KAZI NDIO TATIZO JIPANGE KAKA

    ReplyDelete
  5. kweli IGP hatuna! Yaani waombe na kusomeshwa kazi ya upolisi halafu warudi kutuomba sie tufanye kazi yao ndipo nao wawajibike? Kama umeshindwa kupata taarifa za uhalifu kiintelijensia ondoka wapishe wengine wataotoka kutafuta taarifa bila kutomba sie tusio hata na baiskeli tumpelekee taarifa! Aaakh! Unatia kinyaa bora 2015 ifike uondoke na shemeji yako! Mumesabsbisha nchi iendeshwe kimafia!

    ReplyDelete
  6. Na nyie mnaoshabikia ujinga, mara oo polisi jamii, mara ulinzi ni wa kila mtu! Mbona wasiseme na mashangingi ni ya kila mtu? Au waseme pesa ni ya kila mtu twende benki kuchukua au kuzihesabu? Kuna mgawano wa kazi katika jamii. Aliyechagua kuwa askari na alinde na vita ikitokea na apigane! Aliyechagua kuwa daktari atatibu hata ikiwa usiku au mgonjwa ananuka! Mwalimu na chaki hata kama mshahara unachakachuliwa! Kila mtu na akzi aliyoomba kufanya! Mbona hatusikii madaktari wakisema kila mtu ni mlinzi wa afya ya mwenzie na sote tuanze kuchoma wagonjwa sindano? Hawa askari tumewazoeza wenyewe, wakishindwa kazi tuwasaidie, vita ikitokea watulazimishe kwenda kuwasaidia, magari yetu wapande bure, wakinyanganywa msichana wanapiga kijiji kizima! Tusimame tukatae, tuanze na hili la wao kutaka tuwafanyie kazi waliyosemea na wanayolipwa mshahara.

    ReplyDelete