11 March 2013

Wafariki papo hapo katika ajaliNa Steven William, Muheza

WATU wawili wamefaliki dunia papo hapo baada ya malori
mawili kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika Kijiji
cha Kilapula, kilichopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.


Akizungumza na Majira, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Massawe, alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa
kuamkia jana ambapo malori hayo yalikuwa ya mizigo.
atu wawili kufa papo hapo wakiwa ndani ya magari hayo.

Alisema lori moja lilikuwa likitokea Tanga Mjini na lingine
lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Tangau na baada
ya kugongana, yalilipuka moto na kusababisha vifo vya
watu hao ambao waliungua moto.

“Gari hizi zimeteketea vibaya, hadi sasa zipo katika maeneo
ya Kilapula, kwa sasa tunafanya mpango wa kuyatambua majina
ya watu waliokufa na majeruhi,” alisema Kamanda Massawe.

No comments:

Post a Comment