20 March 2013

Kituo kikubwa cha kuzalisha gesi kujengwa nchini


OSLO, Norway

KAMPUNI za Statoil na BG Group, zinatarajia kutumia dola za Marekani bilioni 10 kujenga kituo cha kuzalisha na kusafisha
gesi ya asili nchini Tanzania ili kuiuza Asia.


Hatua hiyo inatokana na Kampuni ya Statoil kutoka nchini Norway, kugundua uwepo wa gesi nyingi Pwani mwa Tanzania.

Mkuu wa Kitengo cha Uchimbaji wa kampuni hiyo, Bw. Tim Dodson, aliyasema hayo juzi kutokana na utafiti waliofganya kwenye Bahari ya Hadi na kugundua uwepo wa gesi yenye
ujazo wa trilioni nne hadi sita.

“Tunafanya kazi na BG ili kuja na makubaliano ambayo yataweka mambo sawa katika maeneo husika, tunapaswa kukubaliana na mamlaka husika nchini Tanzania wakati tunaingia katika hatua
ya pili,” alisema Bw. Dodson wakati akizungumza na Shirika
la Habari Reuters.

Aliongeza kuwa, gesi waliyoigundua katika bahari hiyo huenda ikawa na ongezeko kubwa kwani rasilimali hiyo inaonekana ni nyingi nchini Tanzania ambapo kwa mujibu wa Reuters, BG imevutiwa na ushirikiano uliopo kati ya kampuni hiyo na
nyingine ya Ophir Energy.

Mwanzoni mwa wiki hii, Kampuni ya BG ilitangaza utafiti wake umefikia katika hatua nzuri za uchimbaji wa gesi Tanzania.

Katika hatua nyingine, Wanajeolojia kutoka nchini Marekani wanadai gesi ya asili inapatikana kwa wingi katika mwambao wa Tanzania, Kenya na Msumbiji kuliko Nigeria ambayo ni nchi
kubwa kwa uzalishaji wa nishati ya mafuta.

Reuters liliongeza kuwa, Afrika Mashariki imeanza kuvutia watu katika sekta ya mafuta kutokana na uhitaji mkubwa wa gesi katika Asia.

“Statoil na BG katika ujenzi wa kiwanda hicho, tutakuwa tunapitia japo hatua mbili, kwanza kuiandaa gesi katika kitalu namba mbili kinachosimamiwa na Statoil na kitalu namba moja cha BG kwa nyongeza kutokana na ujazo wa 10-13 (tcf) ambao tunao.

“Kama ujazo huo utafikia 20 (tcf), wataangalia nini kifanyike ili
gesi hiyo iweze kuandaliwa vizuri, kiasi hicho cha fedha kitatumika katika shughuli hiyo na uwekezaji utafanyika ndani ya miaka mitatu, kabla ya mwaka 2016,” alisema Bw. Dodson.

Wakati huo huo, Mwandishi Peter Mwenda anaripoti kuwa, Wizara ya Nishati na Madini, imeingia mkataba wa utafiti wa gesi, mafuta na Kampuni ya JACKA Resources Ltd ya Australia.

Waziri wa Wazara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana na kuongeza kuwa, watafiti hao wameingia mkataba wa miaka 11 ambao umegawanyika sehemu tatu.

Alisema utafiti  huo utafanyika katika eneo la Ruhuhu mkoani Ruvuma, Njombe na utakuwa wa miaka minne kwa kila awamu.

Aliongeza kuwa, awamu ya kwanza ya mradi huo kama mafuta na gesi itagundulika, kampuni hiyo itachukua asilimia 50 ya mapato
na serikali ya Tanzania asilimia 50.

Alifafanua kuwa, baada ya hapo Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania nchini (TPDC), nayo italipa kodi asilimia 30 na kampuni hiyo italipa asilimia 30 ambazo zitatokana na mapato yao ya asilimia 50.

Awali akizungumza katika mkataba huo, Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Scott Spencer, alisema wao ni wazoefu katika kazi hiyo kwani waliwahi kufanya utafiti katika Bara la Afrika na kufanikiwa kugundua mafuta ya petrol kwenye Ziwa Albart nchini Uganda.

Alisema mradi huo utagharimu dola milioni 20 hadi 50 ambazo ni sawa na fedha za Tanzania sh. bilioni 80.

7 comments:

  1. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya baraka alizotupatia Tanzania hasa kwenye mali asili kama Bahari, maziwa yenye samaki wengi, milima mabonde ya ufa yenye wanyama na ndege na maji ya moto kama Manyara ambayo ni vianzio vya umeme, mbuga za wanyama ,kama SERENGETI ambayo ina kila mnyama apatikanaye duniani, maenneo ya utalii kama Oldvai George eneo linalosemekana kuwa ndio mwanzo wa uhai wa binadamu na wanyama madini ya aina mbalimbali na sasa Mungu kaipatia Tanzania hazina kubwa ya gesi asilia karibu eneo lote la mwambao wa bahari ya hindi na baadaye yatafuata mafuta

    Namshukuru Mungu kwa sababu kwa neema hiyo hapo juu nchi yetu ingekuwa sawa na pepo au nchi nyingi zilizoendelea kama utajiri huo ingetumika vizuri

    Yaliyopita sii ndwele tugange yajao ni msemo wa kiswahili kama hayakufanyika basi tuanze na hili kubwa la gesi asilia

    Kwa mtazamo wangu sioni kwanini tuanze kufikiria kuuza gesi asilia , kwanini lakini hatujifunzi kwa yaliyopita, tulipochimba madini ya dhahabu na almasi tuliwaruruhusu wachimbaji kujenga viwanja vya ndege kwenye machimbo hayo ,matokeo yake tulishindwa kuwadhibiti wachimbaji na usafirishaji wa madini hao tuliona yaliyofanyika huko kwenye machimbo hayo, mauaji , dhahabu kutoroshwa na mabox kuandika viwango tofauti , hakuna TRA HUKO NANI AHAKIKI madini hayo

    Matokeo yake baada ya dhahabu au almasi kwisha ardhini watatukabidhi mahandaki yetu na hakuna faida yoyote itakayokuwa imepatikana. Mheshimiwa baba wa Taifa marehemu Nyerere aliwahi kusema wakati wa kuchimba madini hayo bado aliona mbali, aliwajua hawa wachimbaji kuwa si wanavutia kwao na alisema ngoja tuwe na wataalamu wetu na sidhani kama tayari tuna wataalamu wetu wa kutosha

    Sasa hili la gesi asilia makala moja toka Norway huko nyuma waliwahi kuandika jinsi walivyotafuta gesi kwa shida huko Norway na walipoipata waliwapeleka wataalamu wao kusomea na kujua jinsi gani kuendeleza nchi yao kutumia gesi hiyo ndiyo maana sasa wamekuwa hodari

    Sasa kwa vile wana wataalamu wanatushauri tujenge kiwanda cha kuuza gesi hiyo huko India , hawa ni kama wanatupoteza kwanini tusiwakaribishe wahindi waje kuwekeza hapa nyumbani wajenge viwanda hata vya kutengeneza magari kila mkoa na kuwasamehe ushuru badala ya kuwauzia na wao kupata mabilioni ya faida kutokana na gesi yetu

    Nchi yetu ni kubwa kuanzia kusini hadi kaskazini Mtwara hadi Mwanza / Dar hadi Kigoma , mbeya hadi Kilimanjaro tunaweza kujenga viwanda vingi mno na kwa kutumia wingi wa gesi hii tukawa matajiri kushinda nchi nyingine yoyote duniani

    Lakini tunapoanza kuuza je nani anafuatilia fedha hizo , hapo nyuma tulisikia baadhi ya watanzania wana mabilioni huko Uswisi mpaka leo serikali haijaweza kurejesha fedha hizo kwa maendeleo ta Taifa ,je hilo hamlioni .

    Ni bora tukawa na viwanda kama alivyoshauri mheshimiwa Lowassa ili kuwapa vijana AJIRA kuliko kuanza kuuza na kuwakosesha Tafa ajira na zaidi kujenga mtaji utakaoishia mikononi mwa wachache

    Wananchi wa Mtwara walipoandamana gesi isitoke Mtwara ni kwasababu walitaka maendeleo kwanza na gesi hiyo na kuwapa wana Mtwara AJIRA kwanza

    Naomba sisi kama watanzania tusikubali gesi yetu kuanza kuuzwa nje ya nchi wakati watanzania bado tunapikia kuni NA WATOTO WETU HWANA AJIRA LETENI VIWANZA WEKEZENI HAPA NCHINI

    Kubwa zaidi gharama mnayowauzia ni ndogo sana kwanini tugawane mali asili zetu nusu kwa nusu , Baba wa Taifa alisema tusubiri NAMI NAUNGA MKONO tusubiri hadi tutakapo kuwa na wachimbaji wetu wenyewe kama hatutaweza kuwashauri kuwekeza nchini na kuwa na faida ya angalau asilimia 80


    Namwomba mheshimiwa Raisi kuliangalia hili kwa mtazamo wa AJIRA kwa sababu limekuja kwa wakati ambao watanzania wengi wanamaliza vyuo na hawana AJIRA

    Mungu ibariki Tanzani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dear watanzania, why do we always have to give it away what we have, it is easy to let other to handel it for us,but wat do we gain aftel all.
      look about the victoria fish project, alie kula mifupa ninani????
      from Holland

      Delete
  2. Kwa ninigesi yetu ikauzwe nje halafu tugawane nusu kwa nusu? Tanzania kuweni macho mashimo ya dhahabu mlioyoachiwa bado serikali haijifunzi tu? Mnataka kuzua tena balaa jingine gesi ikauzwe mpaka Urusi? Mali tuliyo nayo tungeyatumia kwa busara sisi tungekuwa 1st class developed county, tutavuna ujinga wetu, huwezi kuotesha bangi utarajie kuvuna mchicha!!!! Serikali iwe macho inadanganywa na hao mabepari. Mikataba mnaandikiwa hamuisomi undani wake mnajifunga wenyewe - mtaleta tean IPTL nyingine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo una mawazo mazuri lakini ukasahau kwamba hatuna technologia ya kuchimba gesi. Sasa labda ushauri iachwe tu mpaka tupate teknologia ama tupunjwe lakini ichimbwe. Sijui wewe ulisomea ninni mwenzangu. Ungesomea petroleum and natural gas extraction ningekupongeza sana vile ndio wakati wa kulikomboa taifa

      Delete
  3. TATIZO NYINYI MAZUZU [ZERO RASILIMALIWATU] CHIMBENI WENYEWE MUKAUZE IWEPO MUNA TEKNOLOJIA NA MITAMBO KAMA MIDOMO NDIO UTENDAJI MUTAFANIKIWA SHIDA MUNAZUNGUMZA SANA UTENDAJI SIFURI NCHI IMEJAZA MAPROFESA WA POROJO HATA NJITI YA KIBIRITI NA SINDANO TU HAWAWEZI KUZIUMBA ILA WAKIUZA SURA KWENYE LUNINGA MAZUZU WANASHANGILIA MTU SI YULE JAMII FORUM WANAOJENGA NYUMBA MBINGUNI KAMA ABUNUWAS

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAPO UMETUELEZA UKWELI BWANA. LABDA RAFIKI ZETU HAWA WAPEWE KUCHONGA VINYANGO NA KUUMBA VYUNGU WATAWEZA. lAKINI KAZI YA MTAMBO, WEWE MUAMBAIE HUYO DOMOKAYA AKATENGENEZE KASINDANO TU UTAONA TAKAVYOKUKWEPA UTAFIKIRI UNAMDAI.
      HAWA WASWAHILI BWANA KUMBE HUWAJUI. UKIJENGA HATA BANDA LA KUKU ZURI ONA WATAKAVYOLALAMA.
      UKIENDA SHULE, OOH HAFAULU HUYO. UKIFAULU VIZURI, KAIBA MTIHANI
      UKIPANDA CHEO, BOSI ANA UPENDELEO.
      hABARI NDIO HIYO.
      ACHIA GESI ICHIMBWE NA WALIOKWENDA SHULE NAWEWE UFAIDI.

      Delete
  4. JAMAA WA KWANZA KAANDIKA KARIBU UKURASA MZIMA LAKINI HAKUNA CHA MSINGI ALICHOANDIKA,,HAKUNA NCHI DUNIANI INAYOCHIMBA MAFUTA AU GESI BILA YA USHIRIKIANO KUTOKA MAKAMPUNI KUTOKA NCHI NYINGINE,,HATA HAO NORWAY WAKATI WANAANZA WALISHIRIKISHA WAGENI KATIKA UCHIMBAJI NA KUGAWANA MAPATO,,RUSSIA YENYEWE NDIO INCHI INAYOONGOZA KWA KUA NA HIFADHI YA GESI LAKINI WANAIUZA GESI YAO UJERUMANI NA ULAYA MAGHARIBI KWA UJUMLA,TUNACHOTAKIWA KUFANYA WATANZANIA NI KUIWEZESHA TPDC IWEZE KUJIFUNZA KUTOKA HAYO MAKAMPUNI YA KIGENI HUKU NAO WAKIANZA KUHUSIKA KWA VITENDO KUFANYA TAFITI,,UCHIMBAJI NA BAADAE UZARISHAJI,,SIO DAWA HATA KIDOO ETI KUSEMA WAPELEKE GESI NJE KUMBUKA BIDHAA SIKU ZOTE INAFUATA SOKO LILIPO ILI KUPATA FAIDA,,TANZANIA HATUNA SOKO LA GESI LA KUTOSHA KWA SASA KURUDISHA MABILIONI DOLA YALIYOTUMIWA NA WAWEKEZAJI KATIKA KUFANYA UTAFITI..WATANZANIA MNAJICHANGANYA MUDA MWINGINE KWA KAULI ZENU,,LIKITAKWA LIJENGWE BOMBA LA GESI ILI KESI ITUMIKE NCHINI MNAKATAA,,IKITAKA IPELEKWE NJE PIA MNAKATAA,,KUONGEA SANA SIO MAANA UNAJUA KILA KITU..

    ReplyDelete