04 March 2013

Maandamano kumpinga Muingereza yaandaliwa


Na Rose Itono

SIKU chache baada ya baadhi ya vyombo vya habari nchi kutoa matangazo yanayohusu udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na raia
wa Uingireza dhidi ya Watanzania, taasisi isiyo ya kiserikali ya Human Settlement of Tanzania (HUSETA), imeamua
kuchukua hatua ya kupinga udhalilishwaji huo.


Taasisi hiyo imeomba kibali kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam ili kufanya maandamano ya amani hadi katika Ubalozi wa Uingereza nchini kupinga udhalilishwaji huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Dagan Kimbwereza alisema,
tayari wamepeleka barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamano hayo Machi 6 mwaka huu.

“Tumepanga maandamano haya yataanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja hadi ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini.

“Wawakilishi wawili watawasilisha azimio lenye saini za Watanzania kuitaka Serikali ya Uingerezaitoe tamko la kutohusika, haisaidii dharau na maovu mengine yanayofanywa na raia wake dhidi ya Taifa la Tanzania,” alisema Kimbwereza.

Alisema Tanzania kama Taifa huru, raia wake wanapaswa kuwa wamoja hivyo kutokana na hali hiyo, hawawezi kuona Rais wa
nchi ambaye wanamuamini akidhalilishwa.

Hata hivyo, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono mandamano hayo yaliyopangwa kuanza saa nne asubuhi
kwa lengo la kuionesha dunia kuwa Watanzania wanajiheshimu.

Bi. Hermitage pia anadaiwa kutoa maneno ya kashfa ambayo yanawadhalilisha viongozi wa nchi, akiwemo Rais Jakaya
Kikwete na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.

1 comment:

  1. haya maandamano ya tija gani wakati ilikuwa kesi ya mengi kugombea shamba na mwekezaji. kaandamane mwenyewe hii kesi tunaijua mwanzo mwisho

    ReplyDelete