26 March 2013

Uwamsho wasomewa mashtaka upya



Na Mwajuma Juma, Zanzibar

KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uwamsho, jana imeanza kusomwa upya katika Mahakama Kuu ya Zanzibar,
mbele ya Jaji Fatma Hamid Mohmoud.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba tisa ya mwaka 2012, walisomewa mashtaka manne na Mwendesha Mashtaka
wa Serikali, Bw. Ramadhani Nassib.

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walisomewa mashtaka ya kuharibu mali, uchochezi, ushawishi, kuhamasisha fujo na
kula njama ambapo mshtakiwa namba nne, Bw. Azan
Khalid, anadaiwa kufanya vitendo vinavyoweza
kusababisha uvunjifu wa amani.

Washtakiwa wengine Farid Hadi (41), mkazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52), mkazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47), mkazi wa Makadara na Bw. Khalid (48), mkazi wa Mfenesini,
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59), mkazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39), mkazi wa Tomondo, Ghalib Ahmada Juma (39), mkazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48), mkazi
wa Misufini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, washtakiwa hao walitenda
makosa hayo kati ya Oktoba 17,18 na 19,2012 katika maeneo
tofauti lakini waliyakana mashtaka yote.

Bw. Nassib alidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo umekamilika ambapo mawakili wa utetezi wakiongozwa na Bw. Taufik Salum,
waliiomba mahakama hiyo iwapatia dhamana washitakiwa hao
kwa sababu tayari wamekaa mahabusu muda mrefu.

“Mheshimiwa Jaji, kwanza tumefurahi kusikia kwa mara ya kwanza kutoka upande wa mashtaka kuwa, upelelezi umekamilika lakini si sababu ya kuendelea kukaa rumande,” alisema.

Hata hivyo, Jaji Mahmoud alichukua maombi ya pande zote na kuahidi kuyapitia kwanza kabla ya kutoa maamuzi kwani kesi
hiyo ameipokea hivi karibuni.

“Nayachukuwa maombi ya mawili wote, ngoja niyafanyie kazi ili niweze kutoa uamuzi unaofaa, naahirisha kesi hii hadi Machi 27 mwaka huu (kesho).

2 comments:

  1. WAMWOMBE SHEIKH SHARIFF HAMAD AWAOMBEE DHAMANA ASIYEAMINI KUWA WAO NI MAGAIDI AFADHILIWE NA PROFESA LIPUMBA ASIYEFAHAMU KUWA SHEHE PONDA NI GAIDI

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha ujinga wewe ugaidi wa ponda ni upi .GAIDI NI PENGO

      Delete