15 March 2013

Pinda ashauri njia za kuepuka tatizo la figo


Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, amewahimiza Watanzania kuwa na tabia ya kunywa maji mengi kila siku ili kujikinga na matatizo ya figo yanayozini kuongezeka kila siku.


Bw. Pinda alitoa wito huo mjini Arusha jana wakati akizungumza
na mamia ya wananchi wa mjihuo waliohudhuria katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Afya ya Figo Duniani ambayo
yaliffanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya AICC.

Kaulimbiu ya siku hiyo duniani mwaka huu inasema “Figo Salama kwa Maisha yako, Epusha Madhara Makubwa kwa Figo” ambapo Bw. Pinda alisema, mtoto wa miaka 10 hadi mtu mzima, anatakiwa kunywa maji yasiyopungua lita moja na nusu kwa siku.

Alisema mtoto mwenye mwaka mmoja, anatakiwa kunywa maji yasiyopungua nusu kikombe (sawa na mililita 100), ambapo kiasi hicho huongezeka kadri mtoto anavyokuwa.

“Hii itasaidia itawasaidia watoto kuhakikisha hawaishiwi maji mwilini, kwa mujibu wa takwimu zilizopo, inakadiriwa kuwa
watu milioni mbili hupoteza maisha kila mwaka kutokana na maradhi ya ghafla ya figo.

Alisema maradhi yanayoweza kujitokeza ghafla na kuharibu figo hayajatiliwa mkazo ipasavyo hasa katika nyanja za utoaji mafunzo ya tiba, utafiti na elimu ya afya ya figo kwa umma.

Aliongeza kuwa, hali hiyo husababisha kutotumika kikamilifu kwa fursa za kubaini maradhi yanayojitokeza ghafla na kuharibu figo ambapo utoaji huduma za afya usiokidhi, husababisha wagonjwa kulazwa muda mrefu hospitalini.

Akifafanua umuhimu wa upimaji afya ya figo, Bw. Pinda alisema Machi 2011, Taasisi ya Figonchini kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ilitoa huduma ya bure na kuwachunguza watu 3,500 ambao kati yao, 1,200 walikutwa na magonjwa ya figo. 

“Mwaka huu, katika maadhimisho yanayoendelea mjini hapa, yaliyoanza Machi 11, watu  2,020 kufikia wamesajiliwa kati yao 1,640 walifanyiwa uchunguzi. 

“Kati yao, 37 walipatikana na  maradhi ya figo na wengine 219 walipatikana na matatizo ya shinikizo la juu la damu, watu 65 kati
ya 141, waliofanyiwa uchunguzi kwa kipimo cha Ultra Sound na walikutwa na matatizo ambapo 63, walifanyiwa uchunguzi wa
moyo kwa vipimo vya ECHO na ECG,” alisema Bw. Pinda.

Alisema jukumu la Serikali ni kuhakikisha fedha, vifaa, vifaa
tiba na dawa za kukabiliana na ugonjwawa mshtuko wa figo, vinapatikana kwa wakati ili kulinda afya ya jamii.

“Katika kudhihirisha azma hii, tayari tuna Kitengo cha Huduma za Tiba ya Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambacho kinatoa huduma kwa wagonjwa wote wanaohitaji tiba ya figo, pia Chuo Kikuu cha Dodoma kimeanza kutoa huduma hii,” alisema.

No comments:

Post a Comment