18 March 2013
Raila Odinga afungua kesi kumpinga Kenyatta
Na Isaac Mwangi, EANA
ALIYEKUWA mgombea urais nchini Kenya kutoka Muungano
wa CORD, Bw. Raila Odinga, amefungua kesi katika Mahakama
ya Juu nchini humo kupinga ushindi wa Bw. Uhuru Kenyatta, ambaye alishinda kiti hicho kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika
Machi 4 mwaka huu.
Bw. Odinga ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi
huo, anaiomba mahakama hiyo itengue matokeo ya urais.
Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya pingamizi hilo katika kipindi cha siku 14.
B. Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ni mtoto wa Rais wa kwanza nchini humo, Bw. Jomo Kenyatta, wakati Bw. Odinga ni mtoto wa aliyekuwa
Makamu wa Rais nchini humo, Jaramogi Odinga.
CORD kinaamini kuwa, mahakama hiyo itasikiliza ombi lao na kutengua matokeo hayo. Wakili Kiongozi wa CORD, George Oraro, alisema wana ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai yaO.
“Tumefungua kesi ya kutafuta haki ili kubatilisha uamuzi wa IEBC kumtangaza Bw. Kenyatta kuwa Rais mteule,” alisema Oraro na kuongeza kuwa, tume hiyo haijatoa taarifa zote ambazo CORD inazihitaji lakini wan ushahidi wa kutosha ndio maana
wakaweka pingamizi mahakamani.
Aliwataja wahusika katika kesi hiyo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa IEBC, Bw. Isaack Hassan, Bw. Kenyatta na Makamu wa Rais mteule, Bw. William Ruto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment