26 March 2013
Mbunge kuweka umeme shule za Chalinze
Na Omary Mngindo, Chalinze
MBUNGE wa Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, Bw. Said Bwanamdogo, anataraji kugawa vifaa vinavyozalisha umeme unaotumia mionzi ya jua (sola), katika shule mbalimbali za msingi na sekondari zilizopo jimboni kwake.
Bw. Bwanamdogo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika
hafla fupi ya kukabidhi mabegi na vyeti kwa wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika Shule ya Msingi ya Pakistan Mtete,
iliyoko Kijiji cha Pera, Kata ya Pera, wilayani humo.
Alisema hatua hiyo inatokana na shule mbalimbali jimboni humo kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme hivyo kukwamisha juhudi za walimu kutoa elimu bora na wanafunzi kushindwa kujisomea kipindi cha usiku.
“Msaada huu utambunguza tatizo la uhaba wa walimu ambao
wengi wao, wanapotakiwa kuja kufunisha katika shule husika
huwa wanakataa kutokana na ukosefu wa umeme.
“Muda wowote natarajia kuweka sola katika shule mbalimbali jimboni kwangu hivyo imani yangu ni kwamba, taarifa hizi ni muhimu kwa walimu na wanafunzi ambao ni fursa nzuri kwao
kufundisha na kujisomea kwa bidii,” alisema.
Aliongeza kuwa, mbali ya msaada huo pia anataraji kuanzisha mpango wa kuwepo kwa huduma ya kwanza katika shule hizo
wenye lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapatiwa dawa
wanapopata homa au maumivu ya mwili.
“Wakati mwingine masomo yanapokuwa mengi, yanamfanya mwanafunzi kutojisikia vizuri hivyo kuwepo kwa huduma hii,
itawasaidia walimu kuwapatia huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa kwa wataalamu afya,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment