15 March 2013

Mbwa mwenye kichaa awauma watu watano



Na Israel Mwaisaka, Chunya

WATU watano wakiwemo wanafunzi wawili, wakazi wa Wilaya
ya Chunya, mkoani Mbeya, wameng’atwa na mbwa mwenye kichaa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya kwa matibabu.


Inadaiwa kuwa, mbwa huyo aliwang’ata watu hao kwa nyakati tofauti katika mitaa ya Sinza na Sinjiriri ambapo wanafunzi
waling'atwa asuhubi wakati wakienda shuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Daktari wa Mifugo
wilayani humo, Benedict Matogo, alisema baada ya kupata taarifa hizo, walifika eneo la tukio kuwachukua watu hao na kuwapeleka hospitali kupata chanjo na kuchomwa sindano ya tetenasi ili
kuwakinga na kichaa cha mbwa.

“Matukio yote yalitokea asubuhi kwa nyakati tofauti wakati watu
hao wakienda kazini na wengine shuleni, Kikao cha Matai ya Ulinzi na Usalama Wilaya kililazimika kukaa kikao cha dharura ili kujadili suala hili kwa kina,” alisema Dkt. Matogo.

Aliwataja watu hao kuwa ni Kervin Mpigauzi (10), anayesoma darasa la tatu, Bw. Salumu Simondi (24), Bi. Devota Mzuna (19) Bw. Maneno Zebedayo (39) na Judith Kabigi (15) ambaye
anasoma Shule ya Sekondari Chunya.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu
Wilaya hiyo, Bw. Morris Kinawiro, aliagiza kusakwa kwa mbwa wote waliozagaa mitaani kiholela na kuwaua ambapo katika msako huo, waliwaua 41 kwa kuwapiga risasi ambapo yule mwenye kichaa wananchi walimuua papo hapo

No comments:

Post a Comment