13 March 2013

Viroba 53 vya mirungi vyakamatwa Arusha



Na Pamela Mollel, Arusha

JESHI  la Polisi mkoani Arusha, limekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya mirungi viroba 53, katika matukio mawili tofauti.


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Liberatus Sabas, alisema tukio
la kwanza limetokea juzi asubuhi katika eneo la Kaloleni jijini humo ambapo jeshi hilo lilikamata viroba 22 vya mirungi vyenye uzito wa kilogramu 360, vikiwa katika gari yenye namba T 224 BAQ, aina
ya Toyota Premio, inayomilikiwa na Bw. George Mungu.

Alisema askari waliokuwa doria, walilitilia shaka gari hilo ambapo dereva wake, alishtuka na kukimbia hivyo jeshi hilo linaendelea kumsaka ili kujibu tuhuma zinazomkabili wakati mmiliki wa gari hilo akiendelea kutafutwa kwa hatua zaidi za kisheri.

Tukio la pili lilitokea saa mbili asubuhi katika eneo la Enaboishu, ambapo askari walimkamata Bw. Benjamini Babu (40), mkazi wa Olmatejoo, akiwa na viroba 31 vya mirungi.

Kamanda Sabas alisema, Bw. Babu anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

“Natoa wito kwa watu wote wanaofanya biashara haramu kama
hii na nyingine waache mara moj, operesheni tunayoifanya ni endelevu na inaungwa mkono na watu wengi,” alisema.

Aliwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ambazo zitasaidia kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na biashara haramu, uhalifu pamoja na matukio mengine ili kurudisha sifa ya mji huo.

No comments:

Post a Comment