Na Raphael Okello,Bunda.
WANAWAKE wametakiwa kutosababisha vurugu ndani ya ndoa zao kwa
kigezo cha kudai haki sawa badala yake wameshauriwa kufuata taratibu katika
kudai haki hizo.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Diwani wa viti maalum
wilayani Bunda mkoani Mara,Bi.Mariamu Sindano wakati wa maadhimisho wa siku ya
wanawake duniani iliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Malembeka wilayani
humo.
Bi. Sindano alifafanua kuwa wapo baadhi ya wanawake ambao
hivi sasa wamekuwa mwiba kwa waume zao na familia kwa ujumla kwa kufanya vitendo
vya ukorofi kwa madai kuwa wananyanyaswa huku wakikataa
kutoa huduma muhimu kwa familia zao.
Hata hivyo alikiri kuwa bado kuna mfumo dume wilayani hapo
ambapo aliwataka wanawake kutambua haki zao ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa
mali, kupata mirathi, elimu na haki
zingine za kushiriki katika vyombo vya maamuzi.
Awali akizungumza kwa
niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda, Ofisa maendeleo ya jamii
wilayani Bunda Bi.Karoline Wanzangi alisema lengo la maadhimisho ya siku ya
wanawake kufanyika Kijiji hapo ni kufikisha elimu zaidi kwa akina mama vijiji
ambao ndio wananyanyasika zaidi.
Alisema vitendo vya ukatili vimeendelea zaidi katika maeneo ya vijijini hivyo ni
jukumu la
vyombo vya usalama, maofisa watendaji wa vijiji na kata kuwasaidia akina mama
na watoto wa kike katika kufafanua sheria zinazohusu ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment