18 March 2013
Watoto wachomwa midomo wakidaiwa kula karanga
Na Lilian Justice, Morogoro
JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linamsaka mkazi wa Ujenzi, katika Kata ya Ndege, Bw. Jaribu Bakari, kwa kosa la kuwachoma moto mdomoni wanawe wawili kwa banio lenye mkaa.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo limetokea Machi 13 mwaka huu, saa 10 jioni.
Alisema mzazi huyo aliamua kufanya kitendo hicho baada ya wanawe kudaiwa kula karanga zake za biashara na kuwataka watoto hao kuwa ni Ibrahim Jaribu (10), mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Msamvu B.
Wengine ni mdogo wake, Marik Jaribu (5), ambao wote walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa huo kwa matibabu.
Alisema taarifa za kutokea tukio hilo zilitolewa na walimu wa shule hiyo baada ya kutomuona mwanafunzi huyo shuleni.
Hata hivyo, jeshi hilo linaendelea kumsaka mzazi huyo ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment