18 March 2013

Mhariri Majira kuwania tuzo uandishi mahiri


Na David John

MHARIRI Mtendaji wa Gazeti la Majira Imma Mbuguni ameteuliwa kuwania Tuzo za Uandishi mahiri wa habari,ambapo sherehe zake zitafanyika Aprili 5, mwaka huu Dar es salaam


Katika sherehe hizo Mgeni Rasmi anatarajia kuwa Rais Zanzibar Dkt. Ally Mohemed Shein.

Akizungumza na waandishi habari Dar es salaam jana kuhusiana na washindi watakaongia kwenye kinyang'anyiro hicho Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi AJAT ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Bw.Kajubi Mukajanga alisema majina 66 ya waandishi wa habari yameingia kuwania Tuzo hizo kati ya kazi 946 zilizowasilishwa.

Alisema miongoni mwa majina hayo Bw. Mbiguni ameingia katika kinyany'iro hicho cha kuwania Tuzo ya umahiri wa uandishi wa habari Tanzania.

Bw. Mukajanga alisema washindi hao wamepatikana katika viwango mbalimbali vilivyotolewa na baraza hilo, ikiwa pamoja na tuzo za habari uchumi na biashara, habari za michezo na utamadiuni, mazingira, Afya, watoto, VVU na Ukimwi.

Alitaja nafasi zingine ni pamoja na habari za utawala bora,Jinsia,Sayansi na Teknolojia, majanga, Elimu,watu wenye ulemavu,utalii na uhifadhi, malaria,Mpiga picha bora wa magazeti,mpiga picha bora Televisheni,mchoraji katuni bora,kilimo na Afya za uzazi wa vijana.

Katika hatua nyingine alisema tuzo ya kuwania washindi wa jumla ni majina saba ambapo kati ya hayo anatakiwa mshindi mmoja ambaye atapa tuzo kwa ajili ya kupata tuzo hiyo

Pia alisema kwa upande wa tuzo ya maisha ya mafanikio katika Tasnia ya habari yameteuliwa majina matatu.

Bw.Mukajanga alisema lengo hasa la kuandaa mashindano hayo nikuhimiza ubora wa uwandishi mahiri wa wanahabari nchini na hasa katika kuripoti habari za uchunguzi.








No comments:

Post a Comment