15 March 2013

Mtoto auawa, kunyofolewa macho


Na Elizabeth Joseph, Dodoma

MTOTO Happyness Paulo (3), mkazi wa Kijiji cha Handali,
Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, ameuwawa na watu wasiofahamika na kumchuna ngozi.


Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Handali,
Bw. Julius Maholi, alisema alipotea juzi ambapo mtoto watu hao
walimchuna ngozi kuazia shingoni nadi kichwani, kumnyofoa
macho pamoja na ubongo.

Alisema mama mzazi wa mtoto huyo alimuacha nyumbani akiwa
na watoto wa jirani na yeye kwenda shambani ambapo baada ya kurudi saa sita mchana, aliwakuta watoto wengine wanacheza
lakini mtoto wake hayupo.

“Baada ya kuwauliza, wale watoto walijibu hawajui mwenzao amekwenda wapi, huyu mama pamoja na waananchi wengine waliamua kumtafuta katika maeneo mbalimbali.

“Wakati wakiendelea na kazi hiyo, ilipofika jioni walimuona
kwenye vichaka amelala akiwa amekufa na kuchunwa ngozi,
huu ni unyama mkubwa aliofanyiwa,” alisema Bw. Maholi.

Aliongeza kuwa, mwili wa marehemu kuanzia shingoni hadi miguuni haukuwa na jeraha lolote na alikuwa amevaa gauni
lake kama alivyoachwa na mama yake.

Bw. Maholi alisema, wakazi wa kijiji hicho wanalihusisha tukio
hilo na mauaji ya kishirikina kwani hakuna historia ya wanyama wakali kuvamia katika kijiji chao.

“Mwili wa marehemu ulichukuliwa na polisi ambao walikwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Mvumi,” alisema

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mvumi Makulu, Hiyana Makulo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai bado hawajajua
mazingira ya kifo hicho.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, David Misime, alikiri kupokea taarifa za kifo hicho na kudai jeshi hilo halijapewa taarifa rasmi kama mtoto huyo alichunwa ngozi na kuahidi kutoa taarifa kamili baadaye.

No comments:

Post a Comment