08 October 2012

Mbunge wa zamani kuibuka kidedea NEC

Na Faida Muyomba, Geita

MBUNGE wa zamani wa jimbo la Nyang'hwale  mkoani Geita,Bw. James Msalika,ameibuka kidedea  katika nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha Mapinduzi (nec)Taifa kupitia wilaya mpya ya Nyangh'wale, baada ya kuwashinda wapinzani wake watatu.


Bw.Msalika aliyekuwa mbunge kwa muda wa miaka 12 aliashindwa kugombea ubunge, baada ya kuangushwa na mbunge wa sasa wa jimbo hilo Bw.Hussein Amari wakati wa kura za maoni ndani ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana katika ukumbi wa shule ya sekondari mjini mjini Geita,Bw.Msalika alipata kura 503 kati ya kura 585 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu huo wa uchaguzi.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa Mkoani Mwanza,Bw.Kambandu Samweli aliwatangaza wagombea wengine katika nafasi hiyo kuwa ni dkt.Peter Mwinginga aliyepata kura 57 na Bw. Jacob Nyanda ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyijundu kura tisa.

Kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani humo,msimamizi huyo alimtangaza Bw.Adam Masudi Mtore kushinda kiti hicho kwa kupata kura 325,huku wapinzani wake Bw. Mayunga Magiri (235) na Sostheness Ngusa akipata kura 25

Wajumbe watano wa mkutano mkuu wa CCM Taifa waliochaguliwa ni. Bi Helena Shija,Bi .Agatha Marugumba,Bi .Veronika Makonge,Dkt Leonard Mugema na Donald Kabosolo huku Said Lufunga Madoshi akichaguliwa kuwa Katibu wa itikadi na Uenezi wilayani humo ambapo Bw. Richard Glani  alichaguliwa nafasi ya Katibu wa uchumi Wilaya.



No comments:

Post a Comment