11 March 2013

CCM yabaini 'madudu' katika miradi yake



Na David John

KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Zakia Meghji, amesema mikataba ya muda mrefu iliyosainiwa
na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika vitega uchumi vyake, imechangi wakose mapato ya uhakika.

Bi. Meghji aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, katika ziara aliyoifanya kwenye ofisi za chama katika mikoa mbalimbali nchini, amebaini vitega uchumi vingi vya chama vinamikataba mirefu.

“Ziara yangu ilikuwa na lengo la kuviona vitega uchumi vya chama ambavyo vina thamani ya sh. bilioni 52 lakini bado mapato mengi yanapotea kutokana na mikataba ya muda mrefu ambayo iliingiwa
na viongozi waliotangulia.

“Ili chama chetu kiweze kupata mapato mengi, lazima kuwepo utaratibu wa Sera ya Uwekezaji ambayo itakuwa ikitoa mgawanyo wa mikataba pamoja na kuisimamia kama ilivyo ilani ya chama.

“Kwanini tuingie mikataba ya zaidi ya miaka 100 ambayo haiendani na wakati uliopo hivyo upo uwezekano mkubwa wa chama chetu kupoteza mapato kama ilivyo sasa,” alisema Bi. Meghji.

Alisema ukiangalia mapato yanayoikia kwenye chama na idadi
ya vitega uchumi ni mambo mawili tofauti hivyo ipo haja ya kuhakikisha chama kinakuwa na Sera ya Uwekezaji ambayo  itasaidia kuleta ufanisi wa mapato.

Katika hatua nyingine, Bi. Meghji alizunguzia suala la wanachama wa CCM ambao wanadaiwa kuhusika na ubadhirifu na kufafanua kuwa, Kamati ya Siasa ndiyo yenye jukumu lakubaini nani anasitahili kufanywa nini na kuchukua hatua.

Aliongeza kuwa, ataendela na ziara katika mikoa mingine kama sehemu ya majukumu yake ili kuangalia mali za chama pamoja
na mapato yake lakini kikubwa ni kuhakikisha viongozi
wanachukua hatua ya kusimamia rasilimali zilizopo
kwa faidi ya chama si vinginevo.

No comments:

Post a Comment