18 March 2013

Wajawazito Amana wapatiwa vifaa vya kujifungulia



Na Heri Shaaban

MADIWANI Wanawake wa Maniaspaa ya Ilala wametoa vifaa vya kujifungulia wanawake wajawazito katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo Amana.

Msaada wa vifaa hivyo vya kuzalia kwa wanawake vilikabidhiwa Dar es Salaam jana,wakati wa ziara ya Kamati ya huduma za Jamii na Idara ya Usatawi wa Jamii Ilala waliotembelea hosptalini hapo.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii Ilala,Angelina Malembemka alisema kuwa katika kuadhimisha kielele cha siku ya wanawake Duniani,wanawake ndio tumepanga kuwapa vifaa hivyo.

"Tunafahamu matatizo wanayokumbana nayo wanawake wenzetu ndio maana leo tumeadhimisha siku hii leo kwa kutoa misaada, ambapo tunaitimisha ziara yetu leo kwa kuwatembelea wanawake wenzetu  kwa kuwafariji.alisema Malembeka.

Kwa upande wake Katibu wa Hospitali hiyo,Tunu Mwachaly alisema kuwa hosptali hiyo ina mrundikano wa wanawake wajawazito wengi, ambao wanajifungulia hapo, ambapo kitanda kimoja ulazimika kulala wanawake watatu.

Tunu alisema kuwa katika kuthibitisha hilo jana walipokea idadi ya wanawake 167 kati yao wanawake 100 wamejifungua salama 15 kwa upasuaji na 67 bado kujifungua.

Alisema kuwa changamoto ni kubwa kutokana idadi kubwa ya wanawake ambao wanajifungulia hapo alishauri wanawake wengine wajifungulie katika vituo vya afya vilivyo karibu ambavyo vinatambulika na Wizara ya Afya.

Alisema kuwa takwimu za mwaka 2013 jumla ya wanawake wajawazito 29700 walijifungulia hosptali hiyo kati yake wanawake 18 walikufa kwa uzazi.

Aliwashauri wanawake wajawazito wakimbilie vituo vya vya afya mapema pindi uchungu unapoanza,kabla uchungu kuzidiwa ili kupunguza idadi ya vifo kwa kujifungulia njiani kabla kufika kituo cha afya.

No comments:

Post a Comment