04 December 2013

MPASUKO ZAIDI CHADEMA

 • M/KITI SINGIDA AJIUZULU, ASEMA HAKUNA DEMOKRASIA


Damiano Mkumbo na Darlin Said

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Singida, Wilfred Kitundu, amejiuzulu rasmi nafasi hiyo akipinga mambuzi ya Kamati Kuu kuwavua nyadhifa za uongozi viongozi wake watatu.


Viongozi hao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.Akikzungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Kitundu alisema kinachoendelea ndani ya chama hicho kwa sasa ni udhalilishaji wa demokrasia ya kweli.

Alisema uamuzi aliochukua ni hiari yake bila kushawishiwa na mtu akiwa na dhamira ya kulinda demokrasia ya kweli ili kuhakikisha inaimbwa na kutekelezwa kwa vitendo."Mimi ni mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA, mkoani hapa pia ni mwanachama wa 300 kitaifa, ninayo heshima kubwa kwangu, sipo tayari kuipoteza heshima hiyo kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia.

"Nitaendelea kuwa mwaminifu na mwadilifu ili kutetea haki na Demokrasia siku zote bila kurudi nyuma," alisema na kuongeza kuwa, kitendo cha kumvua nyadhifa za uongozi Bw. Kabwe na wenzake si kizuri na kimeacha maswali mengi yanayoulizwa na wanachama wake," alisema Kitundu.

Aliongeza kuwa, msimamo wa CHADEMA mkoani humo ni kulaani, kupinga na kukemea maamuzi hayo ambayo yamejaa chuki, hofu na wasi wasi mwingi hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ndani ya chama.

Katika barua yake ya kujiuzulu ambayo alimwandikia Katibu Mkuu wa chama hicho mkoani humo, alisema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bw. Freeman Mbowe, anapaswa kutoa neno ili wanachama na wananchi waendelee kikielewa vizuri chama hicho badala ya kikigawa vipande.

"Msimamo mwingine ni kumtaka Bw. Mbowe na Katibu Mkuu,Dkt. Wilbrod Slaa, kuitisha mara moja mkutano wa Baraza Kuu la chama ili kutoa maamuzi ya suala hili kwani lilifanywa na watu wachache kwa masilahi yao," alisema.

Alishauri jambo hilo ni la msingi sana na maamuzi ambayo yatatolewa yame makini ili kudumisha hali ya utulivu ndani ya chama kiendeleze umarufu wake kwani ipo siku kinaweza kuongoza dola.Kitundu mbali ya kushika nafasi ya Mwenyekiti wa chama Mkoa, pia aliwahi kuwa muasisi na mlezi wa CHADEMA
(1992-2013), Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (1992-2013) na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (1992-2013).

Katika hatua nyingine, Katibu wa CHADEMA mkoani humo,Bw. Patric Msuta, amekiomba chama hicho kuitisha kikao cha Kamati Kuu kikae meza moja na viongozi wenye mgogoro na chama ili kumaliza tofauti zilizojitokeza.

Bw. Msuta aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano wake waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, tangu mgogoro huo uanze, hakuna mwanachama aliyerudisha kadi."Hapa Singida, chama chetu hakina mpasuko wowote kwani wanaelewa vizuri msingi wa maamuzi wa Kamati Kuu kutokana na mgogoro uliyopo ndani ya chama chetu ambao naamini utamalizika kwa njia ya amani," alisema.
 

14 comments:

 1. Majira,
  Mbali na kutoa taarifa za baadhi ya viongozi wanaojiuzuru hebu kama mna divisheni ya utafiti itumieni ili ikusanye maoni juu ya matatizo ya hawa wanaharakati "Kama Joseph Khonyi" muone wangapi wanaunga mkono Zitto kuvuliwa nyadhifa, wangapi wanakataa Zitto kuvuliwa.

  Kisha ripoti hiyo watanzania waijue.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

  ReplyDelete
 2. Usicheze na pesa. Zito sasa kwisha! Ashasahaulika. Wenzake wana pesa ya kutosha kuruka ncchi nzima. Ni zaidi ya serikali. Wanatembeza ubabe kama dola vile

  ReplyDelete
 3. Wenye akili mgando, wasiosoma, na matusi mengine mengi yameirudishia fadhila CHADEMA. Wamepewa kata tatu kati ya ishirini na saba. Tunawasubiri uchaguzi mkuu mtueleze vizuri kwanini mnatutukania wazee wetu kwamba wanadanganyika na kofia na kanga za CCM. Rusheni helkopta zenu sie tutatembea kwa miguu.

  ReplyDelete
 4. thanks for good sharing information

  ReplyDelete
 5. En el canto.

  Siento radiante
  un canto y
  una rima pasar
  donde el sueño
  describe la noche
  y una tierna
  poesía.

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete
 6. Le sourire et le conte du cœur.

  Quelquefois
  le murmure de
  la soirée m'invite
  à traduire le
  chant de la mort,
  et alors le sourire
  devient le manteau
  et un son délicat.

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete
 7. http://agenhammerofthorasli.com/fruit-plant-obat-pelangsing-badan-ideal-di-balikpapan-antar-gratis/

  ReplyDelete
 8. La clarté des sentiments.

  Dans le reste
  de la soirée
  je vois une
  lumière et le
  tendre cadeau
  d'une chanson
  très joyeuse.

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete
 9. En el canto.
  ( last version )

  Cuando viene
  una sombra
  invocando el
  candor de la noche
  estrellada siento
  un llanto y una
  rima avanzar
  suavemente en
  el sueño encantado
  de una tierna
  poesía: la emoción
  reaparece, un eterno
  sonido se difunde
  en el viento regalando
  la gracia de la nueva
  armonía.

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete
 10. Le souffle des sourires.

  Quand le chant
  de la neige
  revient tendrement
  où l'eau disparaît
  j'écoute, en silence,
  la route des
  sourires.

  Francesco Sinibaldi  Quand le son disparaît...
  ( other version )

  En marchant sur
  le sentier qui traverse
  la douce campagne
  je médite sur le présent
  qui rappelle une
  sensation: c'est très
  agréable décrire
  la lumière qui
  couvre le passage
  de la brise qui
  retourne...

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete
 11. The martin's song.

  In the light
  of a white
  rose there's
  a delicate
  swallow, the
  sound of a
  stream and
  a gentle delight.

  Francesco Sinibaldi

  ReplyDelete