Na Veronica Modest
Musoma.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa na wajumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mara kwa
kufanikisha kutekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 kwa kipindi cha julai
2011 hadi June 2012.
Pongezi hizo zilitolewa
hivi karibuni na wajumbe hao katika
kikao cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha
mapinduzi ya mwaka 2010 kwa kipindi cha
julai 2011 hadi june 2012 kilichofanyika katika ukumbi wa
chama hicho mjini Musoma mkoani Mara.
Akiwasilisha taarifa hiyo ya utekelezaji mbele ya wajumbe
hao Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw.Joseph kalinga alisema kuwa katika
kipindi cha mwaka wa fedha wa
2011/2012 mkoa ulipangiwa kukusanya jumla ya
shilingi Bil.63,483,100,000.00 hivyo katika kipindi hicho mamlaka
ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bil.55,609,172,170.00 sawa
na asilimia 88 ya lengo.
Katika kutekeleza ilani ya
uchaguzi ya CCM,mkoa ulipangiwa
kukusanya jumla ya shilingi Bil. 9,227,876,122.00 toka katika vyanzo vyake vya
ndani lakini
hadi kufikia 30,juni 2012 mkoa ulikuwa umekusanya jumla ya shilingi
Bil.5,955,038,283.00 sawa na asilimia
64.5 ya makusanyo.
Kalinga aliongeza kuwa mafanikio yanayopatikana yanatokana na ushirikiano mzuri wa
watendaji
kazi wake kutokana na kujituma wenyewe bila kusukumwa na mtu kwa kuwa ni wajibu
wao kufanya kazi.
Nae mkuu wa mkoa wa Mara Bw.John Tuppa aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika
kujiletea maendeleo ya mkoa wao kwa kulipa kodi.
“Naomba wananchi mjitokeze,mlipe kodi kwa wakati na hata
wale wanaojificha kulipa msifanye hivyo kwani mnajirudishia maendeleo yenu
wenyewe”alisema Tuppa
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) Butiama Bw. Marwa
Siagi alisema kuwa mbali na mafanikio wanayoyapa waendelee kuwashawishi
wananchi kulipa kodi kwa wakati
kuharakisha kasi ya maendeleo.
Alisema kwa wale wanaokwepa kulipa kodi kwa wakati husussani
wafanyabiashara wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwa hakuna maendeleo yoyote
yasiyoletwa na wananchi hivyo ni lazima
wawajibike katika kulipa kodi.
No comments:
Post a Comment