18 March 2013
'Serikali angalieni upya maslahi ya walimu'
Na Mercy James,
Mufindi
SERIKALI imetakiwa kuangalia upya maslahi ya walimu ili kuboresha taaluma katika shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Wito huo umetolewa katika kikao cha wadau wa elimu kilichoketi katika ukumbi wa halmshauri ya wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa,ambapo pamoja na mambo
mbalimbali wadau hao wamejadili kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu hususani kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2013.
Awali Ofisa Elimu msingi, Bi. Farida Mwasumilwe akisoma tarifa ya elimu kwa wadau hao
wa elimu alieleza changamoto kubwa kuwa ni upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari,ufinyu wa bajeti ya fedha za kuendeshea shule, malipo duni kwa
walimu ikilinganishwa na kupanda kwa gharama za maisha, na mwamko duni kwa wazazi katika malezi ya watoto wao.
Aliongeza kuwa kutoka na kukosa haki zao walimu wanakosa ari ya kutoa huduma iliyo bora katika ufundishaji na pia uwajibikaji kufanyika kwa kusukumwa.
Bw.Cyprian Tweve alisema ni mdau kati ya waliochangia hoja zao katika kikao hicho ambapo
amesisitiza kuwa serikali ione umuhimu wa kuthamini sekta ya elimu kwa kutenga bajeti kubwa kama inavyotenga katika sekta ya miundombinu ya barabara, mifuko ya wabunge itumike kuchangia kuboresha mazingira ya shule kuwa rafiki wa mwalumu na wanafunzi kwa kuweka nishati ya umeme wa jua shule za sekondari ili kuwapa muda ziada kujisomea.
Naye Meneja wa shamaba la Serikali Shirika la Green Resources Mafinga ,Bw.Jacob Mushi Mafinga, alishauri kutotafuta mchawi ama kutafuta nini chanzo cha ufaulu duni, malipo ya mishahara yanatofautiana kwa kiwango kikubwa na hivyo walimu wanajua kwanini wanafunzi hawafanyi vizuri wao wanadaiwa ya ugonjwa huo.
Upande wake Ofisa elimu vielelezo Bw. Jumma Fuluge alisema wao wamedai kuwa kama mwalimu atatekelezewa madai yake upo uwezekano wa kufanikiwa kubadilisha hali ya elimu katika shule za msingi na sekondari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment