Na Patrick Mabula,
Kahama,
Wananchi wanaoishi eneo la mitaa ya majengo mjini Kahama wamelalamikia kero ya
mafuriko yanayotokana na mvua zinaponyesha na kufanya mitaro kumwaga maji ambayo
huingia na kujaa ndani ya nyumba zao na kuwafanya wazikimbie na kulala nje huku
wengine wakilala kwa majirani.
Wakiongea na Majira mbele Ya nyumba zao zilizokuwa zimefurika maji kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha walisema wamekuwa wakilazimika kuzikimbia nyumba hizo
kutokana na mafuriko hayo yanayosababishwa na mitaro iliyojengwa kupeleka maji kwa
kasi kweny makazi yao.
Bi.Roza Julius alisema nyumba zao zimekuwa zikifurika maji kila mvua zinaponyesha
katika msimu huu na kuwafanya walale nje na wengine kwa majirani hadi asubuhi
wanapofanya kazi ya kumwaga kuyatoa nje .
Bw.Paulo Sambali alisema wamekuwa wakikumbwa na mafuriko kutokana na kasi ya maji
yanayotoka na mitalo iliyoimalishwa na Halmashauri ya mji wa kahama toka maeneo ya
mitaa ya boma , sokoni , nyamwezi , lumelezi , nyihogo ambayo imekuwa ikasababisha
athari.
Bw.Felex Soko alisema kabla ya mitaro hiyo mikubwa iliyopo barabara kuu la lami
hajaimarishwa kupitisha maji walikuwa hawapati tatizo hilo toka ilipopanuliwa mwezi
mmoja uliopita sasa hivi kila mvua ikinyesha nyumba zao zinapata mafuriko.
Bw.Juma Shagile katika malalamiko yake juu ya kero hiyo aliitaka Serikali iwanusuru
na kero hiyo kwa vile imekuwa ikiwasababishia vitu na mali zao kuharibika kutokana
na maji yanayofurika eneo lao na kujaa ndani ya nyumba zao.
Katibu wa Baraza la wazee wa wilaya ya Kahama Bw.Paulo Ntelya aliyeshuhudia tatizo
hilo la alisema kero hiyo wataifikisha kwa viongozi husika wa Serikali kuhusu
wananchi wa mitaa ya majengo wanavyoteseka na mafurika hayo katika misimu huu wa
mvua.
Diwani wa kata ya Majengo Bw.Bobson Wambura alisema katika mitaa hiyo inatokana na
udogo wa mitaro inayopokea maji toka barabara kuu ya rami na kutokana na nyumba
hizo kuwa misingi yake ipo chini husababisha maji kufurika ndani na aliwaahidi
kulifikisha kwa vyombo husika vya serikali liweze kutatuliwa.
No comments:
Post a Comment