08 October 2012

Sumaye: Sina vita yoyote na Lowassa *Akanusha kufanya kuzungumza na CHADEMA *Adai kuanguka NEC ni tiketi ya mapambano zaidi


Na Willbroad Mathias

WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, amekanusha uvumi uliosambaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa ametangaza vita na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa kama atachukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Sinodi yawatema vigogo Kanisa la Moravian


Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kutokea vuta nikuvute kati ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki na uongozi wa juu wa jimbo hilo, hatimaye Mkutano Mkuu wa Sinodi umebariki kuondolewa madarakani viongozi waliosimamishwa akiwemo Mwenyekiti wa jimbo hilo, Mchungaji Clement Fumbo.

'Wanaosema kiama cha CCM 2015 wamepotea'



Na Yusuph Mussa, Korogwe

MJUMBE wa Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. January Makamba, amesema chama hicho hakiwezi kuanguka katika Uchaguzi Mkuu 2015 na wanaosema kimefikia ukingoni kuongoza dola wamepotea.

MSAKO


Maofisa wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kinondoni Kaskazini wakiangalia ramani ya eneo la Mlalakuwa Mwenge, Dar es Salaam juzi lenye nyumba ambazo wizi wa umeme na ujengaji njia za umeme bila kibali. Kushoto ni Mkaguzi, Bw. Dunia Ngaraba, Meneja wa Wilaya ya Mbezi, Bw. Josephat Josef na Msimamizi wa Kitengo cha Dharura, Bw. Jackson Lwehabura. (Picha na Charles Lucas)

Bodi NBC yamrudisha Mafuru



Na Willbroad Mathias

BODI ya Wakurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imetangaza kumrejesha kazini Mkurugenzi Mwendeshaji Bw. Lawrence Mafuru, baada ya kukamilika uchunguzi wa tuhuma mbalimbali ndani ya benki hiyo.

Urais CHADEMA vita kubwa *Katibu BAVICHA naye atangaza dhamira yake



Na Benedict Kaguo,Tanga

VITA ya kuwania urais mwaka 2015, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imezidi kushika kasi baada ya Katibu wa Baraza la Vijana (BAVICHA), mkoani Tanga, Bw. Deogratius Kisandu, kutangaza rasmi dhamira ya kuwania nafasi hiyo.

OPERESHENI


Mkazi wa Bonde la Mkwajuni, Manispaa ya Kinondoni (jina halikufahamika), akiwa amebeba bati alizoezua kwenye nyumba yake wakati wa operesheni ya kuvunja nyumba zilizojengwa mabondeni iliyoanza eneo la Hananasif, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. (Picha na Heri Shaaban)

Utekelezaji miradi ya maendeleo utapunguza umaskini katika jamii


Na Rehema Mohamed

UBUNIFU na upelekeji wa miradi ya maendeleo vijijini ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla.

Juhudi zinahitajika kupambana na mila potofu zinazowakandamiza wanawake



Na Agnes Mwaijega

SERA ya maendeleo ya wanawake na jinsia ni mojawapo ya sera zilizoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha kuwa wanawake kwa wanaume wanashiriki katika shughuli za maendeleo.

Mikakati kuboresha afya iongezwe kuongeza uzalishaji mali nchini



Na Raphael Okello

MWAKA huu mfuko wa Bima ya taifa(NHIF) imetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 ikijivunia kuwafikia
wananchi katika kila Mkoa.

WAKITETA

Waziri wa Katiba na Sherai Mathias Chikawe (kulia) akiteta na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.

Mchakato wa katiba mpya na ubovu wa sheria zetu



Na Debora Mushi

KATIKA nchi yoyote, mfumo wa kisheria ni muhimu sana katika kujadili na kuelewa haki mbalimbali zilizopokwa raia wake. Ni katika sheria za nchi ndipo wananchi wa makundi mbalimbali wanaweza kuelewa na kudai haki zao za kiraia na kibinadamu za kimsingi.  

Kukosa uzalendo chanzo cha kutonufaika na rasilimali



Na Agnes Mwaijega

TANZANIA ni miongoni mwa nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi na zenye uwezo kumfanya kila Mtanzania akaishi maisha mazuri.

BURUDANI

Wasanii wa Kundi la Dance Team Africa cha Arusha, wakitoa burudani  kwenye tamasha maalum la promosheni ya Bia ya Ndovu Special Mart mkoani Arusha lililofanyika katika Ukumbi wa Masai camp likiw na lengo la kuwaonesha wateja wao muonekano mpya wa bia hiyo. Na Mpigapicha Wetu

AY kuhamasisha mradi kusaidia watoto wenye mahitaji malum


Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Airtel, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii na Msanii wa Bongofleva, Ambwene Yesaya 'AY', wameanza mchakato wa kutembelea shule zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili na kuwahimiza Watanzania kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA).

Azam yatamba kuendelea kuwa juu


Na Speciroza Joseph

BAADA ya kuifikia Simba kilele mwa Ligi Kuu Bara, Kocha wa Azam FC, Boris Bunjak 'Boca', amesema atahakikisha timu yake inaendelea kukaa katika nafasi za juu hadi kumalizika kwa msimu huu wa ligi.

FIESTA

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Rick Ross akiimba jukwaani  usiku wa kuamkia jana wakati wa Tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club na kuhudhuriwa na maelefu ya mashabiki.Na Mpigapicha Wetu.

Kenyela mgeni rasmi pambano la Mashali


Na Mwandishi Wetu

KAMANDA wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania Ubingwa wa Afrika Mashariki na kati ya  Thomas Mashali wa Tanzania na Medi sebyala wa Uganda litakalopigwa Oktoba 14, mwaka huu Friends Corner Manzese, Dar es Salaam.

Wanamichezo watatu waula CCM



Na Omari Mngindo, Bagamoyo

WANAMICHEZO watatu wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wamefanikiwa
kuchaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wilayani hapa.

Simba hadi raha *Yaichapa JKT Oljoro 4-1 *Yanga kazi ipo leo Kagera


Na Zahoro Mlanzi

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, timu ya Simba, imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya jana kuichapa JKT Oljoro ya Arusha, mabao 4-1 katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

MAWAIDHA


Mhubiri wa kiislam (ambaye hakutaka kutaji jina) alikutwa akitoa mawaidha ya dini hiyo huku akiwa amesimama kwenye kizuizi cha Barabara ya Morogoro Magomeni Mapipa mwishoni mwa wiki. (Picha na Charles Lucas)

Gama, Marealle, Chilolo waibuka kidedea CCM


Heckton Chuwa, Moshi na
Damiano Mkumbo,Singida

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Leonidas Gama, Mkurugenzi Mtendaji wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle na mwanasheria maarufu Bi.Elizabeth Minde ni baadhi ya wanachama wa CCM, walioibuka washindi katika uchaguzi mkuu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini.

41 Chuo cha St,Joseph warejea nchini


Na Heri Shaaban

WANAFUNZI 41 wa Uhandisi Chuo cha St,Joseph wamerejea nchini jana wakitokea nchini India katika ziara ya mwaka mmoja ya kimasomo.

Tanzania, Kenya kufanya mkutano wa pamoja Taveta


Na Darlin Said

WIZARA ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki itafanya nkutano wa pamoja baina ya Tanzania na Kenya utakaokuwa unatoa elimu na uhamasishaji wa masuala ya Jumiya ya Afrika Mashariki na ukaguzi wa kituo cha pamoja cha utoaji huduma mpakani Taveta

Mawakala 800 ubungo kupatiwa mafunzo


Na Heri Shaaban

MAWAKALA  800 wa kuhudumia abiria katika kituo Kikuu cha mabasi yaendayo Mikoani Ubungo wanatarajia kupatiwa mafunzo ya kazi zao na Chuo Cha Usafirishaji(NIT).

Vita shuleni *Wanafunzi wamjeruhi vibaya mwalimu wao *Polisi wapiga mabomu ya machozi shuleni


Na Masau Bwire

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makumbusho, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana walimshambulia na kumjeruhi vibaya mwalimu wao aliyefahamika kwa jina moja la Bw. Epimack, ambaye aliumia usoni.

Mazishi ya Rugambwa Bukoba kwafurika, wageni wakosa pa kulala



Theonestina Juma na Livinus Feruzi, Bukoba

WAKATI masalia ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza Afrika, Laurean Rugambwa, yakitarajiwa kuzikwa rasmi leo katika Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Huruma mjini Bukoba, mkoani Kagera, idadi kubwa ya wageni waliofika kushuhudia tukio hilo la kihistoria wamekosa hifadhi katika nyumba za kulala wageni.

Wana CCM walalamikia rushwa katika uchaguzi


Na Daud Magesa, Mwanza

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiendelea na uchaguzi wa viongozi wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, vitendo vya rushwa vimezidi kushika kasi mkoani Mwanza.

Walimu 'waisuta' CWT



Zourha Malisa na Kassim Mahege

BAADHI ya walimu jijini Dar es salaam, wamedai kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na Chama cha Walimu nchini (CWT), kuwa hawatafanya maadhimisho ya siku ya walimu duniani kote kwa sababu Serikali imeshindwa kuwatimizia madai yao.

Yanga yadai mapato 'yamechakachuliwa'

Na Zahoro Mlanzi

SIKU moja baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutangaza mapato ya mechi ya watani ya jadi, Simba na Yanga, uongozi wa Yanga, umekuja juu kwa kusema kuna mchezo mchafu umefanyika kutokana na idadi ya watu walioingia kuwa tofauti na  mapato yaliyopatikana.

Serengeti Boys 'yanusa' michuano Afrika


Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), imefuzu kucheza raundi ya tatu na ya mwisho kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.

Diwani aingia mitaani acharaza viboko wanafunzi wazururaji


Na Severin Blasio,
Morogoro

DIWANI wa Kata ya Kichangani katika manispaa ya Morogoro, Bw. John Waziri ameamua kuingia mitaani kutoa mfano wa kufundisha maadili kwa kuwacharaza viboko wanafunziwa shule ya msingi Kichangani waliokuwa wakionekana wakizurura mitaani wakati wa masomo.

Serikali yaanza kutekeleza ahadi za Rais Kikwete



 Na Gladness Mboma

SERIKALI imeanza kutekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kumaliza tatizo la maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kutekeleza miradi ikiwemo uchimbaji wa visima vya maji.

Mkapa azindua tawi jipya DCB


Na Darlin Said

RAIS mstaafu Bw. Benjamini Mkapa amezindua Tawi la Benki ya Biashara (DCB)Magomeni na kuwataka Watanzania wanao kwenda kukopa warejeshe mkopo kwa kuwa benki hiyo siyo ya kisiasa.

Waandisi waandaa matembezi ya hisani


Neema Kalaliche na
Jane Hamalosi

Taasisi ya Waandisi imeandaa matembezi ya Hissani kwa ajili ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa lengo la kuwajengea uwezo.

Madenge aanza kazi kwa mbwembwe CCM



Na Anneth Kagenda

MWENYEKITI mpya wa Wilaya ya Kinondoni kupitia (CCM) Bw. Salim Madenge ameanza kazi kwa mbwembwe huku akitoa maagizo lukuki ya utendaji na kumtaka Katibu wa Wilaya hiyo Bw.Edwin Milinga na makatibu wengine kushuka chini na kwenda kuangalia utendaji kazi na uhai wa chama hicho.

Mnyika apinga kauli ya Waziri Mukangara


Na Anneth Kagenda

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo,Bw. John Mnyika ametoa wito kwa vijana kote nchini kutokubaliana na utaratibu uliotangazwa kuhusu maadhimisho ya wiki ya Taifa ya Vijana badala yake wafanye shughuli zao za kuwaingizia kipato.

Niwasomee nini wakati hakuna vyanzo vya mapato-Mwenyekiti


Na David John

SIKU chache baada ya wananchi wa Mtaa wa Kivule Kitunda Wilayani Ilala kumtaka Mwenyekiti wa mtaa huo, Bw.Joseph Gasaya kusoma taarifa ya mapato na matumizi na kudai kuwa tangu ashike nafasi hiyo hajawahi kutoa taarifa yeyote kwa wananchi wake.

Mbunge Mwanjelwa ahamishiwa MOI



Jane Hamalosi na
Neema Kalaliche

MBUNGE wa viti maalum Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi.Mary Mwanjelwa amehamishiwa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) kwa uchunguzi zaidi.

Kinondoni waanza kubomoa nyumba za mabondeni Dar



Na Agnes Mwaijega

MANISPAA ya Kinondoni imeanza kutekeleza mpango wa kubomoa nyumba zote zilizojengwa katika maeneo ya bondeni.

Madereva wa daladala waponda ujio wa Treni


Mariam Said na
Zena Mohamed

MADEREVA wa daladala jijini Dar es Salaam wamesema ujio wa usafiri wa treni hautapunguza foleni bali utaongeza foleni mara dufu.

Waya mpya wa umeme utakaolazwa baharini wawasili Zanzibar


Na Mwandishi Wetu,  
Zanzibar                                                                                            

HATIMAE waya mpya wa umeme utakaolazwa baharini kutoka Ras Fumba Zanzibar hadi Ras Kiromoni Dar-es-Salaam umewasili Zanzibar na kupokewa rasmi pamoja na kukaguliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, katika bandari ya Malindi mjini Unguja.

Kampuni uchimbaji madini kufutiwa leseni



Na Agnes Mwaijega

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Bw.Stephen Masele, amesema Serikali haitakuwa tayari kuendelea kuzivumilia kampuni zinazohusika na uchimbaji wa madini ambazo hazilipi kodi naamesisitiza kuwa zitafutiwa leseni.

Mbunge wa zamani kuibuka kidedea NEC

Na Faida Muyomba, Geita

MBUNGE wa zamani wa jimbo la Nyang'hwale  mkoani Geita,Bw. James Msalika,ameibuka kidedea  katika nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha Mapinduzi (nec)Taifa kupitia wilaya mpya ya Nyangh'wale, baada ya kuwashinda wapinzani wake watatu.

Nashangaa Halmashauri kukataa madai ya walimu Lindi -Oluoch


Na Thureya Dabas

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Bw. Ezekiah Oluoch ameshangazwa na kitendo cha halmashauri ya lindi vijijini kukataa madai ya walimu walioko Lindi.

Aliyegombea udiwani 2010 CHADEMA ahamia ADC


Na, Zubeda Mazunde

ALIYEKUWA mgombea wa udiwani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mwaka 2010 Bi.Sudi Ally Tamu amejiunga na chama kipya cha Alliance for Democratic Change (ADC) na kurudisha kadi ya chama hicho.

05 October 2012

Nundu aibu NEC, vijana hawashikiki *Apata kura 127 kati ya 1,183, mshindi azoa 556 *Wana CCM wahoji hatima ubunge wake 2015


Na Waandishi Wetu

CHAGUZI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimeendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambapo sura mpya zimezidi kutikisa na kuwabwaga makada wa muda mrefu.

VYUNGU


Mtoto Mariam Issa (13), ambaye alipaswa kuwa Shule, alikutwa na kamera yetu eneo la Buguruni, Dar es Salaam jana, akitembeza vyungu maalumu kwa ajili ya mapambo. (Picha na Nyakasagani Masenza)

Mahabusu atoroka na SMG *Alimnyang'anya Polisi mahakamani



Na Queen Lema, Arusha

MAHABUSU mmoja ambaye jina lake halijafahamika mkazi wa Jiji la Arusha, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa askari polisi na kutokomea kusikojulikana.

Lowassa: Nasubiri kauli ya Sumaye



Na Kassim Mahege

MGOGORO unaodaiwa kumuhusisha Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa, umechukuwa sura mpya kwa kile kinachoonekana
kila mmoja kumtupia mpira mwenzake.

SAMAKI


Mkazi wa Kijiji cha Umwe Kati Ikwiriri Wilayani Rufiji, Bi. Hadija Malengwe, akiandaa samaki kabla ya kuwauza kama alivyokutwa na mpigapicha wetu mkoani Pwani Juzi (Picha na Seif Nongwa)

Jina langu linatumika kutapeli- Mulugo


Na Anneth Kagenda

ZIARA za kushtukiza zinazofanywa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, zimeanza kumtokea puani baada ya watu wasiofahamika kutumia jina lake kujipatia fedha kwa njia ya utapeli.

Hali ya Dkt. Mwanjelwa sasa yaendelea vizuri


Jane Hamalosi na Neema Kalaliche

HALI ya Mbunge wa Viti Maalumu, mkoani Mbeya, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Mwanjelwa, inaendelea vizuri baada ya kuanza kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam,

MAELEKEZO


Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akimuamuru dereva wa Daladala namba T 840 BHV, kutoka ndani ya gari hiyo, baada ya kukamatwa akisubiri abiria katika eneo lisilokuwa rasmi kwenye Barabara ya Azikiwe, Dar es Salaam juzi. (Picha na Nyakasagani Masenza)

Rugambwa kuzikwa rasmi kesho



Na Salma Mrisho, Bukoba

MASALIA ya mwili wa aliyekuwa Kardinali wa kwanza Mwafrika Mwadhama Laurian Rugambwa, ambaye awali alizikwa kwenye Kanisa Katoliki la kwanza lililopo Kashozi mwaka 1997, mkoani Kagera, kesho yatazikwa rasmi katika Kanisa Kuu Jimbo Katoliki mjini Bukoba, baada ya ukarabati wake kukamilika.

Mbunge ataka uharibifu chanzo cha maji upatiwe ufumbuzi


Na Sophia Fundi, Karatu

MBUNGE wa Karatu, mkoani Arusha, Mchungaji Israel Natse, ameutaka uongozi wa Wilaya hiyo kulipatia ufumbuzi tatizo la uharibifu wa chanzo cha maji cha Qangded.

MKATABA


Kaimu Mratibu wa Taasisi ya Tanzania na Japan Food Aid, Bw. Lucas Mkandya (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, Bi. Immaculatta Senje, wakibadilishana hati za makubalino ambapo taasisi hiyo itatoa Sh. Milioni 300, kwa ajili ya ujenzi wa mfereji wa Mlenge katika mradi wa umwagiliaji wa mashamba ya mpunga kwenye Bonde la Pawaga. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi. (Picha na Charles Lucas)

Mwakyembe awabeza wanaomkosoa


Na Mariam Mziwanda

WAZIRI wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, amewabeza watu wanaokosoa juhudi anazozichukua ili kuboresha miradi na taasisi za Wizara yake akidai watu hao wataendelea kuimba
ngonjera kutokana na elimu yao duni ya darasa la saba.

Wanaorubuni wanachama CCM sasa waonywa



Na Florah Temba, Moshi

CHAMA Cha mapinduzi (CCM), mkoani Kilimanjaro, kimewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, kuacha kuwarubuni wanachama kwa kuwapa rushwa ili waweze kuchaguliwa kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu.

Kero ya wanafunzi Eckernford Tanga ipatiwe ufumbuzi



VYOMBO vya habari, jana viliripoti maandamano yaliyofanywa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Eckernford iliyopo jijini Tanga.

MGAMBO


Mgambo wa Manispaa ya Ilala, akiwa amemkamata mfanyabiasha ndogondogo kama alivyomkuta eneo ambalo haliruhusiwi nje ya Soko Kuu la Kariakoo Dar es Salaam jana. (Picha na Prona Mumwi)

CWT KUSUSIA MAADHIMISHO SIKU YS WALIMU

Na Darlin Said

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kutoshiriki katika maadhimisho ya siku ya walimu yanayofanyika leo duniani kote, kwa madai kuwa Serikali imeshindwa kutimiza madai yao.

Kupata taarifa ni haki ya msingi



Na Salim Nyomolelo

HAKI ya kujua na kupata habari ni muhimu katika kukuza, kuchochea pamoja na kuleta maendeleo katika Taifa.

Nishati mbadala kunusuru misitu yaonesha mafanikio



Na Rose Itono

TAFITI mbalimbali zimekuwa zinafanywa na wataalamu wengi katika nyanja tofauti za kiuchumi ili kuona ni kwa namna gani mwananchi anaweza kujikomboa na umaskini.

MKAA

Baadhi ya wafanyakazi waliopatiwa mafunzo ya namna ya kutengeneza mkaa kwa kutumia mimea mikavu wakiwa kwenye ajira yao katika kiwanda cha Brikwit (BBC) Bagamoyo.Picha na Rose Itono.

'Mfumo wa elimu uandaliwe upya kuhimili mabadiliko'


Na Daniel Samson

ELIMU ni nyenzo muhimu ya maendeleo inayotolewa katika mfumo rasmi ambao hujumuisha malengo ili kutekeleza sera za nchi
katika kuboresha maisha ya jamii.

WANAFUNZI

Kutembea umbali mrefu ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wa sekondari zisizo na mabweni kwani huchoka na kushindwa kujisomea wafikapo nyumbani hali inayoshusha ufaulu.

Juma Nature kuhamasisha Rocky City Marathon



Na Mwali Ibrahim

MSANII mahiri wa Bongo Flava Juma Kassim Ally a.k.a Sir Nature amejipanga kikamilifu kutoa burudani na kuwapagawisha mashabiki na washiriki wa mbio za mwaka huu za Rock City Marathon zitakazofanyika Oktoba 28, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

JUMA NATURE

Msanii maarufu wa Bongo Flava Juma Kassim Ally a.k.a Sir Nature (katikati) akiimba moja ya nyimbo zake aliyofanya na Baby Madaha (kulia) ijulikanayo ‘Narudi Kijijini’ ambayo itazinduliwa Oktoba 28, mwaka huu wakati wa mbio za Rock City Marathon 2012 zitakazofanyika katika Uwanja wa CCM Kiruma jijini Mwanza, anayeshuhudia (kushoto) ni mratibu wa Rock City Marathon  Grace Sanga. Picha na Amina Athumani.

Wizara bado haijapokea tathmini kutoka TOC



Na Amina Athumani

WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imesema inasubiri ripoti ya tathmnini kwa vyama vya michezo kutoka Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ambayo mpaka jana ilikuwa bado haijawasilishwa.

Kupata taarifa ni haki ya msingi



Na Salim Nyomolelo

HAKI ya kujua na kupata habari ni muhimu katika kukuza, kuchochea pamoja na kuleta maendeleo katika Taifa.

Yondan nje ya uwanja wiki mbili


Na Elizabeth Mayemba

BEKI wa Yanga Kelvin Yondan atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili baada ya kubainika kupasuka mfupa wa mguu wakati wa mechi yao na watani zao Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

RAFU

Kiungo wa Simba Haruna Moshi 'Boban' akimchezea rafu beki wa Yanga Kelvin Yondan (katikati), huku mwamuzi Mathew Akrama (kulia) akishuhudia tukio hilo wakati wa mechi yao iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam na timu hizo kutoka sare ya bao 1-1. Picha na Imma Mbuguni

Simba, Yanga zaingiza mil. 390/-



Na Elizabeth Mayemba

PAMBANO la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lililochezwa juzi wanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.

04 October 2012

MWIZI


Mtuhumiwa aliyekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na fedha bandia, Bi. Asha Abdallah (wa tatu kulia), akiwa chini ya ulinzi wa askari kanzu, kwenye ofisi za wakala wa M-pesa Yombo kwa Lulenge, wilayani Temeke, Dar es Salaam jana, wakati akijaribu kuziweka katika mtandao wa simu yake. (Picha na Baraka Kayagali)

Upelelezi kesi ya Msofe haujakamilika


Na Rehema Mohamed

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Msofe (50), umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

TAKUKURU watoa elimu kupambana na rushwa



Na Heri Shaaban

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Wilaya ya Temeke, imetoa elimu ya kupambana na rushwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Ualimu (DUCE) ili waweze kuepuka vishawishi vya rushwa ya ngono.

Wanafunzi.


Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Ualimu DUCE wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya elimu ya kupambana na masula ya rushwa yaliyokuwa yakitolewa na Taasisi ya Rushwa  Mkoa wa Temeke.(Picha na Heri Shaaban)

ATE yataka waajiri kushiriki kutathmini tuzo mwajiri bora


Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Wajiri Tanzania (ATE), kimewataka waajiri kushiriki kufanya tathmini kuhusu tuzo ya mwajiri bora mwaka 2012 ambapo shindano hilo litadumu kwa miezi miwili na nusu.

Jamii ijifunze lugha ya alama-CHAVITA



Na Mariam Mziwanda

CHAMA cha Viziwi Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, (CHAVITA), kimeiomba jamii ijifunze lugha ya alama kupunguza unyanyasaji kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

Mwanafunzi apigwa radi, afariki dunia



Na Moses Mabula, Tabora

MTOTO Husuna Ramadhani (10), anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Msiliembe, iliyopo Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, amekufa hapo hapo baada ya kupiga na radi ambayo pia iliwajeruhi wanafunzi wengine 23 ambao wamelezwa Hospital ya Mkoa Kitete kwa matibabu zaidi.

TAMKO


Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Tanzania Bw.Deus Kibamba (katikati)akizungumza na waandishi wahabari Dar es Salaam jana,(hawapo pichani) kuhusu mchakato wa kukusanya maoni kwa ajili ya uundaji wa katiba mpya Tanzania katika mikoa mbalimbali ya tanzania kushoto ni Mratibu jukwaa hilo Bi.Diana Kidala na kulia ni Mjumbe Bw.Israel Ilunde. (Picha na Prona Mumwi)

Mpasuko Jimbo la Mwibara umalizwe


Na Raphael Okello.

KATIBU  mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) ni mzaliwa wa kata ya Iramba, jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara.

'Wenyeviti wa mitaa wapewe elimu ya PETS'



Na Stella Aron

TAASISI ya Kupambana na Kupunguza Umaskini (MPR) imeshauri Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na kamati mbalimbali za maendeleo, kupatiwa elimu ya Matumizi ya Fedha za Umma (PETS), ili kusaidia upatikanaji wa maendeleo ya haraka.

CKHT chatakiwa kushirikiana na serikali


Na Mariam Mziwanda

CHUO Kikuu Huria nchini (CKHT), kimetakiwa kushirikiana na Serikali ili wataalamu wake wa utafiti katika sekta ya kilimo na uchumi waweze kuchochea maendeleo ya nchi.

UFAFANUZI


Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Mathew Mnali (aliyesimama), akifafanua jambo kwa wawekezaji wazalendo wa sekta ya ufugaji, waliokutana Dar es Salaam jana. Mkutano huo uliandaliwa na kituo hicho kwa kushirikiana na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). (Picha na Nyakasagani Masenza)

Dkt. Mgimwa: Uchumi wetu unaendelea kukua



Leah Daud na Kassim Mahege

UCHUMI wa Tanzania unaendelea kuimarika licha ya kuwepo changamoto mbalimbali pamoja na mfumuko wa bei.

Goba wazidi kulalamikia kero ya maji



Na Rose Itono

WAKAZI wa Goba, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, wamesema mradi wa maji uliokuwa ukisimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika, umekufa na kusababisha wananchi wakose huduma ya maji safi na salama.

03 October 2012

AJALI MBAYA MBALIZI Mbunge CCM anusurika kufa *Ni Dkt. Mary Mwanjelwa, Katibu wake ateketea moto *Watu zaidi ya nane wahofiwa kufa, imehusisha magari 4 *Basi la Dar Express nalo laungua moto, 48 wanusurika


Charles Mwakipesile na Esther Macha, Mbeya

MBUNGE wa Viti Maalumu, mkoani Mbeya, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Mwanjelwa, amenusurika kufa katika ajali mbaya iliyotokea jana eneo la Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini baada ya gari lake kugongwa na kuteketea kwa moto.

AJALI

Baadhi ya wakazi wa eneo la Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini, wakiangalia mabaki ya gari la Mbunge wa Viti Maalumu, mkoani Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa, ambaye alinusurika kufa kama linavyoonekana baada ya kupata ajali mbaya jana. Katika ajali hiyo, Katibu wa mbunge huyo Bi. Amina Mwampashi anahofiwa kufa papo hapo. (Charles Mwakipesile)

Petroli, dizeli zashuka bei *EWURA: Wanunuzi ombeni stakabadhi


Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), jana imetoa bei kikomo za mafuta ya petroli na dizeli ambazo zitaanza kutumika kuanzia leo nchini kote.

CCM yazidi kumuandama Dkt. Slaa



Na Mwanajuma Juma, Zanzibar

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, kuacha kukipigia ramli chama chao.

MAADHIMISHO

kikundi cha ngoma cha watoto yatima cha friends ofDonBosco wakitumbiiza katika maadhimisho ya miaka hamsini ya kiwanda cha Mansoor Daya Dar es Salaam Jana(Picha na Anna Titus)

Kigoda achanua NEC, mchuano bado waendelea


Na Waandishi Wetu

MCHUANO mkali bado umeendelea katika chaguzi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo baadhi ya wagombea waliopewa nafasi ya kushinda, wameangukia pua.

Rufaa ya Lema yasogezwa tena


Na Pamela Mollel, Arusha

HATIMAYE rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), jana imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, baada kuibuka hoja zaidi ya nne.

JK: Tuvute subira mgogoro Ziwa Nyasa


Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuwa na subira kuhusu tatizo la mpaka wa Ziwa Nyasa.

Alisema katika kushughulikia utata wa mpaka huo na nchi ya Malawi, Tume maalumu ilikuwa ikutane Septemba 10 hadi 15 mwaka huu lakini mkutano huo haukufanyika.

ZAWADI


Bw.Husein mussa ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa Mansoor daya, akimkabidhi Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda  zawadi ya picha ya Rais kikwete katika sherehe ya kutimiza miaka hamsini ya kiwanda cha kutengenezea dawa cha Mansoor Daya Dar es Salaam Jana wakwanza kushoto ni Mrs Mansoor Daya na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Bw.Said Mecky Sadik(picha na Anna Titus)

Madiwani Bunda watupiwa lawama nzito


Na Raphael Okello, Bunda

SHIRIKA za Kuwasaidia Wazee nchini (SAWATA), mkoani Mara, limesema madiwani mkoani humo wameshindwa kushiriki maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani kwa sababu hawakutenga posho za kuwapa baada ya maadhimisho.

Kesi ya utapeli wa mil. 102/- yakwama



Na Rehema Mohamed

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya utapeli na kujipatia zaidi ya sh. milioni 102 kwa njia ya udanganyifu, umedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Wanafunzi watakiwa kuepuka vishawishi



Na Omary Mngindo, Bagamoyo

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete, amewataka wanafunzi wa kike waliopo katika shule za msingi na sekondari, kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha wakatishe masomo yao.

OPERESHENI


Fundi wa Mifumo ya Umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Bw. Steven Mganga, akikata umeme kwenye maungio, baada mkazi wa Mbezi Beach, Bw. Emmanuel Mbuga kukutwa akitumia huduma hiyo bila idhini ya shirika hiyo, Dar es Salaam jana. Shirika linafanya operesheni isiyo na ukomo nchini kote kuwakamata wezi wa umeme ili kuliwezesha kujiendesha kwa ufanisi.

Sera za elimu zisiishie katika makabati



Na Agnes Mwaijega

ELIMU ni sekta muhimu yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa lolote duniani.

Ili sekta hii iweze kukua inategemea sera zilizowekwa kwa ajili ya kusimamia suala hilo na kuhakikisha inakuwa na mafanikio.

Tatizo la mimba kwa wanafunzi kikwazo maendeleo ya elimu



TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.

02 October 2012

Tuongeze mapambano kuzuia matumizi ya dawa za kulevya



DAWA za kulevya ni kemikali ambazo huathiri ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu ambao  unajumuisha ubongo, uti wa mgongo na kuleta mabadiliko ya hisia, fikra na tabia.

USALAMA


Mrakibu Msaidizi wa Polisi Makao Makuu Dar es Salaam, Bw. Emmanuel Mkilia (kulia), akishikana mikono na Ofisa Upelelezi wa Tume ya Kuzuia Rushwa nchini Swaziland, Bw. Cyprian Cininza, baada ya kuvishwa vazi la asili la nchi hiyo, mara baada ya kutoa mafunzo ya wiki tatu ya upelelezi wa makosa ya jinai yanayohusu mitandao, Jijini Mbabane hivi karibuni. (Picha na Juma Kintu wa NSSF)

Uchaguzi CCM Ngwilizi chali, rushwa nje nje *Mgombea azirai, mtoto wa Wassira 'apeta' *Shitambala apita NEC, Mshangama aula



Na Waandishi Wetu

KINYANG'ANYILO cha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini.

TIPF wamtaka Slaa aache kumuandama Lowassa


Na Anneth Kagenda

MKURUGENZI wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation (TIPF), Bw. Sadiki Godigodi, amemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa, kuacha kumuandama Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa na Mbunge wa Bariandi Magharibi Bw. Andrew Chenge.

MAHOJIANO


Mkazi wa Mtaa wa Business Mikocheni B, (kushoto) akificha uso wakati akihojiwa na Ofisa Usalama wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kinondoni, Bi. Dunia Shami, Dar es Salaam jana baada ya kujiunganishia huduma ya umeme kwenye nyumba yake bila kibali. Kulia ni Fundi Umeme wa shirika hilo Bi. Grace Ndyetabura. (Picha na Charles Lucas) 

Uchaguzi CCM usiwe kufa na kopona-Pinda



Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao wanagombea nafasi mbalimbali za uongozindani ya chama hicho, wasiligeuze suala la uchaguzi kuwa ni la kufa na kupona.

Siku ya wazee iadhimishwe kwa kusherehekea mafanikio si matatizo



Na Rabia Bakari

KILA ifikapo Oktoba mosi ya kila mwaka, wazee wa Tanzania wanaungana na wazee wengine duniani kuadhimisha siku yao.

SIKU YA WAZEE

Wazee wakishiriki kuvuta kamba katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

Rais ateua Kamishna Jenerali Magereza



Na Mwandishi Wetu

RAIS na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya  Kikwete, amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na Makamishna wa idara mbaolimbali.

Waliojenga maeneo yasiyo rasmi nyumba zao kuvunjwa



Na Salim Nyomolelo

SERIKALI imesema nyumba zote zilizojengwa maeneo ambayo si rasmi zitavunjwa bila ya kuangalia thamani yake kama watabiani zimejengwa bila kwa kukiuka sheria na taratibu.

MAELEKEZO YA SHERIA NDOGO ZILIZOTUNGWA MWAKA 2011

wanasheria wa Manispaa ya Ilala Bi. Pamela Mugaruka akielezea matumizi ya sheria akielezea matumizi ya sheria ndogo zilizotungwa mwaka 2011 kwa watu wanaozikiuka, wa kwanza kushoto ni ofisa usafirishaji Bw. Samweli Bubegwa na wa tatu kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo Bw. Raymond Mushi. (Picha na maktaba)


Sheria ya usafi wa mazingira itekelezwe kivitendo


Na Stella Aron

"USAFI wa mazingira ni jukumu letu sote, ni suala muhimu kwa afya na uhai wetu,"

Kauli hiyo imekuwa ikitolewa mara kwa mara na viongozi mbalimbali nchini kwa nia ya kuhakikisha kuwa jamii inafuata kanuni za usafi wa mazingira nchini.

Hamasa za kilimo ziende sanjari na upatikanaji pembejeo bora



Na Rashid Mkwinda

MVUA za Kwanza ni za kupandia," ilikuwa ni kauli mashuhuri enzi za Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, akihamasisha kilimo ambacho kwa wakati huo kilikuwa na kauli Mbiu ya ‘’Kilimo ni Uti wa Mgongo".

CHAMAZI


Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kiislamu ya Chamazi, iliyopo Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, wakimsikiliza mgeni rasmi, Sheikh Othman Ally Kapolo, wakati wa mahafali ya 4 ya shule hiyo yaliyofanyika juzi. (Picha na Said Njuki)

Manispaa Ilala yaongeza ukusanyaji mapato 2012



Mwali Ibrahim na Amina Athumani

MANISPAA ya Ilala, Dar es Salaam, imefanikiwa kuongeza mapato yake kutoka asilimia 88 mwaka 2010/11, hadi 99 mwaka huu.

Michuano ya Kifimbo kuzinduliwa leo



Na Daud Magesa, Mwanza

MASHINDANO ya kusaka vipaji na kuviendeleza kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, jijini hapa yanatarajia kuzinduliwa leo kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Wabuni 60 kushiriki Swahili Fashion



Na Amina Athumani

ZAIDI ya wabunifu 60 wamejiandikisha kushiriki maonesho ya mavazi ya nguo za kiswahili 'Swahili Fashion Week', yaliopangwa kufanyika Desemba 6 hadi 8, mwaka huu Dar es Salaam.

HUDUMA


Wafanyakazi wa Airtel wakitoa huduma ya internet kwa wateja waliotembelea duka lao lililopo Kinondoni Morocco, Dar es salaam  jana, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja yenye lengo la kuwashukuru kwa kutumia huduma na mtandao huo. (Na Mpigapicha Wetu)

Nyilawila: Cheka alinichezea rafu



Na Amina Athumani

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Karama Nyilawila amesema kushinda kwa Francis Cheka, katika pambano lao si kwamba aliishiwa punzi bali ni kutokana na rafu nyingi alizofanyiwa na mpinzani wake.

RT yaridhishwa maandalizi Rock City


Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha Riadha Tanzania (RT), kimeridhishwa na maandalizi ya mwaka huu ya mbio za Rock City Marathon, zitakazofanyika Oktoba 28 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kayumba mabingwa wapya wa pool


Na Mwandishi wetu, Mwanza

TIMU ya pool ya Kayumba kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala jijini Dar es salaam, juzi ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa taifa wa  mashindano ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012', baada ya kuikung'uta Meeda ya Kinondoni magoli 13-2 katika mchezo wa fainali.

UBIGWA

Mkurugenzi wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Michezo na Vijana, Leonard Thadeo (wa pili kushoto) akimkabidhi kombe nahodha wa Klabu ya Kayumba ya Mkoa wa kimichezo wa Ilala, Emmanuel Martin mara baada ya kutwaa ubingwa wa Taifa wa mashindano Safari Pool 2012. Na Mpigapicha Wetu

Sekta binafsi zatakiwa kuwekeza katika jamii



Na Darlin Said

SERIKALI imezitaka sekta binafsi kuwekeza zaidi katika masuala ya kijamii ili iweze kufikia malengo mbalimbali.

Vyombo vya majini vithaminiwe-Abbas



Na Anneth Kagenda

WITO umetolewa kwa Watanzania kuvitunza na kuvithamini vyombo vya usafiri majini ili ubora wake uendelee kuwepo sambamba na kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.

Tushirikiane kuwapunguza watoto mitaani



Na Jane Hamalosi

SIKU zinavyozidi kwenda tatizo la watoto wa mitaani linaota mizizi na huku juhudi za kulimaliza zikishindikana.

01 October 2012

VICOBA


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), Bw. Ramadhani Madabida, akizungumza na wanawake wa Benki ya Kuweka na Kukopa (VICOBA), Kata ya Buguruni, Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa UWT Wilaya Ilala, Bi. Nora Mzeru na Diwani wa Viti Maalum (CCM), Bi. Batuli Mziya. (Picha na Heri Shaaban)

Wassira sasa amlipua Slaa *Amtaka aache kuita wake za watu chumbani *Dovutwa: CHADEMA inamuogopa Lowassa



Na Mwandishi Wetu, Bunda na Dar

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema watoto wa kaka yake ambao juzi walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi. Lilian na Bi. Esther Wassira, wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Uchaguzi CCM balaa *Nagu afanya kweli, Mfutakamba chali



Na Waandishi Wetu

HATIMAYE kinyang'anyilo cha kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Wilaya ya Hanang’, mkoani Manyara, kimemalizika juzi baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu, kuibuka mshindi.

MAFUNZO


Meneja Masoko wa Benki ya Afrika Tanzania, Bw. Solomon Haule (aliyesimama kushoto), akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Sekondari ya Baobab, waliofika Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam juzi kwa ziara ya mafunzo. (Picha na Nyakasagani Masenza)

Mbaroni kwa kubaka mtoto wake wa miaka 4



Na Faida Muyomba, Geita   

JESHI la Polisi mkoani Geita, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Nyambaya, Kata ya Katoma, wilayani Geita, Bw. Masanja Ilanga (45), kwa tuhuma za kumbaka mwanaye mwenye miaka minne.

Serikali yaombwa kuboresha bajeti ya elimu nchini



Na Daud Magesa, Mwanza

SERIKALI imeombwa kuboresha bajeti ya elimu ili kukabiliana
na changamoto za ukosefu wa vitabu, mabaara, vifaa vyake, miundombinu ya majengo na nyumba za walimu katika shule mbalimbali nchini.

MSAADA


Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizungumza na mkazi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, Bi. Moshi Maleja (kulia) baada ya kukabidhi msaada wa kitanda kwa ajili ya wajawazito na tangi la maji la ujazo wa lita 5000, vilivyotolewa na Mawaziri, Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii na Bw. Bernald Membe wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Katikati ni Diwani wa Kata hiyo, Alhaj Omary Kaliati. (Picha na Charles Lucas)

Mwinyi: Viongozi tekelezeni wajibu wenu kwa jamii



Na Charles Lucas

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka viongozi kutekeleza wajibu wao kikamilifu ili jamii iweze kutambua mchango wao hasa vijana ambao wengi wao hawana ajira hivyo kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

UN yaipongeza Tanzania kwa kupeleka askari polisi Darfur


Na Mwandishi Maalumu

TANZANIA imepongezwa kwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoitikia vyema wito wa kupeleka idadi kubwa ya askari polisi wanawake kushiriki Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa (UN), katika Jimbo la Darfur nchini Sudan.

SHIMO


Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda (wa tatu kushoto), ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, akiangalia shimo lililoko kwenye makutano ya barabara za Bugwe na Soko Kuu mjini Mpanda jana, alipofungua mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa  CCM wilaya za Mlele na Mpanda mkoani Katavi. (Picha Waziri Mkuu)

Padri Mapunda akemea uongozi wa kupeana


Na Goodluck Hongo

PADRI wa Kanisa Katoliki nchini Baptiste Mapunda, amekemea tabia ya kupeana uongozi ndani ya familia akidai hali hiyo itakwamisha utendaji kazi wenye tija ili kuchochea maendeleo.

CCM ikimee visasi baada ya kumaliza chaguzi zake


HIVI sasa, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kipo katika mchakato wa kufanikisha changuzi mbalimbali ndani ya chama hicho baada ya Kamati Kuu (CC), kupitisha majina ya wagombea mjini Dodoma.

BOMU


Baadhi ya Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Juhudi, iliyoko Gongolamboto, Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, wakiangalia mfano wa bomu lililotengenezwa wanafunzi wa fani ya sayansi wa shule hiyo juzi, ikiwa ni sehemu ya masomo yao. (Picha na Charles Lucas)

Uoto wa asili kurejea tena Ukerewe



Na.Jovither Kaijage,
Ukerewe   

ENEO la misitu ya halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza lenye ukubwa wa Hekta 1,160.9  uenda  likarejea katika uoto wa asili kama ombi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) la kuindeleza litalidhiwa.

Wanafunzi 80 waliofanya vizuri wazawadiwa Ilala


Na Heri Shaaban

WANAFUNZI 80 wa shule za sekondari Mkoa wa Ilala wamezawadiwa kwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha tatu na tano.

Tuzo hizo zilitolewa Dar es Salaama jana, na Wakuu wa Shule Tanzania (TAHOSSA)katika afla iliyofanyika sekondari ya Tambaza.

Akitoa taarifa ya uendeshaji wa mitihani Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani Ilala, Bw.Hussein Zuberi alisema kuwa umoja huo lengo lake kuunga jitihada za serikali katika kukuza taaluma katika shule zote za serikali hapa nchini.

Bw.Zuberi alisema kuwa mitihani hiyo huendeshwa katika ngazi ya Kanda na mikoa ,kama ilivyo katika mkoa huo wa Ilala na hiyo ni mara ya kwanza kwa kamati hiyo kuendesha mitihani kwenye ngazi ya mkoa.

"Kamati ya mitihani Mkoa Ilala TAHOSSA huendesha mitihani uendesha mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo kwa kidato cha tatu na kidato cha tano kila mwaka na washindi upewa zawadi,kidato cha tatu wanafunzi 41, kidato cha tano wanafunzi 39,"alisema Bw.Zuberi.

Madhumuni ya mitihani hiyo kuwajengea wanafunzi hali ya ushindani,kuwasaidia walimu kupata uzoefu katika utungaji,kuhariri, kusahihisha mitihani,kusaidia walimu kujua uwezo wa wanafunzi wao.

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Bw.Nyambari Chacha alisema kuwa wamebaini kitu kizuri kwa wanafunzi wa shule hizo ili waweze kujihamini huko mbele,na kuwataka wazazi kushirikiana na kamati za shule katika kufatilia maendeleo ya watoto wao.

Bw.Chacha aliwapongeza mpango huo na kusema kuwa mtaala wa elimu uwe unabadilika kila wakati kutokana na mabadiriko tuliyonayo,pia kabla kubadirisha kwa mtala huo tuwandae walimuwatakaofundisha.

Aliutaka umoja huo wa TAHOSSA kusimamia vizuri shule za kata hili ziweze kutoa wanafunzi bora watakaojenga Tanzania ya baadae.


Vyombo vya habari vyatakiwa kutumia lugha ya alama



Na Agnes Mwaijega

VYOMBO vya habari nchini vimesahuriwa kujitahidi kuanza kutumia lugha ya alama ili viziwi nao waweze kupata taarifa mbalimbalina kutoa maoni.

Wazai washauriwa kuacha ubaguzi

Na Agnes Mwaijega

WAZAZI wametakiwa kuacha ubaguzi,kuzingatia suala la usawa na kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto wa kike ili waweze kuwa na mafanikio na kupambana na chamgamoto mbalimbali za kimaisha.

WANAFUNZI


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilala wakizoa takataka bila kuvaa vifaa maalumu kuwakinga na magonjwa, kama walivyokutwa na mpigapicha wetu eneo la shule hiyo, Dar es Salaam juzi. (Picha na Anna Titus)

Wateja Vodacom kubonga bila mipaka



Na Mwandishi Wetu

WATEJA wa Kampuni ya Vodacom wameendelea kunufaika na gharama nafuu katika kupiga simu bila ya kuwa na hofu ya gharama za muingiliano wa kupiga simu kwenda mitandao mengine.

Serikali yaombwa kuboresha bajeti ya elimu Mwanza




Na Daud Magesa,
Mwanza


SERIKALI imetakiwa kuboresha bajeti ya elimu ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa vitabu,mabaara na vifaa vyake na miundombinu ya majengo na nyumba za kuishi walimu katika shule mbalimbali nchini.

Ludewa watakiwa kujiandaa kupokea wawekezaji mgodini

Na Nickson Mahundi,
Ludewa

WANANCHI wilayani Ludewa wametakiwa kujiandaa na ujio wa wageni zaidi ya 600,00 ambao watakuja katika machimbo ya migodi mikubwa ya Mchuchuma na Liganga iliyoko wilayani humo.

MAPUMZIKO


Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam (jina halikufahamika) anayejishughulisha na uokotaji wa chupa za plastiki akijipumzisha kwa kulalia mfuko wenye chupa hizo baada ya kuchoshwa na mizunguko, kama alivyokutwa kando ya Barabara ya Nyerere Gerezani, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)

Watakiwa kuuza pikipiki zikiwa na kofia mbili


Na Stella Aron

WAFANYABIASHARA wa pikipiki wametakiwa kuuza pikipiki zikiwa na kofia mbili ngumu ili kuwasaidia kupunguza majeraha kwa abiria pindi wanapopata ajali.

Wasomi watakiwa kujenga uzalendo nchini mwao



Na Daud Magesa,
Mwanza

WASOMI nchini wametakiwa kuwa waadilifu na kujenga uzalendo ili kulikwamua taifa na kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali husani elimu.

'Wananchi acheni kuhujumu TANESCO'


Na Mariam Mziwanda

SHIRIKA lKA la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Temeke limewataka wananchi kuacha kulihujumu shirika hilo kwa kukomesha wizi wa umeme ili shirika liweze kujiendesha na kufanikisha utoaji wa huduma bora nchini.

MZIGO


Mwendesha baiskeri ya gurudumu tatu (GUTA), akiwa katika wakati mgumu kutokana na kuelemewa na uzito wa mizigo, kama alivyokutwa Magomeni Usalama, katika Barabara ya Morogoro Dar es Salaam jana. Baiskeli hizo zimekuwa kimbilio mbadala kutokana unafuu wa ghalama inayotozwa ya usafirishaji jijini. (Picha na Charles Lucas)

Tanzania kuiburuta Malawi mahakamani





Na Mwandishi Maalum,Newyork ,Marekani            

SERIKALI imeuambia Umoja wa Mataifa (UN) kuwa itawasilisha madai yake katika Mahakama ya Kimataifa yenye dhamana ya utatuzi wa mgogoro ili iutafutie ufumbuzi mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika ziwa nyasa.

Bundi wazua tafrani mkutano wa CCM Kahama *Watua meza ya Limbeli, Mgeja, wagoma kutoka ukumbini *Diwani asema matukio ya ushirikina lazima yakemewe


Na Patrick Mabula, Kahama

KATIKA hali ya isiyo ya kawaida Bundi wawili wameingia kwenye ukumbi wa mikutano kisha kutua meza kuu wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kahama uliofanyika Shule ya Msingi Rocken Hill.

Naunga mkono Zitto kuwani urais-Kibwangala




Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MBUNGE wa Jimbo la Nzega mkoani Tabora, Dkt. Hamis Kigwangala, ametangaza kuunga mkono dhamira ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe,  ya kutangaza kuwania urais mwaka 2015.

Halima Mdee amvaa mchungaji Rwakatare *Ni katika sakata la hekalu lake linalotakiwa kuvunjwa, *Asema viongozi wa aina hiyo aibu kwa taifa *Adai itatafsiriwa Serikali imewekwa mfukoni


Goodluck Hongo

MBUNGE wa Kawe na Waziri Kivuli wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Halima Mdee, ameshangazwa na hatua ya Serikali kukaa kimya, bila ya kuchukua hatua za kubomoa nyumba ya Mchungaji Getrude Rwakatare, iliyopo Mbezi, jijini Dar es Salaam, inayoelezwa kujengwa kwenye viwanja ambavyo ni kinyume cha sheria.

Jumba la Mchungaji Rwakatare

Jumba la Mchungaji Rwakatare ambalo Bi Halima Mdee anashinikiza libomolewe,picha ndongo ni kitanda anachodaiwa kukitumia.

Migiro kukomesha unyanyapaa, ubaguzi kwa waathirika



Na Mwandishi Wetu

MJUMBE Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi barani Afrika Dkt.Asha-Rose Migiro ameanza majukumu kwa kuitembelea Tume ya Taifa ya UKIMWI (TACAIDS) na kuwataka wadau katika vita kutilia mkazo katika masuala yanayochangia maambukizi mapya kwa kiwango kikubwa.

Ahmadiyya wakutanisha waumini kufahamina


Na Darlin Said

JUMUIYA ya Waislam wa Ahmadiyya umefanya Mkutano wa 43 ambao unafanyika kila mwaka duniani,lengo ikiwa ni kuwakutanisha waumini pamoja ili waweze kufahamina na kujifunza mambo ya kiroho.

Neno Negative lamfanya ajiue akidhani ana VVU



Na Zubeda Mazunde.

KATIKA kile kinachoonesha watu wengi hawapo tayari kupokea matokeo ya vipimo vya Virusi vya UKIMWI (VVU), mkazi wa Tegeta, jijini Dar es Salaam, Bw. Juma Hussen (18) amejiua baada ya kupima VVU na vipimo vyake kuonesha yupo Negative.

TEC: Urasimu bandari za Tanzania umewakimbiza wafanyabiashara


Na Mwandishi Wetu

SABABU kubwa inayochangia wafanyabiashara kuacha kuitumia bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ili kuingiza mizigo yao ni urasimu unaodaiwa kufanywa na maofisa forodha wanaohusika na ushuru wa kodi ya mapato kwa wafanyabishara wanaopaswa kulipia kodi hiyo Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).