08 October 2012
Urais CHADEMA vita kubwa *Katibu BAVICHA naye atangaza dhamira yake
Na Benedict Kaguo,Tanga
VITA ya kuwania urais mwaka 2015, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imezidi kushika kasi baada ya Katibu wa Baraza la Vijana (BAVICHA), mkoani Tanga, Bw. Deogratius Kisandu, kutangaza rasmi dhamira ya kuwania nafasi hiyo.
Uamuzi wa Bw. Kisandu kutaka kuwania nafasi hiyo, unaweza kuongeza mpasuko ndani ya CHADEMA, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kutangaza kuwania nafasi hiyo hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga jana, Bw. Kisandu alisema Watanzania wanahitaji mabadiliko ambayo hayawezi kupatikana kama vijana makini hawatapewa nafasi.
“Nimefanya tathmini ya muda mrefu kabla sijatangaza uamuzi huu na kuiani kuwa, hakuna kiongozi mwenye dhamira na uwezo wa kuliongoza Taifa hili hasa wale wanaotoka katika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini na bungeni.
“Mimi nimejitoa ili kuongoza mabadiliko haya na ninaweza kuwa Rais wa Tanzania, Watanzania wanahitaji kujua Kisandu ni nani, anafanya nini na malengo yake ni yapi kwa mustakabali wa nchi hii,” alisema Bw. Kisandu.
Alisema kwa muda mrefu wagombea urais wamekuwa wakitokea kwenye ubunge na Uwaziri lakini hicho si kigezo cha kupata viongozi hodari kwani wameonesha udhaifu mkubwa licha ya kupewa nafasi hizo.
“Ni wakati wa kuiga mfano ya Mwalimu Nyerere ambaye hakuwahi kuwa mbunge lakini aliweza kuongoza vyema Taifa letu, alipewa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi akiwa hajawahi kushika madaraka makubwa serikalini lakini aliweza kuwaunganisha Watanzania na kupata uhuru wa kisiasa,” alisema.
Bw. Kisandu aliongeza kuwa, umefika wakati wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ambapo kazi hiyo lazima iongozwe na Mtanzania mmoja na yeye yupo tayari kwani hajawahi kuwa mbunge wala Waziri zaidi ya uongozi ndani ya CHADEMA.
Alisema uwezo wa Mwalimu Nyerere kuongoza bila kupitia kada hizo ndicho kinachomfanya akumbukwe kwa ongozi wake ambao umetukuka hivyo wanasiasa wanaotokana na ubunge au Uwaziri hawastahili kupewa urais wa nchi.
“Nilidhani marais ambao wameliongoza Taifa letu wakiwa na uzoefu wa ubunge, Uwaziri kabla ya kupata Urais wangeweza kuiongoza nchi kwa ufanisi zaidi kushinda Mwalimu Nyerere.
“Badala yake wameonesha udhaifu mkubwa ambao unatupa tafsiri kwamba Taifa hili halihitaji kiongozi mwenye uzoefu mkubwa bali aliye na maono, uadilifu na hofu ya Mungu,” alisema Bw. Kisandu.
Alisema amejiandaa kisaikolojia kuwania nafasi hiyo na kuomba Watanzania wamuunge mkono ili kufanikisha dhamira ya kuleta ukombozi wa pili nchini baada ya ule aliofanya Mwalimu Nyerere kuwaondoa wakoloni na kupatikana uhuru.
Aliongeza kuwa, mwanasiasa yeyote mwenye kipaji na maono hawazi jana na leo bali anawaza jana, leo, kesho na kesho kutwa hivyo jambo la msingi ni kutazama ni jinsi gani tunaweza kupata ukombozi wa pili wa Taifa letu,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
CHADEMA ACHENI KIGUGUMIZI FANYENI UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UKIWA WA UWAZI ILI KUANDAA SAFU ITAKAYOCHAGUA MGOMBEA URAIS HATUTAKI MIZENGWE ONYESHENI MUNAVYOPAMBANA NA RUSHWA NA UFISADI ILI KUWAZODOA CCM
ReplyDeleteupinzani siku zote hamjuhi kujipanga mnaharibu deal wenyewe,
ReplyDeleteuingereza ,marekani na nchi zote kubwa nduniani wana vya vingi,lakini wenzenu wanaheshimiana kwenye uchanguzi mkuu .....nchini marekani utaona ni demokaratiki au repabulikani ndio vinasimamisha watu wawili,nyie mnasimamisha kila chama mgombea uraisi(hilo ndio kosa kubwa)
mfano mzuri,pro lipumba ameshindwa uraisi mara zaidi ya mbili,mrema mara zaidi ya mbili,mwitikila na wengine wote walioshindwa zaidi ya mara mbili-----nilazima binadamu mwenye akili timamu,mpenda maendeleo ya ukweli na msomi kutafuta muunganiko wa mtu mmoja mwenye nguvu kusimama kupitia upinza,akishinda wakina (lipumba,mrema,mbowe,mbatia,mwitikila, na wengine ) atawateua kwenye nyazifa ,hata hasipo wateua kama amuaminianai ni bora mgombee ubunge ---lipumba utashinda ubunge,mrema utashinda ,mbowe utashinda,mwikila utashinda ili mwende bungeni mkaongeze nguvu ya kiuchumi nchini,hacheni kuwa "wajinga,walafi,malimbukeni wakungombea uraisi wakati mlishindwa mara 3 na zaidi"
kuunganika kwa upinzani ni ...mrema,mwitikila,mbowe,dk silaha,pro lipumba kutogombea uraisi bali kungombea ubunge na "mtu mmoja mwenyenguvu kugombea uraisi''''mfano zitto,,,,na wengine wenye nguvu ya kisiasa zaidi ya 50% wapewe kipaombele'
kwani chadema ni chama cha siasa au wanaharakati? hata hivyo bado sio wanaharakati maana huku tunakoishi vijana wavuta bangi na wacheza kamari ndio wanachama wenu. mie bora niende chama kingine kuliko huko.
ReplyDelete