01 October 2012
'Wananchi acheni kuhujumu TANESCO'
Na Mariam Mziwanda
SHIRIKA lKA la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Temeke limewataka wananchi kuacha kulihujumu shirika hilo kwa kukomesha wizi wa umeme ili shirika liweze kujiendesha na kufanikisha utoaji wa huduma bora nchini.
Hayo yalisemwa Dar es salaam jana na Fundi Mwandamizi Kitengo cha Udhibiti Mapato TANESCO Makao Makuu Bw.Didas Luwinga katika oparesheni ya kamata wezi wa umeme (KWEU) inayoendelea wilayani humo.
Alisema ili shirika liweze kujiendesha ipasavyo linahitaji wateja waweze kulipia huduma hiyo, hivyo vitendo vya wizi wa umeme vinavyoendelea nchini kwa baadhi ya wateja vinakwamisha maendeleo ya shirika.
"Shirika letu linatoa huduma bora hivyo wateja hawana sababu ya kutafuta huduma kwa njia zisizo halali kama kujiunganishia umeme kinyume na Tenesco na vitendo vingine vya kiarifu,"alisema
Bw. Luwinga alieleza kuwa katika oparesheni hiyo wilaya ya Tameke wamefanikiwa kukagua nyumba za wateja zipatazo 48 na kati ya hizo wateja 11 wamebainika kujihusisha na wizi umeme.
Alisema katika makosa yaliyowahusisha wateja hao ni pamoja na uchezeaji wa mita unaosababisha kupitisha umeme hewa,kujiunganishia umeme kinyume na shirika hilo kwa kutumia vishoka.
Kufuatia makosa waliyokutwa nayo wa hao TANESCO imewakatia huduma ya umeme sambamba na kuwataka kulipa fidia huku wakichukuliwa hatua za kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment