03 October 2012

Kigoda achanua NEC, mchuano bado waendelea


Na Waandishi Wetu

MCHUANO mkali bado umeendelea katika chaguzi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo baadhi ya wagombea waliopewa nafasi ya kushinda, wameangukia pua.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, aliibuka mshindi katika nafasi ya ujumbe wa NEC, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga na kuwabwaga wenzake watatu.

Dkt. Kigoda alipata kura kura 942, Mhandisi Juma Nkondo (75), Bw. Augustino Mwengele (61) na Bi. Hadija Masudi (27).

Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, ilichukuliwa na Bw. Athumani Malunda aliyepata kura 534, akiwabwaga Bw. Saidi Mohamedi Ngole (356) na Bi. Monika Mkwavi (281).

Shinyanga

Mfanyabiashara maarufu mkoani Shinyanga, Bw. Gaspar Kileo ameibuka mshindi katika nafasi ya ujumbe wa NEC baada ya kupata kura zaidi ya 400.

Songea

Bw. Gerold Muhenga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini huku akiwashinda wapinzani wake wawili katika nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo, Bw. Muhenga alipata kura 547, Bw. Golden Sanga (257) na Bi. Eliza Ngongi (37).

Waandishi wa habari hii ni Benedict Kaguo na Joseph Mwambije.

No comments:

Post a Comment