01 October 2012
Uoto wa asili kurejea tena Ukerewe
Na.Jovither Kaijage,
Ukerewe
ENEO la misitu ya halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza lenye ukubwa wa Hekta 1,160.9 uenda likarejea katika uoto wa asili kama ombi la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) la kuindeleza litalidhiwa.
Hayo yameelezwa jana katika kikao cha dharula cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichoitishwa kupokea ombi hilo TFS.
Mwakilishi wa TFS katika wilaya ya hiyo Bw.Ronard Machange alisema kuanzia Julai mwaka huu shughuli za misitu nchini zinaendeshwa na TFS tofauti na hapo awali ambapo ziliendeshwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Alisema katika kipindi kifupi wakala huyo wa huduma za misitu amepata mafanikio makubwa na sasa shughuli zake zinaendeshwa bila kutegemea ruzuku ya serikali .
Aliitaja misitu minne ya halmashauri ya wilaya hiyo ukiwemo wa Itira wenye ukubwa wa hekta 107.2, Negoma hekta 697.7, Kabingo hekta 250 na Mkigagi hekta 116 kuwa tayari imegeuka jangwa na kubaki bila tija yoyote kwa jamii na Taifa.
Akieleza zaidi Machange ambae ni meneja wa ifadhi ya taifa ya msitu wa Rubwa uliopo katika wilaya hiyo alisema TFS inakusudia kuingia ubia na halmashauri hiyo ili kuiboresha misitu hiyo kwa faida ya pande hizo mbili .
Naye Ofisa Misitu na Maliasili wa Wilaya hiyo,Bw.Joseph Song”ola akiwasilisha ombi hilo la TFS alisema kabla ya pande mbili hizo kuingia mkataba baraza la madiwani litakuwa na mamlaka ya kulidhia au la.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw.Vedastus Toto amelitaadhalisha baraza hilo kuepuka dhana potofu zinazoenezwa juu ya suala hilo kwa sababu zinaweza kuwa kikwazo cha kuendeleza rasilimali hiyo muimu.
Mbunge wa jimbo hilo Salvatory Machemli amewataka madiwani kuwa makini wakati wa kuzungumzia suala hilo katika jamiii kwa maelezo kuwa kikao hicho akijapitisha makubaliano ya aina yoyote na TFS.
Alisema baadhi ya viongozi wamekuwa msitali wa mbele kupotosha jamii bila sababu yoyote na kuongeza kuwa kabla ya kuingia mkataba wa kuendeleza misitu hiyo nisharti ipite katika vikao husika kwa faida ya pande mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment