05 October 2012
Hali ya Dkt. Mwanjelwa sasa yaendelea vizuri
Jane Hamalosi na Neema Kalaliche
HALI ya Mbunge wa Viti Maalumu, mkoani Mbeya, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Mary Mwanjelwa, inaendelea vizuri baada ya kuanza kufanyiwa uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam,
Uchunguzi uliofanywa na madaktari wa hospitali hiyo, umebaini Dkt. Mwanjelwa amepata majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa MNH, Bw. Aminieli Aligaisha, alisema Dkt. Mwanjelwa alifikishwa hospitalini hapo juzi na kuanza kupatiwa matibabu.
Alisema mbunge huyo alihamishiwa hospitalini hapo akitokea mkoani Mbeya baada ya kupata ajali mbaya iliyohusisha magari manne, katika eneo la Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 11 na majeruhi zaidi ya 20 ambao baadhi yao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Ifisi, mjini Mbalizi na Hospitali Teule ya Mkoa wa Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment