08 October 2012

Mbunge Mwanjelwa ahamishiwa MOI



Jane Hamalosi na
Neema Kalaliche

MBUNGE wa viti maalum Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi.Mary Mwanjelwa amehamishiwa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) kwa uchunguzi zaidi.


Akizungumza na Gazeti hili ofisini kwake jana Ofisa Habari MOI Bw.Jumaa Almasi alisema hali ya Bi.Mwanjelwa inaendelea vizuri na alihamishiwa katika kitengo hicho jana asubuhi.

"Hali yake inaendelea vizuri ila bado hajaanza kufanyiwa uchunguzi ili aweze kuendelea na matibabu," alisema.

Bi.Mwanjelwa alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili juzi ambapo alipokelewa na madaktari na kuanza kupatiwa matibabu.

Mbunge huyo alihamishiwa hospitali hapo Jumatano wiki hii akitokea mkoani Mbeya  baada ya kupata ajali mbaya iliyohusisha magari manne, katika eneo la Mbalizi Wilaya ya Mbeya vijijini.

Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 11 na majeruhi zaidi ya 20,ambao baadhi yao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Ifisi,mjini Mbalizi na Hospitali Teule ya Mkoa wa Mbeya.

No comments:

Post a Comment