01 October 2012

Wazai washauriwa kuacha ubaguzi

Na Agnes Mwaijega

WAZAZI wametakiwa kuacha ubaguzi,kuzingatia suala la usawa na kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto wa kike ili waweze kuwa na mafanikio na kupambana na chamgamoto mbalimbali za kimaisha.

Hayo yalisemwa Dar es Salaama jana katika mahafali ya 8 ya Shule ya Msingi Maktaba na Afisa Mtendaji wa Kata ya Upanga Mashariki Bi.Oliver Mmwashiuya.

"Naomba wazazi watambue kwamba watoto wa kike nao wana haki ya kupata elimu na kupewa kipaumbele kwa sababu wana mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa," alisema.

Aliwataka wazazi kushirikiana na walimu kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakuwa na mafanikio katika masomo yao na kufikia malengo.


Alitoa wuto kwa wanafunzi hasa wa kike kuwa na bidii na kuacha kuogopa masomo ya sayansi ili idadi ya wanasayansi nchini iweze kuongezeka.

Aliipongeza shule hiyo kwa kuwa na hali nzuri ya kitaaluma na kuwaasa walimu kuongeza bidii zaidi ya kuwafundisha wanafunzi mbinu za kufaulu mitihani yao vizuri.

Awali Mkuu wa shule hiyo Bi.Anna Mshana alisema uongozi wa shule umejitahidi kuweka mazingira bora ya kuwafanya wanafunzi waweze kufaulu.

Hata hivyo alisema bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchakavu wa majengo,ukosefu wa jenfo la utawala pamoja na ofisi za walimu.

Aliiomba serikali na wadu wengine kuendelea kuwatafutia wafadhili na kuwasaudua kuboresha mazingira ya shule hiyo.

No comments:

Post a Comment