08 October 2012
Kukosa uzalendo chanzo cha kutonufaika na rasilimali
Na Agnes Mwaijega
TANZANIA ni miongoni mwa nchi iliyobarikiwa kwa kuwa na rasilimali nyingi na zenye uwezo kumfanya kila Mtanzania akaishi maisha mazuri.
Rasilimali hizo ni pamoja na madini, milima, ardhi, hifadhi za wanyama,mito,maziwa,misitu ya asilina nyinginezo nyingi ambazo kwa ukweli ni hazina ya kutosha kuinua uchumi wa tiafa.
Lakini kutokana na ukosefu wa uzalendo miongoni mwa watanzaia walio wengi rasilimali hizi zimekuwa hazina manufaa makubwa kwetu.
Mara nyingi tumekuwa tukisikia upotevu wa rasilimali mbalimbali za nchi katika maeneo tofauti nchini wahusika wakubwa katika upotevu huo tukiwa ni sisi wenyewe.
Hii inatokana na kutokuwa na uchungu na maendeleo ya nchi yetu hali inayopelekea kuwa wazembe na kutojali hata kidogo ulinzi wa rasilimali za nchi.
Hata hivyo inafahamika wazi kwamba ni suala la ulinzi wa rasilimali ni muhimu kwa maendeleo ya taifa na wananchi wote kwa jumla.
Kwa hiyo ni wazi kuwa hata Jukumu la ulinzi wa rasilimali hizo ni la kila mtanzania ambaye ana uchungu na nchi yake.
Lakini kitu cha ajabu na cha kushangaza asilimia kubwa ya watanzania hatuna kabisa uzalendo na nchi yetu tumeweka mbele maslai binafsi.
kwa mfano tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa zikifnywa nchi na taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali katika maeneo ya kuchimba madini zinaonesha kuwa wahusika wakubwa katika utoroshaji wa madini tena wakati mwingine kwa bei chee ni watanzania wenyewe.
Watanzania wako tayari kupoteza kitu chenye thamani kubwa kwa kuchukua pesa ndogo ambayo kamwe haiwezi kubadilisha mfumo wa maisha yetu.
Kwa upande mwingine hali ya kutokuwa na uzalendo imesababisha kuwepo kwa wageni wengi ambao lengo lao kubwa ni kutuibia rasilimali zetu.
Hali hiyo inadhihirishwa wazi na kuwepo kwa mikataba mingi na kampuni za kigeni hasa katika sekta ya madini ambayo inasababisha ulipaji wa kodi kuwa mgumu.
Katika hilo wapo hata walipewa dhamana ya kulinda na ksuimamia rasilimali hizo lakini hawajali wala kuona umuhimu wa kuzilinda na kuhakikisha zinanufaisha taifa zima.
Mimi naamini kwa asilimia mia kuwa umasikini tunaoupigia kelele unatokana na sisi wenyewe kutokuwa na uzalendo wa kuipenda nchi yetu na kulinda rasilimali tulizobarikiwa na mungu.
Mpaka sasa tumeshapoteza rasilimali nyingi,kwa hiyo ni wazi kwamba tunatakiwa kubadilika na kuwa na uzalendo kuhakikisha kuwa rasilimali zinabadilisha maisha ya watanzania.
Ifike hatua sasa watanzania tuamuke na kuondokana na fikra za karibu ili kuujenga mustakabali mzuri wa taifa letu la sasa na baadaye.
Hakuna mgeni anayeweza kuheshimu na kuonesha kujali ulinzi wa rasilimali zetu kama sisi wenyewe tutapuzia na kujali maslai binafsi.
Tuanpaswa kushirikiana kuwaumbua wote wasio na mapenzi mema na maendeleo ya uchumi wa nchi yetu kwa sababu ni wazi kwamba hawaitakii mema nchi yeu.
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Bw.Stephen Masele alizungumza kwa uchungu mkubwa kwamba anasikitika kuona kwamba watanzania walio wengi wanaoishi katika maeneo ya migodini ndiyo washiriki wakubwa katika kusafirisha madini kwa bei chee.
Inatupasa kujifunza kutoka kwa wenzetu wa mataifa mbalimbali ambao wanajali maslai ya mataifa yao na kulinda rasilimali zao kwa nguvu zote.
Hiyo itasaidia serikali yetu kufikia malengo yake ya mwaka 2020 hadi 2025 ya kuifikisha nchi katika uchumi wa kati utakaowafanya watanzania kuondokana na maisha ya kimasikini.
Naomba ileweke kuwa uzalendo huu wa kulinda rasilimali zetu unapaswa kuanzia kwa viongozi wetu wa nchi waliopewa dhamana ya kuliogoza taifa hili kwa kushirikiana na wananchi na si vinginevyo.
Hii ndiyo njia pekee itayoliwezesha taifa letu kufikia malengo mbalimbali ya kimaendeleo.
Mungu ibariki Tanzania
0717157514
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment