08 October 2012
Diwani aingia mitaani acharaza viboko wanafunzi wazururaji
Na Severin Blasio,
Morogoro
DIWANI wa Kata ya Kichangani katika manispaa ya Morogoro, Bw. John Waziri ameamua kuingia mitaani kutoa mfano wa kufundisha maadili kwa kuwacharaza viboko wanafunziwa shule ya msingi Kichangani waliokuwa wakionekana wakizurura mitaani wakati wa masomo.
Tukio hilo lilitokea juzi saa tatu asubuhi karibu ya nyumba ya wageni ya Zanivina jirani na shule ya msingi Mkwajuni katika Kata hiyo, ambapo watoto hao
walikuwa wakirandaranda mitaani.
Akizugumza na Majira juzi, Bw.Waziri alisema kuwa alifanya hivyo ili kuonesha mfano kwa wazazi wengine ambao wamekuwa wakifumbia macho suala hili huku watoto wakiwaacha wanapoteza maadili.
"Mimi kama mzazi siwezi kufumbia macho suala hilo ..nimewacharaza ili kuwatia adabu
ili kurudisha hadhi ya zamani,"alisema.
Bw. Waziri alisema siku hizi wazazi wamekuwa wakifumbia macho watoto wao wakiogopa
kuwaadabisha kwa hofu yakuwa eti siyo watoto wao wa kuwazaa kitu ambacho kinasababisha mmomonyoko wa madili.
Naye mzazi alishuhudia tukio hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alimpongeza diwani huyo kwa kuonesha mfano na kuwataka wazazi wengine waige.
"Kwa kweli watoto wamezidi sana saa za masomo unakuta wanazurura nafikiri sote tunatakiwa kuiga mfano huu,"alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment