01 October 2012

Wassira sasa amlipua Slaa *Amtaka aache kuita wake za watu chumbani *Dovutwa: CHADEMA inamuogopa Lowassa



Na Mwandishi Wetu, Bunda na Dar

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema watoto wa kaka yake ambao juzi walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi. Lilian na Bi. Esther Wassira, wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa.


Alisema kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod  Slaa kutumia jina na cheo chake wakati akiwapa kadi wanachama hao ni upotoshaji unaofanywa na CHADEMA ili kujipatia umaarufu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bunda, mkoani Mara, Bw. Wassira alimshukia Dkt. Slaa na kumtaka awe makini kuwaita wake za watu chumbani na kuwapa kadi bila maofisa wengine wa chama hicho kushuhudia tukio hilo.

“Namhadharisha Dkt. Slaa kwani alichokifanya kinaweza kuleta mtafaruku katika ndoa za watu, Lilian na Esther ni watoto wa kaka yangu George Wassira si mimi, hawa ni watu wazima na wote wana haki ya kuchagua chama wanachokitaka,” alisema.

Aliongeza kuwa, Dkt, Slaa anaishi kwa kutafuta matukio bila kutumia akili ambapo mume wa Bi. Lilian ni mwanachama wa CHADEMA hivyo uamuzi aliochukua mkewe hauna uhusiano wowote na ukoo wao.

“Hata Makongoro Nyerere awliwahi kujiunga NCCR-Magezui wakati hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (baba yake), akiwa hai, je, tatizo lilikuwa wapi na yeye ni mtu mzima,” alisema.

Alisema siku zote Dkt. Slaa na viongozi wengine wa CHADEMA wamekuwa wakichukizwa na jinsi anavyojibu hoja zao hivyo wanachokifanya ni kumtafutia tuhuma lakini wameshindwa kufanikiwa hivyo wamezna kuwachonganisha katika ukoo.

“Wanachukizwa ninavyojibu mambo yao hasa wanayosema katika majukwaa na kuhatarisha amani, mimi ni mzalendo wa kweli ambaye nalitumikia Taifa lengu kikamilifu na sina tuhuma za ufisadi ambao Dkt. Slaa ameufanya kuwa wimbo,” alisema.

Hata hivyo, aliwataka Watanzania waelewe kuwa ukoo wao msingi wake si vyama vya siasa bali kila mtu ana haki ya kuingia na kutoka katika chama chochote.

Alisema kitendo cha Dkt. Slaa kuhusisha ukoo huo na tukio la watoto hao kujiunga CHADEMA ni kuwadanganya Watanzania kuwa ukoo huo umegawanyika jambo ambalo si kweli.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha United Peoples Democratic Party (UPDP) Taifa, Bw. Fahmi Dovutwa, naye amemshukia Dkt. Slaa kutokana na kauli yake kuwa CCM kinakufa.

Bw. Dovutwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema hivi karibuni, gazeti moja (si Majira), lilimnukuu Dkt. Slaa akisema CCM kimeonesha kila dalili ya kufa baada ya kushindwa kuwaengua wagombea wawili (aliowaita watuhumiwa wa ufisadi), katika nafasi walizowania ndani ya chama hicho.

Wagombea hao ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge ambaye amepitishwa kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

Mwingine ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, ambaye chama chake kimempitisha kuwania ujumbe wa NEC, Wilaya ya Monduli, mkoani Manyara.

“Kauli ya Dkt. Slaa imenishangaza na imevitia doa vyama vya upinzani, yeye hakupaswa kuihadarisha CCM ili isianguke katika Uchaguzi Mkuu 2015, nilitegemea afurahie chama tawala kianguke ili CHADEMA kiingie Ikulu.

“Kutokana na kauli yake, inaonesha CHADEMA kinamuogopa Bw. Lowassa ambaye kama ataamua kugombea Urais 2015, Dkt. Slaa anaamini chama chake hakitafurukuta,” alisema.

Alisema Dkt. Slaa aliamua kuondoka CCM mwaka 1995 na kuhamia CHADEMA ili akajifariji baada ya jina lake kuenguliwa katika kura za maoni mwaka hivyo bado ana mapenzi na chama tawala ndio maana anawajibika kukipa ushauri.

“Ni wazi kuwa Dkt. Slaa hajui chochote kuhusu haki za binadamu kwani katiba ya nchi ya mwaka 1977 ibara ya 13 (6) (b), inasema ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hadi itakapothititika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo,” alisema Bw. Dovutwa.

Alisema kwa mujibu wa kifungo hicho pamoja na Dkt. Slaa kuwataja mafisadi katika Viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, hapaswi kuendeleza tuhuma dhidi yao kwani yeye si polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), wala mahakama.

Bw. Dovutwa alisema inaonesha baada Dkt. Slaa kutoa tuhuma hizo, yeye ndie aliyefanya uchunguzi, kuandaa kesi na kuwatia hatiani.

“Madai ya Dkt. Slaa kuwa kabla hajaondoka bungeni alimwambia Bw. Lowassa kwamba kwa vile amejiuzulu Uwaziri Mkuu kwa madai ya kuwajibika, ina maana alikuwa anamjua aliyesababisha achukue uamuzi huo hivyo alimtaja amtaje ili wamsafishe na kushindwa kumtaja ni siasa za kutishiana ambazo hazina tija.

“Kwa kauli hiyo, baada ya Bw. Lowessa kukataa kumtaja, anachokifanya Dkt. Slaa ni siasa za chuki ambazo haziwezi kukubalika hata kidogo kwa masilahi yake,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ili kujibu madai hayo, Dkt. Slaa aliangua na kusema kuwa “ Mimi sitaki kujibu, waulize waliokuwepo wakueleza kama tulikuwepo peke yetu”.

“Wewe ulikuwepo? alihoji Dkt. Slaa akimuuliza mwandishi wa wetu na baada ya kujibiwa hakuwepo, alisema atafutwe aliyekuwepo ili azungumzie ukweli wa madai hayo.

Akizungumzia madai ya Bw. Duvutwa, alisema kiongozi huyo wa UPDP si saizi yake. “Siwezi kujibizana na mtu ambaye hana hata Mwenyekiti mmoja wa mtaa...nijibizane naye nini? kibinadamu sina sababu ya kumjibu,” alisema Dkt. Slaa.





23 comments:

  1. Hilo zee Slaa hadi umri alio nao hana mke. kwa utamaduni wetu wa Kiafrika hilo ni tatizo. Hivi Watz hamna akili? kwenye katiba mpya mnajadili mambo ya wanasiasa hamjadili kero zenu. hawa wanasiasa wanajaribu kuiteka nyara katiba ili isiwabane pindi wakishika madaraka. hivi unaamini mwanasiasa anaweza kujitia kitanzi mwenyewe? akiifisadi nchi anyongwe? wanawatumia nyie wananchi kuzungumzia mahitaji ya vyama vyao ili wakiingia ikulu iwe pepo kwao. wewe mtanzania amka JADILI:- UADILIFU WA RAIS WAKO AJAE NDANI YA KATIBA MPYA IWEJE. MZINIFU KAMA HUYU SLAA HAFAI KABISA. MAJAJI,MAHAKIMU NA MAWAKILI NAO WAFANYEJWE WANAPOKIUKA TARATIBU ZA SHERIA,TUME YA UTUMISHI IWEJE? NI SAWA MAJAJI NA MWANASHERIA MKUU NA JAJI MKUU KUWA WAJUMBE WAKATI UKIWAPELEKEA MALALAMIKO YAKO HAWASHUGHULIKII SASA UKIPELEKA KWENYE TUME UNAWAKUTA HAOHAO. TUNATAKA TUME HURU YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu naona upeo wako wa kufikiria ni butu mno.Sijui kama Dr.Slaa anazini na mke wako au ni kwa sababu uzinzi ndiyo utajili wa moyo wako.Sisi wenye akili zetu, tusio mbumbu kama ulivyo wewe tunajadili sera(policy issues)wala si ku-attack personalities.

      Delete
    2. Ngoja usifiwe kuwa una akili kutikana na mawazo unayotoa sio ujisifie kusema sisi wenye akili,una akili gani kama hujui hilo zee hadi sasa halijaoa? au anatembea na mama yako hivyo huwezi kumkemea baba yako wa kambo? hivi huji ndoa ya huyo baba yako wa kambo ilipingwa mahakamani? nyie ndio mandondocha mnaofagilia wanasiasa wanaonemeka na ujinga wenu,hivi huji personalities events ndizo zenye taswira ya aina ya mtu? KENGE WEEE

      Delete
    3. fuck u,,, damb ass.

      Delete
  2. The issue is not Dr. Slaa but the deal is the movement for change towards 2015. Politically is not ethical at all to attack a personal directly hence many Tanzanian politicians are wrong since they use to attack personally and not their views. As far as the new constitution is concern, on my view is better to get in touch with the existing constitution in order to reveal the weakens then we can correct and adding new things which will be in our favours.

    ReplyDelete
  3. namuunga mkono dr. slaa kwa sababu zifuatazo:moja ,tulipo sasa ni matokeo ya viongozi wabinafsi na tamaa za ulimbikizaji mali, tuwaulize kina lowasa na wabwekaji wao kama dovutwa na wapiga debe tunaojua wanatoka vyombo vya dola; mbona mmeshindwa kujitakasa kashfa ya richmond badala yake mbinu inatumika kuizima tu bila majibu kuturidhisha wananchi?hamjui watanzania tunajua kuwa kushindwa kwenu kutoa majibu ya kuridhisha ndiko kunafanya tumwamini zaidi dr.slaa kuliko nyie na vyama nyemelezi vilivyoundwa kwa kivuli cha upinzani ili kuhalalisha hujuma mnaotufanyia watanzania wanyonge.vyama vyenu nivyombo vya chama tawalandiyo mnamsakama mpinzani huyu wa ukweli kwa hoja hafifu naisiyo natija, pili, wakina dovutwa na vyama vyao nyemelezi ni wapinzani wa nani?hawajui wanajichora kwa tafiti zao za maprofesa wa uganga wa kienyeji. kama kweli wanajua wanayempinga wafanye kazi hiyo ya kuiamsha usingizini chama tawala, vinginevyo wajiunge nacho waendelee kukumbatia walarushwa na wapokeaji, mafisadi nawahujumu uchumi, waongo na wasingiziajikwa lengo la kulindana ili siku bomu la kuwakataa likilipuka wajipambanue na wanaowapigia debe na si wapinzani.tatu kuendelea na unafiki kunawaumiza wengi na ndiyo chanzo cha hali tulio nayo; watanzania hadi sasa tunashindwa kumweleza MFALME kuwa yuko tupu(UCHI) UNAFIKI HUU NDIYO UNAWAFANYA KINA DOVUTWA washindwe kutoa hojaukweli za kiupinzani badala yake wanajadili watu,komshambulia mwanamapinduzi wa kwelikweli, hatuna viongozi wenye kuumwa na kuwepo nyufa alizotaja baba wa taifa na kusimamiukarabati wa nyufa tajwakwa kusimamia maadili. tunabaki kufumbia macho madhambi ya chama tawala na viongozi wake kwa kuwa mnakula nao na kulala kwao, maogopa kutupiwa virago. hii ni aibu! kubwa! watanzania tunawajua adui zetu wa ndani toka vita vya hayati sokoine vya wahujumu uchumi, hawa niwanafiki wanajifanya wanauchungu na nchi hii huku wakiwanyonya walalahoi jasho lao na kujikusanyia mali ambayo hata ukuwaapisha kwa misahafu gani hawatakuwa tayari kukiri uovu wao ,badala yake wajikinga kwa hoja za kutafuta ushahidi hata kama uhalifu wao unaonekana hadharani,mfano;kina karamagi kusaini mikataba inayonyonya watanzania nchi za nje bado unahitaji ushahidi gani ili asijulikane msaliti wa wananchiwake. je rushwa ya rada nayo inahitaji ushahidi gani kuwapeleka wahusika mahakamani? je usafirishaji wanyamapori kunahitajika mkutano wa mwembeyanga ndiyo waziri awajibike. hapa tunajikanganya wenyewe. wachawi wa hali yetu tunawajua ila tunawaogopa. wapinzani matapeli acheni kufifisha hoja zenye tija. simamieni haki kwani itawasimamia hadi kwenye makaburi yenu. acheni woga wala unafiki , MWAMBIENI MFALME YUKO UCHI, AVAE TUONDOE AIBU YA UMASIKINI!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa watu wa mikoa yenye ushirikina wanafamu majitu ambayo huchukuliwa na wachawi wakafanywa mazezeta,na wewe hapa juu ni kupita zezeta. unawafagilia wanasiasa unaowapenda badala ya kuzungumzia hali halisi ya wanasiasa matapeli katika nchi hii,hivi kweli Mtanzania mwenye akili timamu anaweza kumpa Mbowe au Lema hazina ya nchi na ikapona? Watanzania hatuitaki CCM ambao wamegeuka chama cha kutafutia utajiri na wewe zezeta hebu fikiri hiki chama cha CHADEMA huwa kinachangisha pesa toka kwa matajiri wengi wa mikoa ya kaskazini,nini unategemea kwa hawa matajiri returns zao katika nchi hizi za kiafrika zilizojaa wajinga na mfumo duni wa utawala wa sheria? hamna tofauti kati ya walio CCM na CHADEMA wote hawa baba mmoja mama mmoja ila hapo ni kiasi cha kupokezana vijiti tu cha ulaji. Hebu jiulize ni kwa nini Zitto Kabwe na wenzie walikurupuka kuwaita Bodi ya Tanesco Dodoma kuwahoji sababu ya kumuondoa Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Mr Mhando bila hata kutafakari hata kwa siku mbili tatu ndio wachukue hatua hiyo? hivi kweli kuna mtanzania wa leo atalalamika ukimwambia hata wafanyakazi wote wa Tanesco wafukuzwe kazi? Jiulize ni kwa nini Tindu Lissu analalamikia majaji tu wakati mawakili ndio janga la taifa letu wao ndio driver ya majaji kufanya hovyo. Nyie Watanzania amkeni hawa wanasiasa wananufaika na ujinga wenu na hata ushiriki wao kwenye katiba mpya hawazungumzii mazito ya kuwabana zaidi ya kuwaandikia wafuasi wao nini cha kusema. AMKA WAKATI UNAKWENDA MBELE HAURUDI NYUMA KWA MTANZANIA MNYONGE MWANASIASA NI ADUI YAKO NA AMEKUGEUZA SHAMBA LA BIBI

      Delete
  4. ZEZETA NANI? WEWE UNAYEPIGIA DEBE WEZI WA RASLIMALI ZETU KWA KUWA UNATUPIWA MAKOMBO YAO? UNAFIKI WENU UNAPELEKA NCHI PABAYA KWANI HAMTAKI MABADILIKO,SIMPLY MAKOMBO YATAPUNGUA.SEMA KWELI, WEWE SI USALAMA WA TAIFA? NAKUJUA TENA HADI NYUMBANI KWAKO. USALITI WAKO KWA WANYONGE KWA KUKUMBATIA UFISADI HAUTAKUACHA SALAMA. Nakuhakikishia MWENYEZI MUNGU ATAKULIPA SAWA NA MATENDO YAKO KWETU WANYONGE KWA KUWA UNATUMIKA KUTUNYANYASA....Na leo hii naomba useme ukweli kati ya chadema na ccm nani mchafu mbele ya wananchi? rushwa inayo angamiza haki ya wanyonge inapaliliwa na nani kati ya vyama hivi viwili? kulindana kunakofanywa kwa wahalifu wa watanzania kunakofanywa na ccm wewe hukuoni badala yake unashambulia chadema ambayo haina doa kwakuwa unatolea udenda makombo waliyokula wafalme?! SHAME UPON YOU THE CORRUPT ELEMENT! SITAKUHUKUMU LAKINI NAAMINI KATI YA WATAKAOONJA MOTO WA MUNGU KWA KUKUMBATIA DHULUMA, NA WEWE UTAKUWA KUNI AU MKAA KUWACHOCHEA WANAOTUDHULUMU WANYONGE KWA MIKATABA MIBOVU RUSHWA NA UFISADI. ACHA KUWAONEA CHADEMA,HAWAJAWA NA DHAMANA NA MATATIZO LUKUKI YANAYOTUKABILI, WAAMBIE WATAWALA KUWA WAKO UCHI ILI WAVAE NGUO! KAMA UKO SERIOUS NA SHIDA ZETU ACHA PROPAGANDA CHANGIA MADA USICHANGIE MTU,TUSIJE TUKAKUWEKA KUNDI LA WENYE MAWAZO......KWANI WAO HUJADILI WATU NA MATUKIO! KAMA WEWE UNAVYOFANYA. UKIENDELEA HIVYO DAWA YAKO NI NDOGO, TUTAKUPUUZA>

    ReplyDelete
    Replies
    1. NEVER ARGUE WITH A FOOL PEOPLES MIGHT NEVER NOTICE. ARE YOU SURE YOU KNOW THIS GUY. DO YOU HAVE GOD POWER TO KNOW WHO IS WRITING HERE,THIS IS THE TYPE OF ZEZETAS WE HAVE IN OUR COUNTRY.MAY BE YOU HAVE A DEGREE FROM UNIVERSITY. PLEASE GOD I DONT KNOW TO WHAT TO ASK YOU ABOUT THESE TYPE OF PEOPLES

      Delete
    2. what the heck r u talking about,,, jack rabbit?

      Delete
  5. Wewe unayetetea ccm msenge nyie ndo wezi pumbavu na nyamafu.Miaka 51 ya UHURU HATUONI HAUWENI YA mAISHA UNATETEA CCM,UNA AKILI WEWE AU UNAFIR...NA CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. what u r language.

      Delete
    2. usiilaumu ccm kutokana na hali mbaya ya maisha uliyonayo.Mlaumu Mamayako kwa kukubali kuolewa na mwanaume fukara na ndiomaana hauishi kulalamika na kulia maisha magumu.

      Delete
    3. tuache kutukana tuchangie mawazo, kama chama chenyewe ni cha kutukana, basi tuachane na chama hicho maana hawana maadili

      Delete
  6. Baba yako alikuwa analala na mbuzi sasa mmesomeshwa baada ya uhuru mnaona hakuna kilichofanyika,mmezoa kunya kwenye misitu bila kuchamba na hapa mjini mnakunya kwenye rambo mnatupa popote tu,sasa kweli utaona miaka hamsini ya uhuru ni bure tu

    ReplyDelete
  7. Huna cha kuongea? Tunataka kiongozi msomi anayejua nini afanye pia mwenye msimamo kama Dr na chama chake. Kuoa kutooa si kitu mwanaume mwanaume tu anayetakiwa ni mwanaume wa kweli. Nafurahi Dr kukaribisha na sio kukaribishwa. Kiongozi mwanamapinduzi ndo tunayemtaka sio kiongozi jina CCM toka mwanzo mlishindwa kuleta mabadiliko leo mtaweza? Mambo ya kifamilia unayachanganya na maendeleo ya Nchi kweli wewe mzima? Hospitali za vichaa zipo kwa ajili ya watu kama wewe nakushauri uwahi kupata tiba pia usisahau kutembea na kamba kwani itakusaidia na kusaidia watakaokuwa karibu nawe kukukamata na kukufunga pale yatakapochemka . Maisha mema Mr. President Slaa (Dr. Slaa)

    ReplyDelete
  8. Lazima useme hivyo pengine wewe mtoto wa haramu,hivyo kuona baba aliyemkaza mama yako hakukosea kwani ni mwanaume. Uzinzi siyo sifa katika dini wala mila. hivyo uadilifu wa mtu pia huangalia kazaa nje ya ndoa? lakini wewe pia sikushangai maana ni mtoto wa haramu na pengine humjui baba yako kutokana na mama yako kutembea hovyo na wanaume,hivyo mama yako akiambiwa hiyo ni tabia mbaya utasema ni mambo ya kifamilia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani hata kama kuna maneno ya malumbano ni lazima mtumie lugha ya kueleweka mkiwa watanzania wenye akili timamu. Nadhani nyie ni wasomi wambao mnategemewa pengine kuwepo kwenye nyadhifa za juu sasa mkianza kurushiana maneno mnadhani jamii inachukua picha gani? Kuweni na lugha za kuongelea

      Delete
  9. ooh please Tanzanians!!what the hell are you talking, its time to think instead of talking what ccm or chadema are doing.We need peaceful politics and not words of challenging one another in bad language.Come down and speak sense in these newspapers.From now on wards I expect to read good articles on this newspaper. Thanks is me Bobjossy.

    ReplyDelete
  10. ebu kuweni wazarendo

    ReplyDelete
  11. ebwana wee munabishania nini jama?hii nchi haitokua namaendeleo mpaka ipate rais dictator,i believe madictator wanawapenda wananchi wao.cause kama nikusoma na sera wagombea wote hawamuingii profesa lipumba bt tz tunashindwa kumtumia.to hell vyama vyote atokee dictator ashike nchi

    ReplyDelete
  12. swala la kuoa ni la hiari ndugu zangu, hakuna nchi/taifa lolote linaloweza kumshinikiza mwananchi wake kuoa/kuolewa. Namaanisha kuwa mhe slaa ana uamzi wa kuishi na mke au la.

    ReplyDelete
  13. WASIRA WEWE NI UPEPO WA MAJANI MAKAVU KWA DR. SLAA WEWE MUDA WOTE BUNGENI UMELALA. WAZIRI WA MAHUSIANO MBONA HULETI MAHUSIANO MAZURI KISIASA NA KIJAMII HAPA NCHINI UNACHOCHEA CHUKI HALAFU ANGALIA UZINIFU WAKO NA WA DR. SLAA NANI MZINIFU ZAIDI BE A LOGICAL LEADER AND NOT EMOTIONAL LEADER. JE WAZIRI ASIYE NA WIZARA MAALUMU ANAFANYA KAZI GANI?JE ANATENGEWA BAJETI?JE WAZIRI MKUU NA YEYE WANA TOFAUTI GANI?KIFO CHENU CCM KITAKUWA KIBAYA. DAWA YENU 2015

    ReplyDelete