08 October 2012
Gama, Marealle, Chilolo waibuka kidedea CCM
Heckton Chuwa, Moshi na
Damiano Mkumbo,Singida
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bw.Leonidas Gama, Mkurugenzi Mtendaji wa Executive Solutions, Bw. Aggrey Marealle na mwanasheria maarufu Bi.Elizabeth Minde ni baadhi ya wanachama wa CCM, walioibuka washindi katika uchaguzi mkuu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini.
Katika uchaguzi huo, Bw. Gama alipata kura 514 na kuwa mmoja wa wajumbe watano watakaoiwakilisha Wilaya ya Moshi Mjini katika Mkutano Mkuu wa CCM Taifa. Wengine waliochaguliwa kuwakilisha wilaya hiyo ni Bw.Edmund Rutaraka, Bw.Jacob Mbasha, Bi. Consolata Lyimo na Bi.Florence Mushi.
Katika kinyang’anyiro cha uenyekiti wa wilaya Bi. Minde alishinda nafasi hiyo baada ya kupata kura 479. Katika kinyang’anyiro cha mjumbe wa NEC, Bw. Marealle aliibuka kwa kura 321.
Katika uchaguzi huo, Bw. Paul Matemu alichaguliwa bila kupingwa kushika wadhifa wa Katibu wa Uchumi na Fedha wakati Diwani Priscus Tarimo alichaguliwa kuwa katibu wa Itikadi na Uenezi.
Mkoani Singida Mbunge wa Viti mkoani hapa, Bi. Diana Chilolo, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoani baada ya kujipatia kura 432 kati 451 na kuwaacha wagombea wenzake kwa mbali.
Bi. Chilolo alipata ushindi huo wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo, uliofanyika Mjini Singida juzi. Ushindi huo mkubwa ulipokelewa kwa shangwe na wajumbe.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkuu Dkt.Parseko Kone, aliwataja wengine waliochaguliwa ni mjumbe moja wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Bi. Sara Mkumbo, na mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa Bibi Fatuma Taofiq.
Mkutano huo pia uliwachagua wajumbe 10 wa Baraza kuu la UWT Mkoa. Waliochaguliwa Bi. Rehema Chima, BiMagareth Mlewa, Bi. Debora Ituka,Bi. Salimu Kundya, Bi. Maria Lyimo na TBi. Tatu Daghau.
Wengine ni Elilumba Lula, Bi.Monica Samweli, Bi. Asharose Matambe, Sara Mkumbo, Mariam Kahola na Helena Kitila.
Kwa upande wake Bibi Jenny Kishari, ambaye anakuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Mkoa. Kwa upande wa uwakilishi wa Jumuiya ya Umoja wa vijana CCM, Bi. Janeth Mughwai,aliibuka mshindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment