08 October 2012

Aliyegombea udiwani 2010 CHADEMA ahamia ADC


Na, Zubeda Mazunde

ALIYEKUWA mgombea wa udiwani wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mwaka 2010 Bi.Sudi Ally Tamu amejiunga na chama kipya cha Alliance for Democratic Change (ADC) na kurudisha kadi ya chama hicho.

Akikabidhi kadi hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa ADC uliofanyika Buguruni Malapa Dar es salaam alisema kuwa alianza kujiunga na siasa mwaka 1995 na alijitoa CHADEMA mwaka 2010.

Bi.Tamu alisema kuwa aliamuwa kujitenga na chama hicho kwa sababu hakina ushirikiano katika kazi,kutodhamini watu wa chini na kujikita hasa kwenye familia zao.

Hata hivyo aliendelea kutoa sababu zilizosababisha  aondoke kwenye chama chake ikiwa ni pamoja na kutosaidiwa na uongozi wa chama hicho alipokuwa akigombea nafasi hiyo.

"Mimi kama mwanamke nilijitahidi sana kutangaza chama cha demokrasia na maendelao CHADEMA pamoja na viongozi wa chama hicho,nilikuwa na utubiwa vijiji 14 katika kitongoji, lakini cha kushangaza wabunge walivyopata uongozi hawakunishukuru wala kunipa ahsante wala kunithamini," alisema.

Pia alizitaja sababu zilizomfanya ajiunge na chama cha ADC kwamba sera ya chama hicho, kinajali na kudhamini watu wa kima cha chini ikiwa ni pamoja na walemavu wa aina zote.

"Hivyo basi kwa kuwa nina uzoefu wa kutosha wa siasa ninachukuwa kadi ya kujiunga na chama cha ADC na ninaahidi kushirikiana nao bega kwa bega," alisema.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa chama cha ADC Bw.Kadawi Lucas Limbu alisema wameanzisha chama hicho kwaajili ya manufaa ya wananchi na kusaidia watu wenye ulemavu pamoja na watu wasiojiweza hususani wanawake.

Bw.Limbu aliwataka wananchi kutambuwa uwepo wao katika vyama vya siasa, kwani hakuna idara ya Katiba ya chama iliyotambua uwepo wa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa sababu ya kuanzisha chama kipya ni kuelimisha jamii, kutambuwa haki za walemavu pamoja na za watanzania huku wakiahidi kuwa wakipewa kibali na uongozi wa serikali watafanya usafi katika kijiji cha malapa ili kuepuka magongwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Kwa upande mwingine wa Mwenyekiti wa ADC Taifa Bw.Saidi Miraji Abdulah aliwaasa Watanzania kuchagua chama ambacho kitakuja kuleta mafanikio na sio majungu yasiyo kuwa na mafanikio.



No comments:

Post a Comment