04 October 2012
ATE yataka waajiri kushiriki kutathmini tuzo mwajiri bora
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wajiri Tanzania (ATE), kimewataka waajiri kushiriki kufanya tathmini kuhusu tuzo ya mwajiri bora mwaka 2012 ambapo shindano hilo litadumu kwa miezi miwili na nusu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dkt. Aggrey Mlimuka, alisema kampuni au asasi zitapata fursa ya kujipima na kujiweka kwenye kiwango kinachofaa.
Alisema lengo la shindano hilo ni kutoa hamasa kwa waajiri waweze kuendeleza utendaji bora katika nyanya ya raslimali watu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji mali.
“Washiriki watapata fursa ya kushirikiana, kujifunza, kujilinganisha na kujiweka katika kiwango kinachofaa kiutendaji hasa kwenye rasilimali watu na sera za biashara, mifumo na vitendea kazi,” alisema Dkt. Mlimuka.
Aliongeza kuwa, tuzo ya mshindi itatolewa Desemba mwaka huu ambapo wanachama wa ATE wanaruhusiwa kushiriki bila malipo.
“Shindano hili hutoa fursa sawa kwa wote hivyo ATE inahimiza wanachama kushiriki kwani kutamwezesha mwanachama kuona umuhimu wa kushiriki na inasaidia kuonesha umuhimu wa wanachama kujali utendaji bora ndio maana mwaka huu washiriki wote watatunukiwa vyeti,” alisema.
Aliongeza kuwa, makundi ya mwaka huu yameboreshwa baada ya kufanyika marekebisho makubwa katika shindano hilo ambalo lilianza mwaka 2005.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment