01 October 2012

Wateja Vodacom kubonga bila mipakaNa Mwandishi Wetu

WATEJA wa Kampuni ya Vodacom wameendelea kunufaika na gharama nafuu katika kupiga simu bila ya kuwa na hofu ya gharama za muingiliano wa kupiga simu kwenda mitandao mengine.


Ikitekekeza kwa vitendo kauli mbiu ya kazi ni kwako sanjari na kutoa huduma zenye kukidhi mahitaji na matakwa ya mteja, kampuni ya Vodacom Tanzania imekuwa ya kwanza sokoni hapa nchini kushusha kwa kiwango cha juu kabisa cha asilimia hamsini gharama za upigaji wa simu ambayo ni Shilingi moja na senti hamsini kwa sekunde.

Kabla ya hapo mteja wa Vodacom alikuwa akipiga simu kwenda mitandao mengine kwa Shilingi tatu kwa sekunde.

“Dira ya Vodacom ni kuwawezesha Watanzania wote kuwa sehemu ya mafanikio ya uwepo wa teknolojia ya simu za mkononi nchini bila kujali tofauti ya vipato” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania

“Tutazidi kuwa mbele katika kutoa huduma bora na nafuu zaidi kuwawezesha wananchi kutumia kiasi kingine cha fedha katika shughuli nyengine za kuboresha maisha yao,"alisema Bw.Rene Meza

Akizungumzia zaidi huduma ya BONGA, Bw. Meza amesema kuwa kampuni yake inajitahidi kadri inavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wake na sasa kupitia laini moja ya simu mteja ataweza kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Sasa mteja wa Vodacom anaweza Kubonga bila kubadilisha laini yake ya simu, pia mteja anaweza  kuendelea kutumia huduma nyingine kama M-Pesa , Intaneti, na huduma nyinginezo kupitia Vodacom bila kubadilisha laini yake ya  simu,”

“Sekta ya mawasiliano imekuwa sana na watu wengi sasa wanategemea mawasiliano ya simu katika kuwasiliana kibiabiashara, kifamilia kirafiki. Ili kuunga  mkono maendeleo hayo wateja wetu lazima wawe sehemu ya mafanikio hayo.” Alisema Bw. meza

Ili mteja wa Vodacom kubonga bila mipaka ya gharama anajiunga kwa kupiga *149*01#

Kupunguzwa kwa gharama za upigaji simu katika Vodacom kutoka mtandao mmoja kwenda mitandao mingine inakwenda sanjari na ofa mbalimbali kutoka katika mtandao huo kama ofa ya vifurushi vya cheka vinavyomuwezesha mteja kujiunga na intaneti na kupiga simu ndani ya mtandao wa Vodacom kwa bei nafuu zaidi.


No comments:

Post a Comment