08 October 2012

Mnyika apinga kauli ya Waziri Mukangara


Na Anneth Kagenda

MBUNGE wa Jimbo la Ubungo,Bw. John Mnyika ametoa wito kwa vijana kote nchini kutokubaliana na utaratibu uliotangazwa kuhusu maadhimisho ya wiki ya Taifa ya Vijana badala yake wafanye shughuli zao za kuwaingizia kipato.


Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Bw. Mnyika ilisema kuwa yeye akiwa mmoja wa vijana wa Tanzania na mbunge kijana hakubaliani na utaratibu mzima ulivyopangwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara.

Alisema utaratibu huo ulitolewa kwa kutoa ratiba ya maonyesho na maadhimisho mengine bila kueleza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwa vijana katika maadhimisho kama hayo mwaka 2011

"Natoa mwito kwa vijana katika maeneo
mbalimbali nchini kutokubaliana na utaratibu huo wa kuweka kipaumbele katika maonyesho zaidi badala yake wafanye maadhimisho kwa kuweka kipaumbele masuala na matukio yenye kugusa maisha ya vijana na mustakabali wa Taifa," alisema. 

Pia alisema vijana akiwamo  yeye watumie wiki hiyo kutafakari masuala ya msingi baina yao ili waweze kutimiza wajibu, lakini wakati huo huo wazifuatilie mamlaka zingine zinazohusika na masuala ya vijana kwa upande wao ikiwemo serikali katika ngazi zote.
  
Alisema pia ieleze kuhusu masuala ya ajira,na kwamba ilipendekezwa bungeni na Wizara ikakubaliana nao kuanzisha Benki ya Taifa kupanua wigo wa ajira kwa vijana nchini.

"Lakini pia kuweka mkazo kwenye maonyesho katika Mkoa mmoja badala ya masuala na matukio muhimu yenye kugusa maisha ya vijana katika maeneo mbalimbali nchini mijini na vijijini ndio jambo la muhimu," alisema na kuongeza;

 
Kuhusu masuala ya ajira,aliseka kuwa walipendekeza bungeni na Wizara ikakubaliana nasi kuanzisha Benki ya Taifa ya Vijana ili kuwezesha vijana wasioweza kumudu masharti ya kibenki katika mfumo wa kawaida wa kibenki kuweza kupata mitaji kwa masharti nafuu kwa ajili ya kujiajiri.


No comments:

Post a Comment